SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wakati Yanga wakiendelea kutafuta mchawi aliyesababisha wakapigwa na USMA wikendi iliyopita, baadhi ya mashabiki wao wameanza kuwashutumu baadhi ya watendaji wao kwa usaliti kisa kuvaa nguo zenye rangi nyekundu na nyeupe.
Katika jambo lililoshangaza wengi, siku ya mechi ya USMA kocha mkuu wa Yanga Nabi Nasrubrikegty alivaa jezi nyeupe.
Kama hiyo haitoshi, baada ya mechi hiyo mmoja wa watangazaji wa Yanga katika kitengo cha habari alionekana akiwahoji wachezaji wa Yanga huko kambini Kimbiji huku amevalia jezi nyekundu.
Mashabiki wa Simba walipotafutwa kutoa maoni yao kuhusu matukio haya wengi walijibu tu kwa kauli moja kuwa "sisi tuna watu".
Maoni yangu, Yanga jifunzeni mpira, kufungwa ni jambo la kawaida. Msije mkaaza kuvuana nguo kuchunguzana hadi rangi za vyupi.