Yanga ni bingwa 2023, ni darasa kwa wadau wote wa mpira nchini

Yanga ni bingwa 2023, ni darasa kwa wadau wote wa mpira nchini

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mpira ni uwekeaji, uongozi wa vijana na usajili wa vijana wenye vipaji. Mpira unachezwa na vijana hivyo huwezi kuwa na viongozi wa mpira wazee waongoze mpira.

Mpira sio ulozi na mizengwe bali sayansi ya mpira kama kama waliyonayo Nabi na kaze.

Mpira ni coordination ya wadau wengi, sio mtu mmoja kama Rais wa timu, msemaji, wachezaji, TFF, board ya ligi, serikali wala mashabiki na wanachama TU. Timu zetu lazima na mtu anaeratibu nafasi, maoni na kazi za wadao wote wa mpira.

Mpira ni mradi wa wazi kabisa usiokuwa na makandokando, lazima kila hatua iwe ya wazi ili wadau wakupe inputs zao. Usiwachukie wanaokukosoa hata kukuzomea unapofanya vibaya bali fanyia kazi kile Cha ukweli na puuzia lile la uongo.

Timu zetu nendeni kajifunzeni kwa akina Yanga ili nchi yetu ipige hatua kisoka tusiishie kutaniana na kuchukiana TU.
 
Back
Top Bottom