Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla amethibitisha kuwa wameliingiza jina la kiungo mshambuliaji Bernard Morrison katika mfumo wa usajili wa wachezaji wa klabu hiyo (Transfer Matching system) na wamepeleka katika Shirikisho la soka la Barani Afrika na Shirikisho la soka la Dunia (FIFA).
Msolla amesema kuwa Kiungo huyo ni Mchezaji wao halali na hukumu iliyotolewa na Kamati ya (TFF) haina Uhalali wowote.
Msola amesema Jumatatu watatuma shauri la mchezaji huyo shirikisho la soka Duniani FIFA na ikiwa shirikisho hilo litamuidhinisha kuwa ni mchezaji wa Yanga, basi itawalazimu Simba waende mezani wakamalizane nao.
Orodha ya wachezaji wa Kigeni yaliyoingizwa katika mfumo wa TMS: Farouk Shikalo, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong, Tuisila Kisinda, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Yacouba Sogne, Carlinhos Carmo na Bernard Morrison.
HII TAARIFA MNAONAJE?