Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Baada ya draw ya Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga kupangwa na Rivers United ya Nigeria, mashabiki wa Yanga wameonekana wenye matumaini makubwa ya kufuzu Nusu Fainali kwa kuona Rivers pengine ni timu ya kawaida na wanauwezo wa kuitoa.
Yanga ilivyopangwa na Rivers United, viongozi na baadhi ya mashabiki walishangilia lakini ukiangalia baadhi ya wachezaji waliokuwepo [Mudonda, Mzize na Mayele] pamoja na Kocha Msaidizi Cedric Kaze wote walikuwa ‘wamenyuti.’
Viongozi na wale wapambe inaonekana kama wanachukulia mambo kwa urahisi labda kwa sababu wao hawaingii kwenye pitch! Lakini kufanya vile si dhani kama wanajua athari yake.
Kwa dunia hii ya teknolojia ile video inaweza kuwafikia Rivers United wakaona namna Yanga wanavyosherekea kupangwa nao. Maaa yake wataweka extra care.
Kuna jambo unaweza kulifanya ukihisi linakupa faida kumbe inaweza kuwa tofauti. Sisi kwetu huku tunapenda maisha ya ‘kiki’ lakini kuna vitu vya kubaki navyo tu moyoni na sio kwenda kwenye jamii.
Kwa upande wanu sioni kama ni kitu kizuri kwa sababu, msimu uliopita walikutananao haohao wakapigwa nje ndani na kutupwa nje ya mashindano. Sasa anaepaswa kufurahi ni nani?
Inawezekana wamefurahi kwa sababu timu yao labda haijapangwa na timu kutoka mataifa ya kiarabu lakini kwa timu zote zilizofika hatua hiyo hakuna timu nyepesi.
Credit: Shaffih Dauda