Yanga yaingia matatani na Jeshi la Tanzania, kauli zao kuwaponza

Yanga yaingia matatani na Jeshi la Tanzania, kauli zao kuwaponza

masau bwire kaongea ukweli ambao yanga hawataki kuusikia kwanza yanga watueleze kwanini mwaka jao washabiki wao walimpa hela yule beki kwa kumkaba tambwe na kumfanyia vurugu halafu leo kwa kitendo hicho hicho walalamike pia wanasahau yondani alipompiga kicha okwi kwenye mechi ya mtani jembe
 
Hivi FIFA si wanakataza mmiliki mmoja kuwa na timu zaidi ya moja kwenye ligi husika?

au sisi sio wanachama wa FIFA?

JKT Ruvu vs Ruvu shooting

Jamal Malinzi
 
Last edited by a moderator:
​hawa nao mishahara ya bure inawachanganya sana sasa ngoja vita ije watumikie mishahara yao
Hiyo mikwara ya kike Masau Bwire akawapigie kuruta wa JKT sio anatuletea na sisi,,
Nasubiri sana ili nione hao wanajeshi vitambi watafanya nini!!!
 
Hiyo mikwara ya kike Masau Bwire akawapigie kuruta wa JKT sio anatuletea na sisi,,
Nasubiri sana ili nione hao wanajeshi vitambi watafanya nini!!!
Ngoja waje wakubebe
 
Hawa wanajeshi hawana changamoto kama wenzao wa sudan, somalia nk. kwa hiyo wanataka kujaribisha mbinu zao za kijeshi uwanjani.. tafadhali MH. J.MALINZI futilia mbali hizi timu zitakuja kuua mtu uwanjani,
 
Huyo Bwire naye ni kilongalonga tu...

Mambo yanayotokea kwenye mpira wa miguu yanaamuliwa na taasisi husika...

Hii si nchi ya kijeshi kiasi kwamba wao kuitwa Boko Haram basi waoneshe ubavu na maamuzi ya kijeshi...

Kama hawawezi mambo ya michezo inayojumuisha raia basi waunde ligi yao...

Kama wana maamuzi ya kijeshi waende Ikwiriri wakawamate majambazi walioteka kituo na kuiba silaha. Unajeshi wao ndio unahitajika zaidi huko. Tunawajua kazi zao ni kuzushia watu kesi, kupokea rushwa vituoni. Mambo ya mpira yataamuliwa kimpira.

Kwanza imefika wakati kutimiza maagizo ya FIFA. Kila taasisi iwe na timu moja tu. Polisi, Magereza na JKT waunganishe timu zao tuondokane na upuuzi huu mpirani.
 
Hawa wanajeshi hawana changamoto kama wenzao wa sudan, somalia nk. kwa hiyo wanataka kujaribisha mbinu zao za kijeshi uwanjani.. tafadhali MH. J.MALINZI futilia mbali hizi timu zitakuja kuua mtu uwanjani,

SADC kuna ligi ya majeshi. Waende huko. Hatuwezi kuwa na utitiri wa timu za polisi, magereza na JKT!
 
Hata kama msimu ujao ikibaki timu moja ya jeshi, chondechonde Jeshi letu pendwa tubakishieni Ruvu Shooting, hasahasa "beki katili" George na msemaji abakie Komredi Masau Bwire.
 
Wanyama pori wanauwawa maelfu kwa maelfu huko mbugani, kwanini wasipelekwe hawa wakalinde huko kuliko kuleta kelele zisizo na maana hapa kwasababu za kipuuzi. Hawa wanakula mshahara wa bure tu, tena ni kodi za hao hao raia wanaowawekea mikwara kila siku. Kuna wanajeshi wengine utawakuta wanakunywa gongo hata jumatatu, hawa wapelekwe wakalinde tembo wetu, tusitaniane hapa.
 
Unawezaje kuiita taasisi ya jeshi ni Al shababu au boko haram? Kwa tendo lipi walilofanya linalofanana na matendo ya kigaidi
Mbona tayari kuna jibu kwenye post ambayo ume-quote? Jibu hili hapa... msisitizo kwenye RED!
Huyo Bwire naye ni kilongalonga tu...

Mambo yanayotokea kwenye mpira wa miguu yanaamuliwa na taasisi husika...

Hii si nchi ya kijeshi kiasi kwamba wao kuitwa Boko Haram basi waoneshe ubavu na maamuzi ya kijeshi...

