Yanga wazindua jezi yao nchini Malawi

Yanga wazindua jezi yao nchini Malawi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania wamezindua jezi mpya za Club ya Yanga usiku huu kwenye Ikulu ya Malawi ambako Yanga na Rais Samia walialikwa kusherehekea uhuru wa Nchi hiyo.

Kwenye video fupi ya tukio hilo Rais wa Club ya Yanga Engineer Hersi Saidi ameonekana akiwapatia Marais hawa jezi zao
 
Klabu ya Yanga imetambulisha jezi zao rasmi kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/2024.

Kupitia video fupi iliyopakiwa katika mitandao ya kijamii, Mchezaji Mayele pamoja na walimbwende kadhaa wameonekana wakicgeza kwa madoido na jezi hizo mpya za msimu unaotarajiwa kuanza Agosti 2023.
 
Hizi ni miongoni mwa jezi za hovyo nilizo zishuhudia
 
Baada ya purukushani nyingi kwenye mitandao ya kijamii hatimaye timu ya Yanga imefanikiwa kuzindua Jezi zake mpya za msimu wa 2023/2024
png_20230705_231117_0000.jpg
 
Walizopewa Rais Samia na mwenzake zina nembo ya Haier. Halafu tunaposema hii safari imetibua mipango ya klabu muwe mnaelewa, msikae tu kushangilia.
 
Ule si uzinduzi labda kama maana ya uzinduzi imepotea. Pale ni kuwa wamekabidhi jezi mpya ilabidi watoe tangazo lao la itel.
 
Back
Top Bottom