OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
YANGA YAACHANA NA KOCHA NASREDDINE NABI.
Taarifa rasmi zitakuijia hivi punde. Usiondoke
Anaandika Jemedari Saidi
Habari za uhakika zinasema Kocha NASRIDEEN MOHAMED NABI maisha yake na Yanga SC yamefikia tamati na ataondoka muda wowote.
Pamoja na mambo mengine lakini usajiri wa baadhi wa mastaa unahusishwa, huku ikisemekana kwamba aligomea kwa kutoa sababu za kiufundi. Nabi pia anahusishwa na magomvi na wasaidizi wake kwa muda sasa na misimamo mikali.
Kwenye soka sajili zingine ni "Political Signings" ambazo wakubwa ndiyo wanajua zaidi kwanini wanamtaka Kisinda, Morrison au Makambo kwa mfano, kuliko vile Kocha anavyotaka.
Kwahiyo kocha kuleta mambo yake ya kiufundi ni kutaka kuchelewesha maisha kuwa mepesi na kuyatia ugumu.
Kocha wa Vipers ya Uganda Mbrazil Roberto Oliveira anahusishwa na kuchukua nafasi ya Nabi ambaye ameiongoza Yanga SC kwenye michezo 43 ya Ligi Kuu bila kupoteza.
Mechi ya Derby ilikuwa ndiyo njia rahisi kumuondolea kama Yanga wangepoteza lakini mechi ikaisha kwa sare. Kama atafika salama mechi dhidi ya Club Africain itakua mtihani mkubwa sana kwake, asipotoboa hana chake. Waswahili wanasema 'Kamba hukatikia pabovu
Credit: Bin Kazumari