Kama hawawezi mambo ya michezo inayojumuisha raia basi waunde ligi yao...
In short, ni sawa na unapotaka kuingia kwenye siasa, basi uwe tayari na makando kando yake!
 
Yanga ni zaidi Jeshi la Kujenga Taifa usishangae Mkuu wa JKT kuwa mwanachama wa Yanga.
 
Wanyama pori wanauwawa maelfu kwa maelfu huko mbugani, kwanini wasipelekwe hawa wakalinde huko kuliko kuleta kelele zisizo na maana hapa kwasababu za kipuuzi. Hawa wanakula mshahara wa bure tu, tena ni kodi za hao hao raia wanaowawekea mikwara kila siku. Kuna wanajeshi wengine utawakuta wanakunywa gongo hata jumatatu, hawa wapelekwe wakalinde tembo wetu, tusitaniane hapa.

Wakuu chondechonde, Masao Bwire si msemaji wa Jeshi letu, ni msemaji ovyo wa timu za Ruvu Shooting na JKT Ruvu. Tuepuke kulisakama Jeshi letu, tumsakame Bwire na timu zake. Sidhani kama Majenerali wanaweza kukaa mezani wakijadili kauli ya Yanga. Tatizo Bwire anachanganya michapo ya michezoni na mambo ya Jeshi.

Kwa hali hii MMJKT na MMJ wanatakiwa watafakari uhalali wa Bwire kuendelea kuwa msemaji wa hizi timu maana anaonekana hana weledi kabisa.

My take: Tusilisakame Jeshi kwa kauli iliyotolewa na "CHIZI' Bwire.
 
Hata kama msimu ujao ikibaki timu moja ya jeshi, chondechonde Jeshi letu pendwa tubakishieni Ruvu Shooting, hasahasa "beki katili" George na msemaji abakie Komredi Masau Bwire.

Na mimi naomba tu Kagera Sugar iendelee kuwepo na ka Toto Africans kapande daraja, shughuli ianze tena!
 
Mkuu ,sabato bado haijaanza?

Mpaka jua lizame.

Breaking News:

TFF imemfungia mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Ruvu Shooting kwa kufumbia macho vitendo alivyofanyiwa mchezaji Amisi Tambwe. Mwamuzi huyo hatapuliza kipienga tena hapa nchini na nje ya nchi hata nyakati 3 zitakapotimia.
 
Mpaka jua lizame.

Breaking News:

TFF imemfungia mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Ruvu Shooting kwa kufumbia macho vitendo alivyofanyiwa mchezaji Amisi Tambwe. Mwamuzi huyo hatapuliza kipienga tena hapa nchini na nje ya nchi hati nyakati 3 zitakapotimia.

Ahaaaaa.....mkuu hilo lilitazamiwa

TFF si wamejaa ma Yanga watupu

Saa TFF wamesha set precedence.....mtu akichezewa tu faulu mbaya ....

Baada ya mchezo aite vyombo vya habari

Then atafungiwa refa.
Jamal Malinzi at his best
 
Last edited by a moderator:
Mpaka jua lizame.

Breaking News:

TFF imemfungia mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Ruvu Shooting kwa kufumbia macho vitendo alivyofanyiwa mchezaji Amisi Tambwe. Mwamuzi huyo hatapuliza kipienga tena hapa nchini na nje ya nchi hata nyakati 3 zitakapotimia.

Kweli refa alionyesha kutokuumudu mpira.na si mara yake ya kwanza kumbuka msimu uliopita kati ya Simba na Coast Union. ila ndala mnalalamika sana
 
Hiyo mikwara ya kike Masau Bwire akawapigie kuruta wa JKT sio anatuletea na sisi,,
Nasubiri sana ili nione hao wanajeshi vitambi watafanya nini!!!

hujawah kula kichapo na jeshi. Wew sema hivyo halafu siku jichanganye ndo utajua ni vitambi au ni nn
 
Mpaka jua lizame.

Breaking News:

TFF imemfungia mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Ruvu Shooting kwa kufumbia macho vitendo alivyofanyiwa mchezaji Amisi Tambwe. Mwamuzi huyo hatapuliza kipienga tena hapa nchini na nje ya nchi hata nyakati 3 zitakapotimia.

Ni kulalama tu.
 
Back
Top Bottom