Yanga wasema mchango wa Milioni 100 kwa CCM ulitolewa na GSM Foundation, Sio Fedha za Klabu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kutoa ufafanuzi kwa Umma, kuhusu mchango wa Shilingi milioni 100 uliotolewa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), siku ya tarehe 12/08/2025.

Mchango ule ulitolewa na Taasisi ya GSM Foundation iliyo chini ya mdhamini na Mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Said Mohammed na sio kupitia hela za Wanachama au kutoka kwenye mfuko wa Klabu, kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.

GSM Foundation imekuwa ikishirikiana na Klabu ya Yanga, kwa kipindi cha miaka mitatu kutoa fedha na misaada kwa jamii na makundi mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Soma Pia: Klabu ya Yanga imechagia milion 100 CCM gala dinner 2025

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuomba radhi kwa Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu wowote uliojitokeza kupitia sintofahamu hii.

IMG_5912.jpeg
 
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kutoa ufafanuzi kwa Umma, kuhusu mchango wa Shilingi milioni 100 uliotolewa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), siku ya tarehe 12/08/2025.

Mchango ule ulitolewa na Taasisi ya GSM Foundation iliyo chini ya mdhamini na Mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Said Mohammed na sio kupitia hela za Wanachama au kutoka kwenye mfuko wa Klabu, kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.

GSM Foundation imekuwa ikishirikiana na Klabu ya Yanga, kwa kipindi cha miaka mitatu kutoa fedha na misaada kwa jamii na makundi mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuomba radhi kwa Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu wowote uliojitokeza kupitia sintofahamu hii.
Si kweli. GSM foundation ndiyo waliotoa zile bilion 10. Sasa iweje tena wote milion 100 nyingine kwa mgongo wa Yanga?
 
Wameona imekuwa ajenda ya baadhi ya wapuuzi kufanya kichaka cha kujifichia na kujifariji wametoa ufafanuzi makini usiokuwa na maswali wala mbambamba👇
 
Attachments

  • FB_IMG_1755183895191.jpg
    FB_IMG_1755183895191.jpg
    100.9 KB · Views: 48
Hata kama ni yanga kamili kwa namna Watanzania walishambulia kwenye page zao lazima ubadili tu maelezo.

Na hawakuwa na njia nyingine zaidi ya kujitete ni kumsukumia GSM mzigo.

Yaani Mtu atoe 10B alafu aje atoe hela nyingine tofauti 100M na why itajwe Yanga?

Hapa viongezi wa Yanga hawakufikiria vema wakati wanajingiza kwenye hili.

Watanzania wanazipenda sana Simba ya Yanga ila zitakapojiingiza huko kwenye siasa aisee zitachukiwa balaaa... Haya ya Taifa star kukosa watazamani mi moja ya mipira kuwekwa siasa. Yanga jitizameni maana shida viongozi wazuri mnao ila wanafeli kwenye kuweka mahaba sana ya siasa pia
 
Yaani kwa ufafanuzi uo, Mbumbumbu wote Wana changanyikiwa.
Watu wanasahau kuanzia TAA mpaka TANU waanzilishi wa ivyo vyama ni Yanga zamani Young Boys/Wananchi kwakua Mwingereza hakutaka vyama vya siasa apa Tanganyika.
Yanga ndio baba wa ivyo vyama vya siasa kwakua wakati wa mkoloni siasa/ Mbinu za kumuondoa mkoloni zilifanyika kwenye klabu za Mpira

Young Boys/ Jangwani FC/ Yanga ilikuwepo tangu 1920 ikichagiza uhuru wa Nchi hii.
Fedha zilizo patikana katika mechi mbali mbali za Yanga zilitumika kuchangia TAA/ TANU kuji imarisha kisiasa.
 
Si kweli. GSM foundation ndiyo waliotoa zile bilion 10. Sasa iweje tena wote milion 100 nyingine kwa mgongo wa Yanga?
Usiwe kama rofa usichokijua uwe unauliza,,GSM foundation ni taasisi inayojitegemea ambayo Ina fungu lake kwa ajili ya misaada mbalimbali,
Kampuni ya GSM ndio iliyotoa bilioni 10 na sio GSM foundation usiwe unachanganya mambo soma taarifa kwa umakini usikurupuke!
 
