Yanga tusitarajie makubwa toka kwa wachezaji wapya, huwezi kutenganisha mpira na ushirikina, wachezaji watapigana misumari

Mdukuzii

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
2,552
Reaction score
6,422
Hili ni angalizo.

Naona watu wameweka matumaini makubwa kwa wachezaji wanaosajiwa Yanga.

Niwaambie kitu Africa mpira na ndumba ni mapacha wawili.

Simba na yanga ni mara chache sana walisajili wachezaji wabovu,wengi walitoka huko wakiwa na kiwango cha juu leo wapo Kitayose,Ihefu sijui Namungo.

Fei toto hawezi kukubali apotee kisa Aziz ki wakati babu yake mzee Makame yupo hapo pemba,atapanda boti na sox ya Aziz ki,kifuatacho ni majeruhi yasiyokoma au kushuka kiwango.inside job.huo ni mfano tu japo unaweza kuwa kweli.

Adui wa viwango vya wachezaji huwa hawatoki mbali ni washkaji zao wa karibu.

Pale msimbazi kuna kakijana kanacheza beki ya pembeni na kuna mlevi kiungo ya chini 😳.

Mtamlaumu viongozi kuwa wameleta magarasa kumbe sababu ni za kiufundi zaidi.

Fuatilia profile ya Mavugo,Chikwende,Nyoni wa malawi, Sarpong ,Moringa na Chirwa huko walipotoka kabla ya kutua nchini walikuwa wanawindwa na PSG.leo wako wapi.

Msimu uliopita Yanga tulikuwa na hamu ya makombe wachezaji tukaweka ubinafsi pembeni.tukaipigania timu

Msimu huu Mayele akifikisha goli 12 mniite mbwa.

Aziz Ki akitoa asist kumi njooni mniue.
 
Kama uchawi una saidia, Simba wangekua Mabingwa wa Afrika. Wamepuliza madawa kwenye vyumba vya kuvalia nguo, wamefukia wanyama hai uwanjani, wamebeba mapaka uwanjani, wame washa moto uwanjani Tena ugenini lakini sikuzote wame angukia pua.
Kikubwa ni kujituma na mazoezi ya kutosha wachezaji watafanikiwa.
 
Umeongea ukweli japo hata hao wachezaji wapya nao ni wachawi wazuri
 
Kama uchawi una saidia, Simba wangekua Mabingwa wa Afrika. Wamepuliza madawa kwenye vyumba vya kuvalia nguo, wamefukia wanyama hai uwanjani, wamebeba mapaka uwanjani, wame washa moto uwanjani Tena ugenini lakini sikuzote wame angukia pua.
Kikubwa ni kujituma na mazoezi ya kutosha wachezaji watafanikiwa.
Uchawi kwenye soka hapa afrika upo ndugu yangu .ile yanga ya Zahera tulikuwa tunafunga magoli ya ajabu ajabu huku tumeshindia uji kambini,kimataifa tunakutana na wachawi wa kimataifa ,uchawi unazidiana nguvu
 
Kama uchawi una saidia, Simba wangekua Mabingwa wa Afrika. Wamepuliza madawa kwenye vyumba vya kuvalia nguo, wamefukia wanyama hai uwanjani, wamebeba mapaka uwanjani, wame washa moto uwanjani Tena ugenini lakini sikuzote wame angukia pua.
Kikubwa ni kujituma na mazoezi ya kutosha wachezaji watafanikiwa.
Kwa taarifa yako tuu uchawi unasaidia sana hapa Afrika na dozi ya uchawi wa simba nindogo inaishia robo fainali tuu. Labda wapate ucahwi wa kiarabu watavuka nusu ambao ni gharama sana kuupata
 
Hajacheza mpira huyu dogo hawezi kuelewa
 
Kwa taarifa yako tuu uchawi unasaidia sana hapa Afrika na dozi ya uchawi wa simba nindogo inaishia robo fainali tuu. Labda wapate ucahwi wa kiarabu watavuka nusu ambao ni gharama sana kuupata
Yaani Al Ahl asajiri mchezaji mmoja kwa 1B ana coach wa viwango training facilities za kisasa wachezaji wanalipwa mshahara mkubwa bado aende kwa mganga?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kama uchawi ungekuwa unafanya kazi, basi msimu huu simba ingefuzu hatua ya nusu fainali kule Afrika ya Kusini.
Ila kwa bahati mbaya ndiyo hivyo tena. Hayo ni mambo tu ya kufikirika.
 
Back
Top Bottom