Yanga wanachangisha pesa ya mganga kutoka visiwani

Yanga wanachangisha pesa ya mganga kutoka visiwani

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Aisee nilikuwa Yanga makao makuu pale ,huwa naenda kusikiliza stori za klabu yangu pendwa Yanga, pale nakutanaga na wazee kina mzee was Moro, mzee mpili, n.k

Sasa kuna daftari lipo pale UKIFIKA jioni linatembea la kuchangia pesa ya mganga kutoka VISIWANI Zanzibar, Lina karibu wiki 2, uchangiaji umeanza mapema kwa sababu ,HUYU mganga Awali alicheleweshewa pesa yake kwenye mechi ya nusu fainal ile ya Mwanza na akasema ilikuwa Yanga tushinde goli NYINGI.

Sasa Safari hii maandalizi yameanza hii itakuwa wiki ya tatu katika kuchangia ili Simba afe kwenye ngao ya jamii

Kilichonishangaza had Viongozi wakubwa wanachangia pesa ya mganga kutoka VISIWANI

Ila nasikia Simba walimtumia mganga wao akakuta tayari Yanga anaongoza goli 3, ikafanyika kazi zikapunguzwa ndipo likabaki goli 1

Ndio Maana wazee wa Simba waliongea mapema HII MECHI TUMEPIGWA .

Pita kuanzia saa 10 pale makao makuu utakuta daftari la mchango wa mganga

Kwa imani yangu mimi sikuweza kuchangia hata Mia japo nilipigwa elimu na wazee, binafsi naamini katika wachezaji wazuri na mbinu.
 
Aisee nilikuwa Yanga makao makuu pale ,huwa naenda kusikiliza stori za klabu yangu pendwa Yanga, pale nakutanaga na wazee kina mzee was Moro, mzee mpili...
Hivi kwenye mpira uchawi unasimama namba ngapi ya mchezaji?? Tz kuna mikoa inayosemekana kwa uchawi ipo vizuri sana ila hata timu ya ligi kuu kutoka hiyo mikoa hakuna. Huki zanzibar timu ya taifa na timu za vilabu huwa zinafika hatua gani kimataifa?? Kuamini uchawi kwa kizazi hiki ni ujinga
 
Mtaishia kuruka ukuta Kila siku Ili msifungwe na Simba.

Kila kukicha mechi na Simba utopolo mnaruka ukuta au mnapita kwenye Mlango wa waandishi wa Habari.

Piteni Mlango wa kawaida.

Acheni ushamba
 
Back
Top Bottom