Yanga tukatae Uhuni wa GSM huko mbeleni tutajuta

Yanga tukatae Uhuni wa GSM huko mbeleni tutajuta

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
GSM Waliokuwa Home Shopping Centre ni wahuni toka Serikali ya Kikwete. Hawa tunawafahamu walikuwa wakifanya uhuni kukwepa kodi, baadaye alipoingia Magufuli madarakani walijifanya wamefilisika na kubadili jina luwa GSM.

Ni wahuni toka zamani na wezi wakubwa. Hawa wamekuja ichukua team yetu kinyemela nasi kwa kuwa mzee wetu Akilimali hayupo hai tumeshindwa kulitambua hilo.

GSM wanasajili team yao. Hawasajili team ya Yanga. Wanasajili team yao wakiiweka ndani ya Yanga. Huu ni Uhuni ambao tunapaswa wanayanga kuukemea.

Hakuna mtu anayefahamu kwa sasa viongozi wa Yanga wanahusika na nini. Ni kama GSM imechukua team na kuifanya yao. Tunaomba kama wanaitaka watumie taratibu ionekane ni wawekezaji au basi wainunue tujue moja.

Angalieni wenyewe hata usajili unavyofanyika. Naenda kufanyikia sijui nyumbani kwa anayesajili au sijui qapi ambako huoni hata nembo ya klabu yetu pendwa.

Uhuni wa mikataba walifanya hata kwa Tshishimbi. Walisema amesajiliwa na kurusha videos kumbe hakuwa amesajiliwa. Wameendelea mpaka kugushi barua ya Sure Boy kwenda Azam.

Hawa jamaa hawana nia njema na soka letu. Hawana nia njema na klabu yetu. Kama haki ingetendeka jana kwa suala la Morrison sisi tulitakiwa kunyang'anywa points za mechi zote alizocheza. Kuna watu walitakiwa kushtakiwa kwa kosa la kughushi mkataba.

TFF wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite. GSM ni mwanaharamu.


Screenshot_20200812-231452~2.png
 
Hapo kwenye points ni kweli kabisa kombe lilifunikwa na ni bora Morrison aende kuliko point hata 1 kwenda.
Gsm hata kama wana hela club ianze kuwatilia mashaka janja janja pale iko mingi sana.
 
Wewe binafsi..umechangia kiasi gani kwaajili ya usajili wa club yetu pendwa mkuu
 
Mkuu inawezekana usemalo ni sahihi... But. The reality is yanga wanahitaji mwekezaj mwenye pesa... Bila hilo hakuna litakalofanikiwa yanga zaid ya maneno tu... Duu umasikini unaweza sababisha ukauza hata mkeo ili usiaibike.....
 
Ninyi ndo huwa mnaolewa familia mzima na mtu ambaye amemwoa dada yenu.mnajikuta tu wewe,wadogo zako wazazi wako wote mnaenda olewa na jamaa hata kama anamtesa dada yenu mnasisitiza dada asioñdoke sababu nanyi mtakosa pa kwenda.jamaa ataanza kutembea na ninyi mmoja mmoja mnafurahia tu.

Wewe una mchango upi kwenye timu? achana kauli za kimaskini, mpira ni pesa sio maneno ya kipumbavu
 
Maana ya hizi picha ni kwamba wakati Team nyingine wanasainia kwenye club husika pamoja na matangazo ya club husika,wale wa Yanga wanasainia kusikojulikana, yaani hawataki hata Logo ya Team ionekane,hebu amkeni kuna kitu hakiko sawa hapo nahisi mleta uzi yuko sahihi
 
Maana ya hizi picha ni kwamba wakati Team nyingine wanasainia kwenye club husika pamoja na matangazo ya club husika,wale wa Yanga wanasainia kusikojulikana, yaani hawataki hata Logo ya Team ionekane,hebu amkeni kuna kitu hakiko sawa hapo nahisi mleta uzi yuko sahihi
Watakua wanasainia Sebuleni kwa Engineer Hersi
 
Wewe una mchango upi kwenye timu? achana kauli za kimaskini, mpira ni pesa sio maneno ya kipumbavu
Tatizo lako haujui thamani yako kama mashabiki ndio maana kwa uwelewa wako unasema huyo mtoa mada kachangia shiling ngapi. Klabu ya Yanga na mashabiki wake wanathamani kubwa sana kuliko hao GSM. GSM wanawahitaji nyie zaidi na ndio maana wapo hata wasemwe kwa mabaya. Angalia hata kwa Simba mo hata asemwe vipi ataendelea kung'ang'ania kuwepo coz anafaidika na Simba. Simba na mashabiki wake wanathamani kubwa kuliko mo.. narudia hujui thaman yako km mashabiki wa Yanga.
 
