SI KWELI Yanga Sc yaachana na Kocha wake Mkuu Nasreddin Nabi, leo Oktoba 25, 2022

SI KWELI Yanga Sc yaachana na Kocha wake Mkuu Nasreddin Nabi, leo Oktoba 25, 2022

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kuna tetesi zimeibuka leo 25/10/2022 zinadai kuwa Yanga imeachana na kocha wake Mkuu Nasreddin Nabi. Tetesi hizi zimeshika kasi baada ya kuchapishwa na Gazeti la Mwanaspoti pamoja na kutumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mpaka kufikia saa saba mchana Uongozi wa Yanga, umeendelea kuwa kimya na kutokuwa tayari kulizungumzia suala hilo, hata walipotafutwa wamesema Nabi bado ni kocha wa timu hiyo hadi hapo itakaptangazwa kivingine.

1666678097371.png
 
Tunachokijua
Klabu ya Yanga imekanusha taarifa za uvumi kuhusu kuachana na kocha wake Mkuu zilizoanza kusambaa mitandaoni kuanzia kumalizika kwa mechi na watani wao Simba.

Uongozi wa Yanga unapenda kuwataarifu mashabiki na Wanachama wake kuwa Nasreddin Nabi, bado ni kocha mkuu wa timu yetu.

Nabi alijiunga na Yanga April, 2021 na amekuwa na rekodi nzuri ya kuiongoza timu yetu kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, bila kupoteza.

Akizungumza na YANGA MEDIA, Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine amewaomba mashabiki na wanachama wa Yanga kufuatilia taarifa za uhakika za timu yao kupitia vyanzo rasmi vya habari vya klabu.

“Niwaombe mashabiki na wanachama wetu kuwa na utaratibu wa kufatilia taarifa za klabu yetu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari.

“Tuna YANGA APP. Tuna Website ya Young Africans na kurasa zetu za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikitoa taarifa za klabu yetu na kwa wakati sahihi,”
alisema Andre.
Back
Top Bottom