Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Mkuu, Asante sana.Mnao mshambulia Nifah nadhani hamuelewi au mnajilazimisha kutokuelewa kwa ajili ushabiki maandazi uliowajaa. Msiwe na akili kama makolo bana, Aucho hana nidhamu na ni mwepesi kujaa upepo kitu ambacho sio sahihi kwa mchezaji wa level yake na umuhimu alionao kwenye timu yetu. Alikosa fainal ya pili dhidi ya USMA kwa ajili ya tukio la kipuuzi ila pia juzi kati dhidi ya Coastal almanusura ale umeme kwa ajili ya upuuzi. Badala acheze rafu zinazookoa timu anaenda kuwapiga watu viwiko mpira ukiwa umesimama, huyu ni proffessional au mswahili tu flani wa mpira wa vichochoroni?
Ila naomba nikurekebishe hakukosa fainali ya pili, alikosa fainali zote mbili kwa sheria ya CAF.
Fikiria mtu anafanya kosa la kuigharimu timu wakati ambao team inaongoza kwa Aggregate ya 3-0 ugenini, tena nusu fainali na ni dakika za mwishoni hapo mahesabu yote ni fainali.
Anatokea mjinga mmoja anampiga makusudi mwenzie na mpira nje ya uwanja, wakati anajua ana kadi 2 za njano tayari!
Hao wanaoongea nimewaacha tu, sitaki ubishani kwakuwa nafahamu ninachozungumza.
Hakuna mechi yoyote ya Yanga niliyoikosa msimu wote uliopita iliyochezwa Dar, sio ligi sio klabu bingwa wala shirikisho.
Huyo Aucho namjua vya kutosha, na nilikuwa namkubali kuliko wao.
Ukiona mpaka nafikia kusema hivi ni wazi amefikia kiwango cha mwisho cha makosa ya kizembe.
Kwa akili ya kawaida tu, kwanini huo uamuzi wa usajili wa mbadala wake uje sasa? Ni kwamba hadi ngazi ya uongozi wa klabu wameshaona hatari ya Aucho kuigharimu timu wakati huu ambao timu inasaka rekodi mpya.