Yaani kwa ufafanuzi uo, Mbumbumbu wote Wana changanyikiwa.
Watu wanasahau kuanzia TAA mpaka TANU waanzilishi wa ivyo vyama ni Yanga zamani Young Boys/Wananchi kwakua Mwingereza hakutaka vyama vya siasa apa Tanganyika.
Yanga ndio baba wa ivyo vyama vya siasa kwakua wakati wa mkoloni siasa/ Mbinu za kumuondoa mkoloni zilifanyika kwenye klabu za Mpira

Young Boys/ Jangwani FC/ Yanga ilikuwepo tangu 1920 ikichagiza uhuru wa Nchi hii.
Fedha zilizo patikana katika mechi mbali mbali za Yanga zilitumika kuchangia TAA/ TANU kuji imarisha kisiasa.
Acha mambo ya 1920's hayo ni mambo ya zamani sana hii ni Karne nyingine
 
Yaani kwa ufafanuzi uo, Mbumbumbu wote Wana changanyikiwa.
Watu wanasahau kuanzia TAA mpaka TANU waanzilishi wa ivyo vyama ni Yanga zamani Young Boys/Wananchi kwakua Mwingereza hakutaka vyama vya siasa apa Tanganyika.
Yanga ndio baba wa ivyo vyama vya siasa kwakua wakati wa mkoloni siasa/ Mbinu za kumuondoa mkoloni zilifanyika kwenye klabu za Mpira

Young Boys/ Jangwani FC/ Yanga ilikuwepo tangu 1920 ikichagiza uhuru wa Nchi hii.
Fedha zilizo patikana katika mechi mbali mbali za Yanga zilitumika kuchangia TAA/ TANU kuji imarisha kisiasa.
Mbumbumbu ni wewe unayejidhihirisha hapa.

Wenzako wameona hilo jambo halijakaa sawa hadi wameamua wafafanue, wewe unaleta umbumbumbu promax,🤣🤣🤣🤣🤣
 
Usiwe kama rofa usichokijua uwe unauliza,,GSM foundation ni taasisi inayojitegemea ambayo Ina fungu lake kwa ajili ya misaada mbalimbali,
Kampuni ya GSM ndio iliyotoa bilioni 10 na sio GSM foundation usiwe unachanganya mambo soma taarifa kwa umakini usikurupuke!
Kwahiyo GSM katoa bil 10 alafu GSM FOUNDATION kupitia yanga katoa m 100? Mtajua Hamjui Mnachanganya Siasa na Mpira
 
Pale utopoloni wenye akili wawili tu.
wakati mama Samia anatoa ndege muende kucheza fainali hamjahoji hela anatoa wapi?
wakati mama Samia anatoa hela Kwa Jina la "GOLI LA MAMA"Wala hamjauliza.
Leo imekula kwenu mnaanza kulia lia.nani amewaaambia Kuna pesa za Bure?
 
Yaani kwa ufafanuzi uo, Mbumbumbu wote Wana changanyikiwa.
Watu wanasahau kuanzia TAA mpaka TANU waanzilishi wa ivyo vyama ni Yanga zamani Young Boys/Wananchi kwakua Mwingereza hakutaka vyama vya siasa apa Tanganyika.
Yanga ndio baba wa ivyo vyama vya siasa kwakua wakati wa mkoloni siasa/ Mbinu za kumuondoa mkoloni zilifanyika kwenye klabu za Mpira

Young Boys/ Jangwani FC/ Yanga ilikuwepo tangu 1920 ikichagiza uhuru wa Nchi hii.
Fedha zilizo patikana katika mechi mbali mbali za Yanga zilitumika kuchangia TAA/ TANU kuji imarisha kisiasa.
Zamani ilikuwa ni chama kimoja, vipi sasa?!
Acha utetezi wa 'Kindezi'. Kama timu imeona ije na barua hiyo tafsiri wameona wapi walipojikwaa na sio kujitekenya kama ufanyavyo.
 
Back
Top Bottom