Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kutoa ufafanuzi kwa Umma, kuhusu mchango wa Shilingi milioni 100 uliotolewa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), siku ya tarehe 12/08/2025.
Mchango ule ulitolewa na Taasisi ya GSM Foundation iliyo chini ya mdhamini na Mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Said Mohammed na sio kupitia hela za Wanachama au kutoka kwenye mfuko wa Klabu, kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.
GSM Foundation imekuwa ikishirikiana na Klabu ya Yanga, kwa kipindi cha miaka mitatu kutoa fedha na misaada kwa jamii na makundi mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Soma Pia: Klabu ya Yanga imechagia milion 100 CCM gala dinner 2025
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuomba radhi kwa Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu wowote uliojitokeza kupitia sintofahamu hii.
View attachment 3441344