Yanga Vs Simba: Kadi nyekundu ya Jonas Mkude yafutwa, Simba yalimwa milioni 5

Yanga Vs Simba: Kadi nyekundu ya Jonas Mkude yafutwa, Simba yalimwa milioni 5

Kwahiyo ndio mnafunga kwa mikono kwa sababu halifutwi!
Ngoja nikupe somo kidogo!

Mabao ya aina hii yamebatizwa jina "Hand 0f GOD".

Hilo jina limetokana na ustadi, Ujuzi, Umakini na Utaalamu wa kiwango cha juu sana ulio tumika na mchezaji husika kufunga bao bila mwamuzi kutambua chochote.

Mara nyingi mabao ya aina hii si rahisi waamuzi wa pembeni na yule wa katikati kuweza kugundua....

"HII NINKUTOKANA NA KUWA MAGOLI YA AINA HII HUFUNGWA NA MCHEZAJI 'UNCONSCIOUSLY' YAANI BILA SHURUTI YAKE"

Mabao ya aina hii hufungwa mara nadra sana Ulimwenguni.

Unaweza kupewa nafasi kama 20 ya kufunga mabao ya mkono lakini mwamuzi akaweza kuona kwa kuwa umefanya "KUSUDIO".

Mara zote pongezi humuendea mchezaji, na lawama kwa mwamuzi....


Hauhitaji Hasira Sana kuhamisha lawama za Mwamuzi kupeleka kwa Mchezaji. Hizo hasira za kung'oa viti ni bora uzipeleke Shambani huenda ikasaidia.
 
hivi hiyo hali ya kufuta kadi hata kwa wenzetu ipo au si tunaiga wapi maana sielewi naona mauzauza tu
Nasikia wamekaa na kuangalia mkanda wa video ya marudio ya mechi ndipo wakaamua wafute kadi nyekundu.

Sasa sijui mechi za mikoani zisizo onyeshwa Luningani itakuwaje!
 
Unafuta adhabu ya muamuzi kwamba ilitolewa kimakosa halafu muamuzi na linesmen unawaacha eti kiporo.

Hivi hawaoni impact iliyojitokeza kwa Simba kucheza pungufu kwa karibia 2/3 ya dakika tisini.

Referee ndiye alipaswa aadhibiwe kwanza sababu ndiye chanzo cha vurugu zote uwanjani.
 
Ni kawaida kamati za mashindano ya vyama vya Mipira vya nchi husika kupitia mchezo husika na kuona kama hizo matches zilichezeshwa kwa halali au la. Makosa Kama ya kutoa kadi kimakosa hasa nyekundu hufutwa.
Hata hivyo hatua hizo hazihusu matokeo ya uwanjani kama goli lililofungwa au kukataliwa. Hivyo matokeo ya October mosi hayatabadilika kwa vyovyote vile. Pia mwamuzi kama ataadhibiwa ni lazima Kamati husika ijiridhishe kwamba kwa nafasi aliyokuwepo angeweza kuona hilo kosa. Kimsingi mapungufu mengi yanayojitokeza wakati wa mchezo ndiyo ladha yenyewe.
 
Naona TFF nao wapigwe faini na FIFA kwa kupanga mwamuzi ambaye si mara ya kwanza kuharibu mchezo.Sanya aliwahi kupigwa ngumi jicho likavimba.Aliharibu mechi ya coastal kwa kuibeba vyura Fc.Walitumia kigezo gani kupanga mtu kama huyu.Simba nasisi tujifunze kudai haki kwa nidhamu. Sanya apiwe faini kwa kutuchezesha pungufu 65min.
 
angalia jumla ya idadi za mechi. Nani ameshinda mechi nyingi! Nani amemfunga mwenzake mabao mengi! N.K
Malizia... Nani amepokea vipigo vikubwa vikubwa vingi!
6-0 awamu ya Nyerere
4-1 awamu ya Mwinyi
4-1 awamu ya Mkapa
5-0 awamu ya Kikwete

Juzi hii kwenye awamu ya Magufuli ilikuwa iwe 7-0, ila imeahirishwa tu. Kila awamu lazima ipate heshima yake!
 
mbona hawamzungumzii refa, na goli la yanga wangelikataa tu
 
Hawa tff nao, yani mchezaji amtukane refa af red card ifutwe!
Na katika hali ya kawaida , alipokuwa refa, si rahisi kuona lile tukio la kusogeza mpira kwa mkono, goli lilifungwa kwa mguu baada ya Tambwe kujitengenezea pasi kwa kutumia kifua na mkono!
 
Na la Kosceiline wa Arsenal ni la mguu kama la Tambwe ni la mkono?
 
Back
Top Bottom