Yanga SC 0-0 Mbeya City | Benjamin Mkapa | NPL

Yanga SC 0-0 Mbeya City | Benjamin Mkapa | NPL

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City, mchezo umeshaanza kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

YANGA 0-0 MBEYA CITY - FULL TIME

Dk 1: Timu zimeanza kwa kusomana, matokeo ni 0-0.
Dk 5: Mchezo una kasi na timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dk 10: Mashambulizi ya zamu kwa timu zote, Mbeya City wanaonekana kufunguka.
Dk11: Winga wa Yanga, Moloko yupo chini, anapewa matibabu baada ya kuumia.
Dk 17: Zawadi Mauya wa Yanga anapiga shuti kali kutoka nje ya 18, kipa wa Mbeya City, Deo Munisha anapangua na kisha kuudaka.
Dk 18: Mchezo una kasi, Mbeya City hawaonyeshi dalili ya kukaa nyuma kuzuia, Yanga nao wanatengeneza mashambulizi mdogomdogo.
Dk 20: Kasi ya mchezo inatulia kidogo.
Dk 23: Yanga wanawapa presha Mbeya City.
Dk 25: Yanga wanapata kona lakini hawaitumii vizuri.
Dk 28: Yanga wanafika langoni mwa Mbeya City mara mbili lakini mipira inaishia kwa kipa Deo Munishi.
DK 30: Dickson Job wa Yanga anafanya kazi nzuri ya kuzuia mashambulizi ya Mbeya City.
Dk 31: Yanga wametulia na kumiliki mpira muda mwingi.
Dk 35: Saido anachezewa faulo nje ya eneo la 18, inakuwa faulo.
Dk 36: Saido anapiga inagonga ukuta na kuokolewa.
Dk 40: Mchezo bado ni wa kushambuliana kwa zamu.
Dk 45: Kipa wa Yanga yupo chini ameumia na anapatiwa matibabu.
Dk 45+5: Licha ya kuongezwa dakika 3 lakini bado mchezo unaendelea

Dk 45: MAPUMZIKO

Dk 46: Kipindi cha pili kimeanza.
Dk 49: Yanga wanaumikili mpira muda mwingi lakini safu ya ulinzi ya Mbeya City inakuwa ngumu.
Dk 50: Saido anapambana kutafuta nafasi lakini anakutana na upinzani mgumu.
Dk 55: Mbeya City wanarudi nyuma kidogo na kuwapa nafasi Yanga kuuchezea mpira.
Dk 63: Yanga wanaendelea kuonyesha kuwa imara hasa sehemu ya kati.
Dk 67: Yanga wanafanya shambulizi kali, Mayele anashindwa kutumia nafasi nzuri aliyopata kutoka kwa Aucho.
Dk 70: Yanga wanapata faulo karibu na lango la Mbeya City.
Dk 71: Saido anapiga lakini inaokolewa.
Dk 75: Kasi ya mchezo imepungua kiasi, timu zote zikipambana kutafuta nafasi ya kufunga.
Dk 76: Zawadi Mauya anacheza vizuri na Farid Musa lakini mpira unapotea.
Dk 77: Mayele anabaki na kipa lakini mwamuzi anapuliza filimbi kumaanisha ni faulo kwa Mbeya City.
Dk 86: Presha ni kubwa kwa timu zote, lakini Yanga ndiyo wanaonekana kuwa na presha ya kuafuta ushindi.
Dk 90: Mbeya City wanachelewesha kuanza mpira.
Dk 90: Yanga wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.
Dk 90: Mwamuzi anamaliza mchezo matokeo ni 0-0.
FULL TIME
 
Habari,

Haya sasa leo ndio siku ya Mabingwa wa Kihistoria nchini Tanzania watashuka dimbani kuwakaribisha Mbeya City katika dimba la Benjamin Mkapa saa moja kamili usiku.

Hadi muda huu Dar Young Africans wenyeji wapo juu kabisa katika msimamo wa league wakiwa na point 35 na Mbeya City wakiwa nafasi ya Nne wakiwa na point 22.

yangasc-20220205-0001.jpg
 
Saa 1:00 usiku vinara Yanga SC watakuwa katika dimba la Benjamin Mkapa kumenyana na Mbeya City.

Yanga wanataka alama tatu ili kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wakati Mbeya City nao wanataka alama tatu ili kupanda mpaka nafasi ya tatu.

Tuwe pamoja Hapa JF kwa Live Updates

Kikosi Cha Yanga Kinacho Anza Leo

View attachment 2109148
 
Back
Top Bottom