Yanga tumejifunza nini na uwezo wa kocha wa simba?

Bila kujari wewe ni Yanga fan au ni Kolo FC kikubwa umeongea point... Inabidi tulifanyie kazi hili maana unaonesha kutupenda sana Wananchi japo wewe ni Kolo😆 ili tuendelee kuwapakuwa Kila tukikutana
 
Mwisho wa siku kolo akafa[emoji23][emoji23]acheni kujifariji
 
Kimsingi kocha kaibadilisha simba kwanza namna inavyopress na spidi imeongezeka tofauti na mwanzo,DM akipatikana na wakiweza kumchezesha yule zungu mashabiki hoyahoya watatulia
 
Na kuichukulia uto poa
Tatizo kubwa la kocha wa Simba ni sub aliyofanya. Kumtia Kanoute, chama na Kibu. Hawa walikuwa ameubeba mchezo pale Katikati. Kanoute alikuwa anaharibu sana pale Katikati, chama alikuwa anapenyeza. Kibu alikuwa na power, nguvu
 
Kimsingi kocha kaibadilisha simba kwanza namna inavyopress na spidi imeongezeka tofauti na mwanzo,DM akipatikana na wakiweza kumchezesha yule zungu mashabiki hoyahoya watatulia
Kabisa mi kwa kile kikosi sikutegemea ,nlichojifunza ni wachezaji walicheza kitimu

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Yeah sub ya kanoute ilitokana na kadi yake ile ya njano aliyopata ila kati tulikua tumewazidi...nina uhakika mechi ijayo tunawafunga

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Simba ilikuwa afe nyingi siku ile. Basi tu.
 
Simba walifanya uzembe upi? Vp Yanga haikufanya uzembe Simba kupata goli kipindi cha kwanza??

KOLO unajifanya YANGA.
Shida yako mada ya mbinu na ufundi unataka kuijadili kimahaba. Jaribu kufatilia vyema humu, mimi ni mshabiki wa Yanga niliyeanza kuupenda mpira kabla ya kupenda timu.

Simba waliizidi Yanga kimbinu kipindi cha kwanza chote, Simba wakipoteza mipira walikuwa wanawahi sana kurejea umiliki, pasi zao zilikuwa zinafika, wakapiga mipira mingi ya hatari golini kwa Yanga.

Wachezaji wa Yanga walikuwa hawawezi kufikisha hata pasi kumi mipira mingi ilikuwa inaporwa ama kupiga pasi mbovu. Timu ya Yanga ilizidiwa kipindi cha kwanza na wala sio swala la uzembe. Bahati ya Nabi ni Simba kutopata magoli mengi kipindi cha kwanza.
 
Ww jamaa lini ukawa yanga siku zote ni kuinanga yanga.
 
Ndio maana yake, kwamba ili ufungwe lazima ufanye huo uzembe au makosa.
 
Sasa kama Yanga alizidiwa kipindi cha kwanza kihivyo kwa nini sasa Simba hakupata magoli mengi kipindi hicho basi.

Mnachambua baadaye mnaharibu kwa kuleta ushabik.
 
Acha upimbi wewe, sasa nani alitakiwa kujifunza kwa mwenzake pale? AZIZ KI peke yake alitengeneza Chance za magoli 4 ambapo 1 ilikuwa goli, 2 Mayele alikosa, na moja Morrison alikokota kubwa.

YANGA HAINA LA KUJIFUNZA LOLOTE KWA MAANA SIMBA ALIZIDIWA KILA MAHALI ILE GAME, MFUMO WA SIMBA ULIKUWA 4-2-3-1 kwa akili yako huo mfumo ni wa kushambulia au Kuzuia??

Haya lete hapa takwimu za chance ambazo zilikuwa created na SIMBA siku ile zaidi ya YANGA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…