Yanga vs Singida ni FIXED MATCH

Sasa mbona hata timu yako ya simba nayo inapocheza na Yanga huwa inafungwa! Na ikijitahidi sana basi huambulia sare! Unataka kusema na yenyewe pia huwa inakosa hiyo fighting spirit?
Yaani wao wanataka wawe mabingwa kwa kupambaniwa na team zingine wangekua wanashinda mechi zao haya yote yasingekuepo
 
Huu upembuzi yakinifu ungeufanya wakati Simba anatoka droo na Singida, au wakati Simba anafungwa na Azam
 
Shida sio kufungwa shida ni ile fighting spririt team zikicheza na simba na zinapocheza na yanga zinakuwa tofauti ile mechi ya mtibwa na yanga ilikuwa fixed na ile ya jana wachezaji wa team pinzani walikuwa hawajitumi kabisa.
Niambie hiyo FIGHTING SPIRIT inakuwaga wapi wakati Simba anacheza na Yanga? Huwa inakuwaje mnafungwa? AU NA NYIE MNAPEWA BAHASHA NA YANGA??
 
Unateseka ukiwa wapi? Tupe location
 
Mleta mada inaonekana hujui mpira au unafanya kusudi. Kwa mpira wanaocheza SBS wanaojua mpira hawashangai timu hiyo kufungwa na Yanga. Binafsi hata sare na Simba nilishangaa maana nilijua watafungwa kutokana na aina ya mpira wanaosheza. Haiwezekani wapishane vile uwanjani na Yanga huku wakiwa na akina Kaseke na Ndemla katikati halafu watoke salama.
 
Wewe siyo wa kiwango hiki Mkuu. Umeshavuka level, jitofautishe na Wahuni.
 
Hawa ndio walimwiza Banda makusudi Jana kaseke anapoteza pasi ila kabakizwa hadi mwisho
 
Hata hii mechi ilikua fixed maana inonga aliinua mguu makusudi Ili mayele apitishe mpira.
Kama vile diarra alivyomuachia lidobo okra majic apige goli bora la msimu
 
Kwani mwenye namungo ni mshabiki lialia wa Simba kama mwiguru Alie msajiri mpaka Feisal
 
Hakuna haja ya kuumiza vichwa hapa, hiyo mechi ilikua fixed OVER!!

1. Angalia goli la kwanza wakati krosi inapigwa beki hakujishughulisha hata kublock kasimama kama mti.

2. Goli la 3 alofunga kibwana kuna yule beki mkongo anakabia macho tu.

3. Goli la 4 Mayele anapiga beki yupo mbele yake hakuna blocking alofanya kasimama kama mti.

Watu wanasema mechi ya Simba na Mtibwa ilikua fixed, ni bora Mtibwa walipambana kuliko wale walima alizeti walikua wanafanya jogging uwanjani.
 
Alimuingiza Wawa kusaidia kupunguza idadi ya magoli. Mkuu wewe ukocha ulisoma ili ukusaidie kujua tactical substution zinavyokua au unajaribu ku guess tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtapata taabu Sana safari hii nakuambia.
 
Shida sio kufungwa shida ni ile fighting spririt team zikicheza na simba na zinapocheza na yanga zinakuwa tofauti ile mechi ya mtibwa na yanga ilikuwa fixed na ile ya jana wachezaji wa team pinzani walikuwa hawajitumi kabisa.
Shida mnachodhani kile mlichokutana nacho ndicho na sisi tunakutana nacho. Sababu ya kidwanzi sana kwa sababu tunatofautiana ubora yawezekana nyie ndio uwezo wenu uliishia pale na sisi tumefaidika na kwa wachezaji wao muhimu kutokuwepo na kubwa zaidi ni ubora wa Yanga kwa sasa. Hivi kwa ule mpira wa jana hasa kipindi cha kwanza kuna timu gani ingechomoka pale?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…