Yanga SC 0-0 Club Africane | CAF Confederation Cup | Mkapa Stadium

Yanga SC 0-0 Club Africane | CAF Confederation Cup | Mkapa Stadium

Kunguru akikunyea si kwamba ana shabaha mechi haijaisha hii, hawa tunawapelekea moto nyumbani kwao. Achaneni na makolo wachawi wakubwa hao
Kama wewe kweli mwamba usiishie kuwa shujaa kwa maneno matupu, hiyo hata mimi naiwezi

Could you put your money at stake?

Beti tuone huo umwamba unatokea wapi
 
Byutiiiiiiiii byutiiiiiiiiii.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hivi ulozi huvukagi mipaka?
Huyu mzee afukuzwe yanga na sio Nabi🤣

Screenshot_20221102-192529_Instagram.jpg
 
Fujo za Utopolo hizi
Kitimu kidogo badala ya kujitafuta kupambana uwanjani kujiweka kwenye nafasi nzuri ndio kwanza kimeanza na vurugu

CAF wakikapiga rungu na mafaini kibao lawama ziende kwa Karia tena?
 
Bado, save hii comment, vile vifo unavyovisikia vya mkanyagano kwenye nchi za wenzetu mtakuja kuvishuhudia live Tanzania, naandika kitu ninachokijuwa vizuri.

Hizi timu mbili zinamilikiwa na Ccm na imefaulu kuwapumbaza Watanzania.
Ofsa mbona unatutisha?

Unataka wote tuwe na siku mbaya wakati wewe na timu yako ndio mmepata matokeo mabovu?
 
Hii ni improvement kubwa kwa Yanga mwaka jana alicheza mechi mbili za mashindano na alipoteza nyumbani na ugenini lakini mwaka huu amecheza mechi tano mpaka sasa ameshinda mbili, ametoa sare na suluhu 2 amepoteza moja!!! Tuwe na shukran na kila hatua tunayopiga jamani sisi binadamu!!
Halafu hawa ni vigeu geu

Kipindi wanatoa sare na Al Hilal hapa si walikuwa wanasema Al Hilal timu kubwa na ndio maana walikutana na ugumu huo

Sasa kama umekubali kuwa mpinzani wako ni mkubwa, nafasi ya kumpa lawama kocha hapo inatoka wapi?
 
Sasa imagine msimu huu Yanga ndio INA kikosi bora kabisa kuwahi kutokea, kwa hili siku za Nabi kuwa Yanga zinahesabika, kiu ya Wana Yanga ni international games ambazo kimsingi zimemshinda.
Yanga ina kikosi kizuri kuliko Simba, ila sijui nini huwakuta kimataifa
 
Sasa nimejua kwanini Nabi alifurushwaga kula Al merikh ya Sudani.
Abaki hapa aifunge simba na Geita kwa msaada wa marefa.
Wana unbeaten lakini bado hawana furaha

Hiyo tu inatosha kuwapa majibu uwalakini wa hiyo unbeaten
 
Hata kama Mkuu. Kwa kikosi tulichonacho hatupaswi kuwa tia maji tia maji bana.
Kikosi gani mlichokuwa nacho chakufanya mjutie sana sare ya leo?

Ni hiki hiki kilichocheza leo au kingine mmekihifadhi stoo?
 
Mmeganywa mkakubali kugawanyika, kamwe Watanzania hawatokaa wajitambuwe na Ccm itatawala milele.

Siku utakayogunduwa siri ya Simba na Yanga zinamilikiwa na nani ndio utajuwa kumbe hujui vitu vingi sana nchi hii.

Simba na Yanga mmiliki wake ni mmoja.
Kumbe umezunguka kote huko lakini hoja yako kumbe iko hapa?

Hilo ni sawa tunajua namna CCM inavyotumia hizi timu kama fursa kwenye agenda zao

Na sio Simba na Yanga tu, kuna vitu vingi ambavyo wanaweza kuzitumia kama mbinu

Kwa kulijua hilo, basi sioni mantiki yeyote ya kuona mijadala ya Simba na Yanga ndio njia pekee ya kututoa kwenye reli na kutuondolea fokasi yetu kwenye yale maswala ambayo wo wameyalenga

Ingefungwa Simba leo hii sidhani kama ungekuja na hoja hii

Kwa hiyo mambo ya siasa hayawezi kutuzuia sisi kujadili mambo ya soka katika namna yeyote ile
 
Daah Yanga mnavunja moyo sana daah sina hamu kabisa kuwashabikia.
Mnakubalije kuwa wa mchangani siku zote.
Wanaume wanaupiga mwingi kimataifa ninyi mmeridhika mchangani? Aaaaah.

Inatosha
Pole sana Arajiga atafuta kilio chako
 
We ndiyo umeongea pointi,Yanga akiendelea hivi misimu mitatu mfululizo atafika mbali
Kipindi sisi tunapigwa goli 5, wo walikuwa wakwanza kuchekelea

Na sisi hatukukata tamaa kwasababu tulijua malengo yetu kuyafikia ni lazima ukutane na majabali kama hayo

Wao wametoa sare tu tayari wamepoteana, huko mtunis akipiga jackpot hali itakuwaje?
 
Back
Top Bottom