Yanga na teams zote za ligi kataeni huu upuuzi

Yanga na teams zote za ligi kataeni huu upuuzi

Ila yanga mna lawama ambazo hata hamfikirii kwakweli, game ya yanga vs azam, kuna miujiza niliona, lakini sijaona yanga wakilaumu , lile goli walofunga azam hahahahahaha , refa kagoma eti faulo khaaa!! Emu vibanzi vyetu tuvipeleke pande zote!! Timu inacheza judo uwanjani kwanini refa asitoe faulo, cha msingi jipangeni msimu ujao ili mje mchukue kombe !! Makocha wanaojua mpira wala huwa hawalaumu!!
 
Hakuna kitu kibaya kama kutaka matokeo yako kichwani ndio yawe.
 
Sio kazi ya TFF, Bodi ya Ligi au Marefarii kuzijengea uwezo baadhi ya timu kuchukua ubingwa. Uwezo unatokana na maandalizi ya kila timu moja moja, kuanzia usajili hadi training. Kumbuka mlivyokuwa mkibeza bajeti ya bilioni 1.3, mnadhani mambo yanajiendea kwa mazoea tu? Watu wamewekeza, viongozi wa timu hizo za Kagera Sugar na Lipuli pia wakitafuta fedha za kutosha maandalizi kama ya Simba, watatoa ushindani hadi wa kubeba ubingwa, na wala sio ajabu. Mbona Azam amebeba ndoo, tena zote ya Bara na ya Kagame Cup? Kwa kuwa aliwekeza katika usajili na uendeshaji. Yanga ilikuwa inagoma kufanya uchaguzi, sasa nani atawapa malezi wachezaji, kocha? Yaani kocha ameajiriwa uje umtegemee ndio awabembeleze wachezaji wasigome? Yanga mkubali kuwa hamkuwa na kikosi kizuri kama Simba, na hamkuwa na viongozi wazuri kama Simba
soma uelewe grounds za posts zangu hapo juu ...budget kubwa ya simba itumiwe in right ways...tunahitaji fairness kwenye ligi tupate ligi bora yenye ushindan itakayotupatia team bora ya taifa
 
Sportpesa hujabeba, FA hujabeba, mapinduzi hujabeba na ligi hujabeba.unatembeza bakuli.

fikiri kwa kichwa na si matako.

Kama mapungufu yapo ni muda sana hayajaanza sasa.
 
Au Mpira ukaendelea huku kipa ameumia [emoji23][emoji23][emoji23]. Daah, comedy indeed
Naona amekuteka akili na wewe umetekeka! Akiwa peke yake kabisa mbali kabisa na wachezaji wote, kipa kaenda kuokoa back pass mbali na goli lake karibu na kibendera ili isiwe kona, akaupiga ukatoka nje ukawa wa kurushwa. Yeye kwa ile kasi ya kuuwahi usiwe kona, alipitiliza halafu akiwa nje ya pitch akaendelea kukaa chini huku lango likiwa wazi. Simba wakarusha mpira haraka haraka, ikapigwa ndefu golini, ikaunganishwa kwa kichwa. Kipa kuona ameboronga, akajilaza kabisa eti aliumia. Sasa mchezaji upo nje ya pitch, nani asimamishe game wakati hakuna uhakika kama umeumia au umeona utachelewa kurudi langoni?
 
Sioni tatizo la Simba SC kuendelea kuchukua ubingwa.Yanga is too corrupted.
 
Sportpesa mmekosa.
F.A mmekosa
Mapinduzi mmekosa
Kagame Cup mmekosa
TPL mmekosa

Ina maana hata Sportpesa mlikoseshwa na TFF ?
Ambao hawakuhusika na chochote...!

Wacheni visingizio.
Chezeni Mpira
Mshinde mechi zenu.
 
Naona amekuteka akili na wewe umetekeka! Akiwa peke yake kabisa mbali kabisa na wachezaji wote, kipa kaenda kuokoa back pass mbali na goli lake karibu na kibendera ili isiwe kona, akaupiga ukatoka nje ukawa wa kurushwa. Yeye kwa ile kasi ya kuuwahi usiwe kona, alipitiliza halafu akiwa nje ya pitch akaendelea kukaa chini huku lango likiwa wazi. Simba wakarusha mpira haraka haraka, ikapigwa ndefu golini, ikaunganishwa kwa kichwa. Kipa kuona ameboronga, akajilaza kabisa eti aliumia. Sasa mchezaji upo nje ya pitch, nani asimamishe game wakati hakuna uhakika kama umeumia au umeona utachelewa kurudi langoni?
refa ndiyo boya..alitakiwa asimamishe mpira angalie mchezaji ana tatizo gan, hii ligi mchezaji atakuja kufa kizembe kwa uboya wa marefa wa usimba na uyanga
 
Ushabiki tuweke kando, ligi yetu ya Tanzania bara ipo corrupted, kuanzia daraja la kwanza ndiyo madudu kabisa, ligi kuu bingwa anaandaliwa kabla ligi kuchezwa

Tatizo lipo TFF, nachelea kusema bodi ya ligi au chama cha marefa....sababu TFF wanajua kabisa madudu ya hizi idara na wana mandate ya kuzivunja wapo kimya.

