Tetesi: Yanga sc Kushusha Mbadala wa Aucho

Mkuu, Asante sana.
Ila naomba nikurekebishe hakukosa fainali ya pili, alikosa fainali zote mbili kwa sheria ya CAF.

Fikiria mtu anafanya kosa la kuigharimu timu wakati ambao team inaongoza kwa Aggregate ya 3-0 ugenini, tena nusu fainali na ni dakika za mwishoni hapo mahesabu yote ni fainali.

Anatokea mjinga mmoja anampiga makusudi mwenzie na mpira nje ya uwanja, wakati anajua ana kadi 2 za njano tayari!

Hao wanaoongea nimewaacha tu, sitaki ubishani kwakuwa nafahamu ninachozungumza.

Hakuna mechi yoyote ya Yanga niliyoikosa msimu wote uliopita iliyochezwa Dar, sio ligi sio klabu bingwa wala shirikisho.
Huyo Aucho namjua vya kutosha, na nilikuwa namkubali kuliko wao.
Ukiona mpaka nafikia kusema hivi ni wazi amefikia kiwango cha mwisho cha makosa ya kizembe.

Kwa akili ya kawaida tu, kwanini huo uamuzi wa usajili wa mbadala wake uje sasa? Ni kwamba hadi ngazi ya uongozi wa klabu wameshaona hatari ya Aucho kuigharimu timu wakati huu ambao timu inasaka rekodi mpya.
 
Aucho alikera sana hio siku , sijui alikua kavuta majani gani
 
Nilikuwa shabiki mkubwa wa Aucho ila utovu wa nidhamu awapo uwanjani umenivunja moyo.

Anafanya makosa ambayo huwezi kuyategemea kutoka kwa mchezaji pro kama yeye, mbadala wake sio mjadala tena... anahitajika haraka.
Wewe hujui mpira nini? Uliwahi kuwaona Patrick Vieira na Riy Keane? Jwa kiungo mkabaji siyo rahisi kutopata kadi.
 
Mimi nililia Mkuu. Niliwaambia kabisa niliokuwa naangalia nao kwamba tunaenda kupoteza fainali, pengo la Aucho ni kubwa sana.
Nadhani njia iliyosahihi ni kupata mtu sahihi wa kusaidiana na Aucho maana ukichana na mambo ya kinidhamu kuna kuumia pia ukiangalia Yanga ni Aucho, kuhusu kupata kadi za kizembe hilo ni jambo lisilokwepeka kwake kwasababu ni moja ya madhaifu yake ni kutokuwa na ustahimilifu pindi ukimkwaza hyo ni asili yake hata aambiwe vipi itakuwa ni jambo gumu kwake kuji control labda kama atasidiwa na watalaamu wa saikolojia. Hakuna jambo gumu uwanjani kama ku control temper huku damu ikiwa inachemka mwilini.

Baada ya mechi kuisha kule Africa kusini, wachezaji wote walikuwa na furaha wakishangalia kufuzu fainali ila ni Aucho pekee hakuwa mwenye furaha wakati wote alionekana hayupo sawa, moyoni mwake alijutia kosa alilolifanya. Tusifikie kumchukia huyu ndiye mwamba wa pale Jangwani anayejua ili Yanga iondoke na kitu uwanjani lazima yeye avuje jasho na apambane kwa asilimia mia.
 
Sidhan kama anachukiwa, anachopaswa ni kubadilika mpira wa kisasa ushavuka kwenye mambo ya kihuni yaliyopitiliza ambayo ameyafanya kwenye mechi na coastal .
Kupata kadi kwa kiungo wa chin si jambo la kushangaza lakin kupata kad ya nje ya mchezo ni upumbavu na kosa ambalo linaweza kukufanya usisajiliwe na Tim kubwa.. tulete mtu wa kumsaidia na yeye abadilike
 
Mpira tumecheza. Mtovu wa nidhamu ni mtovu wa nidhamu tu. Mstaarabu ni mstaarabu tu. Mwaka jana kwa nini Aucho alimpiga na mpira mchezaji wa Malumo wakati hata hakukua na sababu ya kufanya hivyo, ndiyo damu kuchemka?

Lile pengo la Aucho lilionekana kwenye fainali ya kwanza. Kocha kaliona hilo ndio maana anataka mbadala wake.
 
Aucho hana makosa km unavoyakuza, ni normal na kakosea match chache sn.
Lkn mbadala ni kuongeza ubora tu.
 
Nadhani hujui umuhimu wa Aucho, kuna muda anakosa nidhamu ila kumkinai bado sana. Huduma yake ni ya muhimu mno haimbwi sana ila ni mtu kazi kweli kweli. Kumpata mbadala wake sio rahisi hata kidogo.
 
Aucho hana makosa km unavoyakuza, ni normal na kakosea match chache sn.
Lkn mbadala ni kuongeza ubora tu.
Ndo shida ya mashabiki hiyo. Ukiwa unasikia na kusoma maandishi tu unaweza kufikiri labda sasa Aucho atakuwa kazi yake uwanjani ni u-mwakinyo tu mpira hachezi, wakati ndo engine ya timu yake.

Hata baada ya Yanga kupigwa na Ihefu kuna mtu alikuja humu mbio na uzi wa kulalamikia ufupi wa Diarra, akasisitiza kuwa kipa huyo hafai, aletwe mwingine! Na supporters wa hoja yake aliwapata humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyekuambia anaondoka ni nani?Anatafutwa mbadala kwa maana ya backup ikitokea hayupo katika mechi fulani.
 
B... ukishaona timu inamtegemea mchezaji mmoja, basi ujue ni ya kawaida sana hiyo. Haijajiweza bado ila mbwembwe tu.

Ova
Kumbuka mbadala wa Aucho kwa misimu miwili nyuma alikuwa ni Yanick Bangala.Sasa Yanick Bangala kaondoka na nafasi yake ajaletwa kiungo mwingine.
 
Hilo ni sawa lakini kusema atupishe hapo kapuyanga pakubwa
 
Umesema vyema, kama timu fulani kumkosa mchezaji mmoja ndani ya dakika chache wakafungwa goli 4!
Mbwembwe ni nyingi kuliko uhalisia b…
[emoji23][emoji23][emoji23]ume muweza[emoji2772][emoji2772][emoji2772]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…