Yanga wachezaji wazawa wanatuangusha

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Hili ndio tatizo namba moja,

Wazawa wote wanaocheza nafasi za viungo na mbele akiwemo na Niyonzima wakubali tu kuwa viwango vipo chini waondoshwe. Kwa modern soccer kwa sasa mpira umebadilika mno hebu tuwaangalie kesho timu ya Mamelodi quality yao pale ndipo utakapoona kuwango anachostahili kuwa nacho Yanga.

Jingine ni umiliki wa mpira, tuna tatizo dogo la kupoteza mipira mingi pale tunapopenda sana kutumia mipira ya juu badala ya pasi za mtu kwa mtu pamoja na matumizi ya V pass hili limewashinda kabisa hasa wachezaji wazawa kama Nchimbi na wenzake.

Yanga ipo vizuri, mwalimu mzuri shida ipo hapo tu ambapo tunahitaji uwekezaji mkubwa tuongeze wachezaji ma-pro wazuri makombe tutayazoa mpaka tuseme basi.
 
Uto mkipata mtoto kama huyu ana miaka 27 tu lakini ametupa clean sheets 5 dhidi ya timu bora afrika yaani vita na mabingwa wa 3 wa dunia ahly bila kusahau miamba ya west africa plateau achilia mbali platinum
 
Hata wachezaji wa kigeni baadhi ni mizigo! Mcheki Fiston, Sarpong, HB wa kireno, hata Tuisila sio yule wa Vita! Mpaka nawakumbuka kina Molinga, Sibomana, Balinya hata Anko Mrisho! Tuzidi kuisapoti timu naamini mambo yatakuwa sawa na Inshaalah tutachukua ubingwa!
 
Umeikosoa yanga na ukasema Tena Haina tatizo!!

Nilidhani labda marefarii huwa wanayakataa magoli Yanga akifunga.

Kiukweli Yanga Haina wachezaji wenye ubora wa kudumu msimu mzima wakipata matokeo Bora.

Uwezo wao karibia wote Ni mdogo Sana!
 

Kweli tutachukua ubingwa baada ya kushinda ile kesi yetu fifa, unajua bana morrison ni mchezaji halali wa yanga kwahiyo mechi zote alizocheza morrison simba itapokonywa point 3 na Morri emecheza mechi kama 10 hivi mpaka sasa kwahiyo simba watapoteza point 30 hapo. Ubingwa ni wetu kudadadeki [emoji471][emoji471] na sisi tunapanda ndege mwaka huu [emoji928][emoji929]
 
Ubingwa sidhani msubili labda mwaka kesho
 
Ubingwa sidhani msubili labda mwaka kesho
Kuna mwaka Man U na Man city walikuwa wanafukuzia ubingwa wa England! Mpaka dakika ya 91 Man U walikuwa wana uhakika wa kubeba ndoo! Kilichotokea hawaamini hadi leo! Ndugu zangu mchezo wa soka hautabiliki, wekeni akiba ya maneno! Bado mechi ni nyingi sana!
 
unasema hawawezi kumiliki mpira, hawawezi pasi za MTU Kwa MTU,hawawezi V pass halafu bado unaita ni team nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…