Ushauri wangu kama hakutatokea mabadiliko kwenye hizo sehemu hapo juu...tutegemee simba kuchukua ubingwa misimu yote mpaka mabadiliko ya uongozi wa TFF, chama cha waamuzi na bodi ya ligi vipo corrupted.
Acha upuuzi huo na usipotoshe watu....najua we ni shabiki na mwanachama nguri wa yanga thus unaumia simba sports club kuchukua ubingwa mara mbili mfurulizo.

YANGA imechukua ubingwa mara nne mfulilizo hakuna aliyelalama kutoka na uwezo wa wachezaji na timu ilivyokuwa imejizatiti kuwa na wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa compare na timu zingine.

SIMBA nayo tumeona uwezo wake kwa misimu yote miwili ni club yenye vijana wanaopiga mpira mzuri wa kisasa na imewekeza pesa nyingi na imefanikiwa kuonesha kiwango cha hali ya juu ndani na kimataifa.hayo unayozungumza ni maneno ya mkosaji tu.
 
refa ndiyo boya..alitakiwa asimamishe mpira angalie mchezaji ana tatizo gan, hii ligi mchezaji atakuja kufa kizembe kwa uboya wa marefa wa usimba na uyanga
Lakini inaweza ikawa ni ujanja wa golikipa kwa kuwa aliona ametoka golini
 
jiulize kwanini referees waliochezesha matches za yanga walifungiwa...na kwanini wasifungiwe waliochezesha matches za simba?.....hiyo ni evidence tosha ya hayo yote nliyoyaongea hapo juu

Unaongea vitu usivyovijua plus ulimbukeni na ushabiki uchwara!
Marefa waliochezesha mechi ya simba na kmc wapo wapi?...
Huna evidence yoyote ya maana zaidi ya ushabiki maandazi!
Kama kweli una evidence kwamba hakuna refa aliyechezesha mechi za simba na akafanya makosa lakinihakuchukuliwa hatua kakate rufaa...
 
tatizo TFF inaipendelea Simba wazi wazi, mpira wa tanzania ngumu sana kuendelea
 
Naona mnapoteza muda kubishana na masabiki wa Yanga. Tatizo ni Mwinyi Zahera kila akishindwa anawaaminishwa mashabiki wa Yanga kuwa wameonewa. Sasa hii kitu imeingia kwenye vichwa vya masahabiki wengi wa Yanga. Hawaamini bado kama Simba tayari bingwa wanabaki kulalamika tu kama kocha wao. Hivi unaweza kuwa bingwa kweli kipa Kindoki, beki Juma Abdul, Kiungo Makapu na Buswita, Fowadi Matheo Anthony na Tambwe?

Na hili TFF inabidi wawe makini sana kwenye ligi ijayo. Kwani haya malalamiko ya uongo yakiendelea sana mwisho wake watu wanadhani ni kweli. Ona sasa kila shabiki wa Yanga anaamini kuwa Yanga ilistahili kuwa bingwa kwa sababu tu Mwinyi Zahera aliwaaminisha kuwa wanaonewa.

Kiukweli Yanga walikosa ubingwa kwa sababu kuu mbili. Moja ni kikosi kutokuwa kipana wakitokea majeruhi timu ilikuwa inayumba sana. Mbili kitendo cha kumfukuza Kakolanya na kutegemea Kindoki na Kambwili wawavushe lilikuwa ni kosa kubwa sana la kiufundi. Lakini haya Zahera hawezi kuwaambia mashabiki wa Yanga kwa sababu Kindoki kamleta yeye.

Lakini kikubwa kwa mashabiki wa Yanga ule wimbo uliovuma sana wa kila mtu ashinde mechi zake halafu mahesabu yafanyike mwisho wa ligi mbona umsahaulika mapema badala yake mbnaanza wimbo mpya?
 
Naona amekuteka akili na wewe umetekeka! Akiwa peke yake kabisa mbali kabisa na wachezaji wote, kipa kaenda kuokoa back pass mbali na goli lake karibu na kibendera ili isiwe kona, akaupiga ukatoka nje ukawa wa kurushwa. Yeye kwa ile kasi ya kuuwahi usiwe kona, alipitiliza halafu akiwa nje ya pitch akaendelea kukaa chini huku lango likiwa wazi. Simba wakarusha mpira haraka haraka, ikapigwa ndefu golini, ikaunganishwa kwa kichwa. Kipa kuona ameboronga, akajilaza kabisa eti aliumia. Sasa mchezaji upo nje ya pitch, nani asimamishe game wakati hakuna uhakika kama umeumia au umeona utachelewa kurudi langoni?
Mkuu kwa maelezo yako pia bado mpira hautakiwi kuendelea km alikaa chini unless na ww umekosea kunhadthia maana binafsi sjashuhudia
 
Komaeni na hali zenu, wakati ukifika mkawa na hela nunueni na nyee, pumbuless fc
 
Back
Top Bottom