Una point halafu yule engineer ni muongeaji sana kuliko vitendo
 
Hapa kitu cha msingi tupange kuandamana mpaka kwenye club yetu.hatuna imani na mwenyekiti
 
Haya mapungufu ya kusajili wachezaji bila nembo (banner) ya mfadhili na ya Yanga kuwepo tuliyapigia kelele sana hapa jamvini naona sasa wameanza kujirekebisha. Hata jambo la mfadhili kusajili mwenyewe nyumbani kwake halafu anakwenda kuwabwagia viongozi wachezaji nalo naona ameanza kuliacha. Walau sasa tunaona kwa hawa wachezaji waliosajiliwa mwishoni hapa kuna bango nyuma ya mchezaji na hata viongozi wanakuwepo.

Walau kidogo sasa viongozi wa Yanga watakuwa na nguvu juu ya maamuzi ya wachezaji kuliko ilivyokuwa kabla ambapo wachezaji walikuwa wanamheshimu mfadhili halafu wanadharau viongozi. Tokea mwanzo huyu mfadhili angewashirikisha viongozi nina uhakika asingepata aibu ya mwaka na ule ubatizo wa moto aliobatizwa na Morison kwani mnapokuwa wengi na uzoefu tofauti lazima tu mapungufu kwenye ile mikataba yote miwili ya Morison yangeonekana na kurekebishwa kwa wakati kabla ya kusainiwa.

Yote kwa yote pamoja na mapungufu yote hayo ya mfadhili lakini lazima tumpongeze kwenye usajili alioufanya hadi sasa na hasa iwapo atampata Larry Bwalya maana huyu jamaa ni mashine sawa sawa na Chama. Timu iliyomaliza ligi ilikuwa dhaifu mno walau hii iliyosajiliwa inaonyesha mwanga wa mafanikio huko mbele.
 
Haya mapungufu ya kusajili wachezaji bila nembo (banner) ya mfadhili na ya Yanga kuwepo tuliyapigia kelele sana hapa jamvini naona sasa wameanza kujirekebisha. Hata jambo la mfadhili kusajili mwenyewe nyumbani kwake halafu anakwenda kuwabwagia viongozi wachezaji nalo naona ameanza kuliacha. Walau sasa tunaona kwa hawa wachezaji waliosajiliwa mwishoni hapa kuna bango nyuma ya mchezaji na hata viongozi wanakuwepo. Walau kidogo sasa viongozi wa Yanga watakuwa na nguvu juu ya maamuzi ya wachezaji kuliko ilivyokuwa kabla ambapo wachezaji walikuwa wanamheshimu mfadhili halafu wanadharau viongozi. Tokea mwanzo huyu mfadhili angewashirikisha viongozi nina uhakika asingepata aibu ya mwaka na ule ubatizo wa moto aliobatizwa na Morison kwani mnapokuwa wengi na uzoefu tofauti lazima tu mapungufu kwenye ile mikataba yote miwili ya Morison yangeonekana na kurekebishwa kwa wakati kabla ya kusainiwa.

Yote kwa yote pamoja na mapungufu yote hayo ya mfadhili lakini lazima tumpongeze kwenye usajili alioufanya hadi sasa na hasa iwapo atampata Larry Bwalya maana huyu jamaa ni mashine sawa sawa na Chama. Timu iliyomaliza ligi ilikuwa dhaifu mno walau hii iliyosajiliwa inaonyesha mwanga wa mafanikio huko mbele.
Lini wamejirekebisha?
 
Back
Top Bottom