Yanga wasema mchango wa Milioni 100 kwa CCM ulitolewa na GSM Foundation, Sio Fedha za Klabu

Yanga wasema mchango wa Milioni 100 kwa CCM ulitolewa na GSM Foundation, Sio Fedha za Klabu

Usiwe kama rofa usichokijua uwe unauliza,,GSM foundation ni taasisi inayojitegemea ambayo Ina fungu lake kwa ajili ya misaada mbalimbali,
Kampuni ya GSM ndio iliyotoa bilioni 10 na sio GSM foundation usiwe unachanganya mambo soma taarifa kwa umakini usikurupuke!
Milioni 100 zimetolewa kwa jina la yanga sio GSM Foundation
 
1755199626590.jpg
 
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kutoa ufafanuzi kwa Umma, kuhusu mchango wa Shilingi milioni 100 uliotolewa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), siku ya tarehe 12/08/2025.

Mchango ule ulitolewa na Taasisi ya GSM Foundation iliyo chini ya mdhamini na Mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Said Mohammed na sio kupitia hela za Wanachama au kutoka kwenye mfuko wa Klabu, kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.

GSM Foundation imekuwa ikishirikiana na Klabu ya Yanga, kwa kipindi cha miaka mitatu kutoa fedha na misaada kwa jamii na makundi mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Soma Pia: Klabu ya Yanga imechagia milion 100 CCM gala dinner 2025

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuomba radhi kwa Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu wowote uliojitokeza kupitia sintofahamu hii.

View attachment 3441344
Kunawatu huwa hawaelewi hata kidogo
 
Back
Top Bottom