Yanga tusipokuwa makini na suala la likizo tutaukosa ubingwa mapema

Fundi kipara

Senior Member
Joined
Oct 27, 2019
Posts
125
Reaction score
247
Salam wananchi, natumai hamjambo na mnaendelea na majukumu ya kulijenga taifa la mama kizimkazi. Naomba kusema kitu japokua roho na nafsi vinauma.

Viongozi wa team yetu pendwa ya Young African kuna sehem wana shida kubwa sehem sana kuhusu suala la kutoa likizo kwa wachezaji nyota katika tena wachezaji hao wakipewa likizo pia huchelewa kuripoti kambini.

Niwakumbusheni kuhusu suala la Key Master (Aziz Stephanie) amekua ni mchezaji mwenye shida hio na suala hili viongozi wetu wa ngazi za juu wamekua kimya sana sio msimu huu tu ata msimu jana alifanya hivyo lakini kama viongozi hawajapata dawa ya tatizo lake?

Nashangaa kutomuona kwenye pitch super captain (Nondo) yuko wapi, mbona waliocheza AFCON wengine wanahudumu kwenye club zao? Hamad Ibra Bacca ndio kaoa na kaacha mpira kabisa?

Okrah Magic nae hajacheza ata game 1 karudi home kudinya zoo nguvu viongozi mnazitoa wapi kumruhusu?

Mdaka mishale ya kashaaga kule AFCON au bado nae kabakia kuwasapoti Cote D'ivoire (Ivory Coast)

Nakumbuka hata last season predator Kalala Fiston Mayele alipewa likizo ya hovyo kisa anaongoza kwa mabao lakini Said Kipara akam surprise kwa idadi kubwa ya mabao. Viongozi wa mpira hawako hivyo buana acheni umangungu.

Toeni likizo muda huo tushatawazwa kua machampion wa ligi hii otherwise hii dharau itatucost na kuanza kumtafuta sijui nani mchawi.

Wachezaji nyota wa kikosi hawapo kambini halafu mnataka kutetea taji la ligi kuu kizembe hivyo!😥

Siko hapa kukosoa but nasema vile vitu macho ya kiroho yanaona.

Viva Yanga Daima Mbele
 
Kocha wa Yanga anaonekana kama hana sauti vile kwenye maamuzi. Yaani mchezaji anafunga ndoa wakati ligi inaendelea! Badala ya mwishoni mwa msimu!!

Wakati ligi iliposimama, baadhi ya mastaa walipewa mapumziko yasiyo na sababu za msingi. Na matokeo yake ndiyo haya sasa. Timu inapata matokeo kwa shida ukilinganisha na wapinzani wetu simba ambao hawakufanya ujinga kama huo kwa wachezaji wao.
 
Likizo walizopewa wachezaji wa Yanga zitaigharimu sana timu, unaona kabisa timu imerudi nyuma hatua zaidi ya 10 yaani wachezaji wamekuwa wazito, mbele maelewano hakuna ni vulu vulu. Wachezaji fitness hawana, angalau mechi ya Dodoma jiji nimeanza kuona baadhi ya wachezaji wameanza kurejea katika utimamu wa mwili na akili mfano Aucho japo ajawa bado katika asilimia zake za utimamu. Wachezaji wa Yanga wamekula bata haswa hawa dah tuombe tu tupatage point tatu hata kwa kwa jasho la goli moja. Laah sivyo ligi itakuwa ngumu kwa Yanga.
 
Kocha wa Yanga anaonekana kama hana sauti vile kwenye maamuzi. Yaani mchezaji anafunga ndoa wakati ligi inaendelea! Badala ya mwishoni mwa msimu!!

Wakati ligi iliposimama, baadhi ya mastaa walipewa mapumziko yasiyo na sababu za msingi. Na matokeo yake ndiyo haya sasa. Timu inapata matokeo kwa shida ukilinganisha na wapinzani wetu simba ambao hawakufanya ujinga kama huo kwa wachezaji wao.
Suala la kufunga ndoa nakupinga ndugu yangu, kuna ubaya gani mchezaji kufunga ndoa ili aishi kihalali na mpenz wake kama mke na mume na sioni ulazima wakusubiri mpaka msimu uishe ndio ufunge ndoa kwa sasa Bacca anapaswa kupewa hata mwezi mmoja tu wa Honeymoon kisha atarejea kuungana na wenzake mapema mwezi wa 3 wala sioni ubaya wowote kwenye hilo
 
nawaahid ili tutalifanyia kazi haraka iwezekanavyo. asante
 
Kocha wa Yanga anaonekana kama hana sauti vile kwenye maamuzi. Yaani mchezaji anafunga ndoa wakati ligi inaendelea! Badala ya mwishoni mwa msimu!!

Wakati ligi iliposimama, baadhi ya mastaa walipewa mapumziko yasiyo na sababu za msingi. Na matokeo yake ndiyo haya sasa. Timu inapata matokeo kwa shida ukilinganisha na wapinzani wetu simba ambao hawakufanya ujinga kama huo kwa wachezaji wao.
Hizi ni zile ndoa za Ramadhani kwa hiyo kocha ameona asiingilie imani ya mtu
 
Suala la kufunga ndoa nakupinga ndugu yangu, kuna ubaya gani mchezaji kufunga ndoa ili aishi kihalali na mpenz wake kama mke na mume na sioni ulazima wakusubiri mpaka msimu uishe ndio ufunge ndoa kwa sasa Bacca anapaswa kupewa hata mwezi mmoja tu wa Honeymoon kisha atarejea kuungana na wenzake mapema mwezi wa 3 wala sioni ubaya wowote kwenye hilo
Naheshimu maoni yako.
 
Kocha wa Yanga anaonekana kama hana sauti vile kwenye maamuzi. Yaani mchezaji anafunga ndoa wakati ligi inaendelea! Badala ya mwishoni mwa msimu!!

Wakati ligi iliposimama, baadhi ya mastaa walipewa mapumziko yasiyo na sababu za msingi. Na matokeo yake ndiyo haya sasa. Timu inapata matokeo kwa shida ukilinganisha na wapinzani wetu simba ambao hawakufanya ujinga kama huo kwa wachezaji wao.
Hahahaha nimecheka sanaaa sasa mnataka aoe lini jamani...unataka wampore mchumba ake? Kwa sasa ana kibunda cha Afcon wacha awowe...
 
Chakuzingatia ni maandalizi ya kimataifa kwa wachezaji wote ila kwa awa waliopo Bado wanauwezo wa kutwaa ubingwa wa NBC bila shida yoyote.
 
Watakuja kushtuka gap la points 5 wamezidiwa, kila game sasa imekuwa ngumu
 
Chakuzingatia ni maandalizi ya kimataifa kwa wachezaji wote ila kwa awa waliopo Bado wanauwezo wa kutwaa ubingwa wa NBC bila shida yoyote.
jihadharini pale mnapojiaminisha kuwa ubingwa wa ligi kuu msimu huu, alafu ikatokea tofauti.
utasononeka na moyo wako
 
Back
Top Bottom