Yanga tutaishije bila GSM? Ufadhili una kikomo

Yanga tutaishije bila GSM? Ufadhili una kikomo

Mimi kama mwanachama wa Yanga nampongeza mfadhili wetu GSM Kwa mazuri anayoifanyia timu yetu

Lakini tukumbuke GSM ni binadamu anaweza siku akaamka hana furaha, akasitisha ufadhili wake, Kuna kufirisika, kifo n.k

Viongozi watueleze, je bila GSM sisi wanayanga tutakuwa vipi imara

Sifurahii kuishi Kwa pesa za mfadhili

Sifurahii GSM kuitwa mfadhili Bali aitww mdhamini, yaani ananufaika na Yanga ina nufaika sio kusema anatufadhili kama Yatima, hiyo ni kauli mbaya kwetu Yanga kuishi Kwa kufadhiliwa tunataka udhamini sio kufadhili

Tuliwahi kuwa timu Bora kipindi tuna Yusuph Manji, Gulmali, Mengi, Tarimba lakini walitoka timu yote ilipitia magumu sana

Eng Hersi nakuheshimu ila njoo na mikakati mizuri Yanga utoke kwenye wafadhili ije kwenye wadhamini

GSM aje na mahesabu atwambie anawekeza sh ngapi na ananufaika vip kutumia Logo ya Young Africans sio sisi mashabiki tuwe tunamwimba tu

GSM aweke pesa kulingana na mikataba, na vyanzo vya mapato ya club yawe wazi,

Binafsi naamini Kwa taasisi kama Yanga tunaweza kutumia brand yetu kujiendesha na kuingiza pesa ndefu bila kuwa na wafadhili

Tunahitaji uwanja wa timu
Viongozi achaneni na hapo jangwani kwenye Mafuriko, Tanzania ni kubwa ardhi ipo, tafuta sehemu Jenga uwanja sio mpaka kulilia vibali na ku risk ili uwanja ujengwe sehemu isiyo salama

GSM anafanya kazi nzuri ila tusifurahie maisha ya kufadhiliwa kama Yatima au wajinga
Unayo mawazo mazuri but sidhani kama unafatilia kwa Umakini kinachoendelea pale yanga,,usiingie kwenye propaganda ambazo hazina kichwa Wala miguu,,Yanga ndio klabu pekee ambacho kipo kwenye mchakato chanya wa mabadiliko ya kiuendeshaji hapa nchini,,na yanga hatua waliyofikia kwenye mabadiliko ayo ni hatua za mwisho mwisho kutangaza tenda kwa wawekezaji kwakuwa tiyali kampuni iliyopewa tenda ya kujua klabu Ina thamani Gani kiujumla imeshakamilisha kazi yake,
Baada ya hapo kinachofata ni kutangaza tenda kwa wawekezaji watakaowekeza kwenye klabu ambao wanatakiwa kuanzia wawili na wasizidi wanne ambao watagawana hisa 49% kulingana na dau la Kila mwekezaji na 51% zinabaki mikononi mwa wanachama!
Kwa maana iyo habari za sijui wafadhili sijui wadhamini vitabaki kama mengineyo unajua yanga aiendeshwi kwa mihemko ya watu wanafanya kazi yao kwa Umakini na kwa kuzingatia Sheria za nchi!
Nakupa mfano Mmoja tu juu ya suala la ujenzi wa uwanja mashabiki wengi wanaona limekwama lakini awajui ni kitu Gani kilichelewesha,,ni kwamba yanga waliambiwa na wizara wasubili wafanye tathmini yao juu ya upanuzi wa mto msimbazi kupitia wataalam wao ili mradi ukianza uendane na uwekezaji watakaofanya yanga hivyo Iliwabidi yanga wasubili kwakuwa waliomba pia kuongezewa eneo kwa maana iyo uvumilivu unahitajika kwa mipango endelevu na tujue klabu inafanya nini na kwa wakati Gani!
 
Acha propaganda na mazingaombwe ya jana, timu za simba na yanga zitaishi kwa ufadhiri mpaka mwisho.
Sheria ya nchi hii hairuhusiwi hizo timu kuwa na uwanja wala uwekezaji. Hizo unazoziona huko simba ni propaganda na siasa za kitoto
Kuwa shabiki wa Utopolo Ndio kipimo tosha kuonyesha ww hauna Akili yaani ni Zezeta.
Onyesha Hiyo Sheria!
Simba inaenda kujenga Uwanja
 
Gsm hatoi masada wala haisaidi yanga, Gsm anafanya biashara na yanga!!, Hivyo aondoke hata leo.
 
Back
Top Bottom