Kobello
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 8,967
- 8,547
Klabu kongwe ya Young Africans Sports Club leo inaingia mkataba na Azam Media utakaogharimu jumla ya shilingi Bilioni 34.8 (Bilioni 41 with VAT). Mkataba huu utadumu kwa miaka kumi(10) na utafanyiwa marudio/maboresho baada ya miaka mitano.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Kaimu Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Haji Mfikirwa alisema kuwa mkataba huu, utakua ni kichocheo kwa wadau wote wanaotaka kushirikiana na klabu hii ya Yanga. Kwa mfano, wawekezaji, makampuni ya matangazo n.k.
Kabla ya hapo, Katibu Mwenezi wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli alibainisha kuwa Yanga ndiyo klabu ambayo habari zake zinafuatiliwa sana hewani, magazetini (print) na kidijitali kwa ujumla. Akishukuru, CEO wa AZAM MEDIA ndugu Tido Mhando aliahidi kuboresha huduma ya matangazo inayotolewa na Azam Media. kalabu ya Yanga itakuwa inapokea jumla ya Shilingi 200 kwa mwezi, ambazo zitaongezeka kwa jumla ya milioni 20 kila mwaka hadi kufikia milioni 380 kwa mwezi.
Klabu ya Yanga itaweza kupokea hadi shilingi Bilioni 5.9 kwa mwaka kama Media rights ambapo kwa miaka kumi (10), watapokea kiasi cha Shilingi Bilioni 52.4 (jumlisha VAT).
Klabu nyingine pia zinakaribishwa kuingia mkataba na Azam Media.
My Take:
Simba (Vunjabei Sports Club) tunasubiri mkataba wenu.