Yanga tumrudishe Zahera kikosini

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kama tumeweza kumrudisha Lamine kikosini sio vibaya kumrudisha Zahera. Kimichezo mapungufu ya Zahera ni madogo kuliko mazuri yake.

Hatutajuta kama tutamrejesha Zahera kikosini.
 
Ngoja wanakuja Gongowazi wenzio.
Huenda nikaambulia matusi lakini huo ndio ukweli wenyewe. Ni vigumu Sana kumpata kocha mwenye kiwango cha Zahera ambae anafundisha national team ya taifa ambalo liko mbele kwenye mpira kuliko Tanzania. Congo sio wajinga hata kidogo kumtumia Zahera kuifundisha timu Yao ya Taifa.

Makosa ya Zahera yanafahamika na yanavumilika. Uwezo wa Zahera kashauonyesha kwetu kuwa anaweza pamoja na kufundisha wachezaji waliokuwa na manung'uniko mengi ya fedha zao na stahiki zao mbalimbali.
 
Ushemeji na kujuana kulisababisha Zahera akaondoka.

..........Timu ilikuwa na wakati mgumu lakini Zahera alipambana ikashika nafasi ya pili, Wacha tuone Mzee wetu ataifikisha wapi timu msimu huu.

..............Nakupenda Yanga.................
 
Mkuu sorry,kwani makosa ya zahera ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkwasa anatosha sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zahera ni kocha mzuri na ni mvumilivu sana. Anajua sana saikolojia ya wachezaji na namna ya kuwavusha wachezaji kwenye mechi ngumu hata kama timu ina uwezo wa wastani.

Tatizo la Zahera ni kuongea sana na vyombo vya habari hata mambo ambayo ni siri ya klabu yeye atayapeleka hewani "live" bila chenga. Udhaifu wa Zahera unakuja pale anapoona kisemeo "mic" yeye huwa hajali ni nani anamhoji hata ikiwa Maneromango TV yeye yumo tu. Kwa Yanga kumrudisha itakuwa ngumu kwani baada ya kumvunjia mkataba alipita vyombo vya habari karibu vyote bongo kuwasema vibaya Yanga.
 
Kama tumeweza kumrudisha Lamine kikosini sio vibaya kumrudisha Zahera. Kimichezo mapungufu ya Zahera ni madogo kuliko mazuri yake.

Hatutajuta kama tutamrejesha Zahera kikosini.
Labda baadae....kama kuna uhitaji wake, kwa sasa atafute timu nyingine yy bado ni kocha bora..

Kumbuka Yanga ni kubwa kuliko hata Ndg. Mwenyekiti wa Yanga.

Weka hii akilini..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wewe ni baba na unafamilia na unakuwa na mawazo kama haya......jitafakari sana
Bahati mbaya au nzuri rekodi za Mh. Mkwasa za ufundishaji kabumbu tunazo na zinafahamika, maana alikuwepo na yupo sasa. Alifundisha Yanga na hata Timu ya taifa bila kuacha rekodi ya kupigiwa mfano. Wote ni mashahidi wakati Zahera alipokuwa akihangaika na akina Kakolanya, Yondani, Dante na wangine na kuinusuru timu kuangukia nafasi 2 kwenye ligi. Katika hali kama ile wallah kama kocha angekuwa mtu wa kawaida tu timu ingeshuka daraja
 
Anzisha timu then Zahera yupo available kabisa utampata,we wachezaji aliokuja nao Zahera na kuwasajili msimu huu uliwaona au game plan ya Zahera ulikuwa unaona timu inachokifanya?

Kisa Zahera alikuwa anatoa hela zake ndiyo abaki tu hata kama ubora hauonekani uwanjani?

Bora tuwe hata wa kumi,ila Zahera aliishiwa pumzi kabisa
 
Hata wewe mwenyewe unafahamu kuwa anadanganya, Zahera kapoza mechi moja na kutoa sare mechi moja sawa na Simba yenye kikosi kipanda na jeuri ya fedha pia imepoteza mechi moja na kutoka sare moja, hiyo punzi aliishiwa lini? Zahera alicheza mechi kadhaa za champion league tofauti na Simba waliotolewa mechi ya kwamnza tu na UD Songo. Wewe kaka utaishi maisha mabaya sana hasa kwa uongo. Molinga kaletwa na Zahera na ndiye tegemeo la Mkwasa sasa, au huoni?
 
Kama hujui mm ni mmoja wa watu waliokuwa wanamtetea Mwinyi Zahera,achana na hizo story zako za Simba haziihusu yanga,kwanza alianza kujiona yupo juu ya timu,baada ya afcon badala ya kuja kuandaa timu akaenda kwao wakati alijua mashindano yamebadirika,amekuja kwenye mechi za ushindani kwa kubahatisha tukaitoa rollers.Kumleta Molinga ndiyo excuse ya kuendelea naye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…