rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Tatizo ni wanachama, wapenzi wana uchungu mkubwa kuliko wanachama lakini wanachama wana uwezo mkubwa wa kubadirisha hivi vilabu lakini wanaangalia maslahi yao binafsi.Issue kubwa ni weledi kwenye club zetu hizi. Ukiwaangalia viongozi wa club zetu hizi hawana nia ya kuzifanya kuwa na tija. Ukiwauliza wanasema shida ni pesa, hivi unakampuni au biashara inayopendwa kama simba na yanga unakosaje hela? Ukiwa na t shirt za kawaida tu 100000, ukaziuza kwa kawaida tu, unakaribia b,Zahera aliwaonyesha pia, watu wanapenda club zao, ukiwaambia wachangie wanachanga. Viongozi wanashindwaje kuleta wachezaji watano bora, wakigeni,nasema bora nikimaanisha bora kutoka ligi bora afrika. Waungane na wazawa bora wakachukua kombe la Africa na hivyo wakapata pesa? Au wakachukuwa vijana wadogo maeneo mbalimbali wakawalea wakawauza? Hivi viongozi gani hawa tulio nao?
Hivi inakuaje jezi za simba na yanga zinauzwa kienyeji badala ya kuuzwa kwenye maduka yanayotambulika. Hapo kuna ujanjajanja unaofanyika ndio maana wameruhusu hivyo.