Yanga yakubali kichapo cha kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara

Yaani hawa Yanga wanacheza Kama kikundi fulani hivi Cha wahuni uwanjani !!

Hebu badilikeni bana mnatutia aibu nyie timu kubwa acheni utopolo huo.

Huyu sarpong kazi ya kuanguka anguka tu muda wote daah hebu kazeni bana.
Mimi hilo nililiona mapema kabisa sema kwasababu sina jina wala sio public figure watu hawakunizingatia ila laiti kama maneno yale yangesemwa na mtu maarufu kongole nyingi zengemuendea

Tangu juzi hapo walipocheza na ken gold na kushinda kwa penalt hapo ndio nikajua ubovu wa hii timu. Siku fichi asilimia almost 97 ya wachezaji wa ken gold ni masela wangu ambao walikua wanachezea timu ya shule kule chunya

Kikosi kile cha ken gold ndio kilichocheza umiseta shuleni, kiukweli siku inayocheza yanga na ken gold mi sikuwa na taarifa kabisa

Nilishangaa tu redio za mtaani zilivyokuwa zina tangaza mpira nikawa naskia mtangazaji kamtaja tuisila kisinda kapigwa chenga maridadi na mchezaji ambaye jina lake lilivyotajwa nikastuka nikabaki najiuliza "huyu si mchizi wangu ambae tulikuwa tunakaa naye chimbo kule mbeya"?

Baadaye nimeingia JF nakuta update ya hiyo mechi kuangalia heading ni yanga vs ken gold nikasema haiwezekani huwenda kuna international club ina jina kama hilo, kuangalia kikosi chote mpaka benchi wote nawajua wakati nimepigwa na butwaa na scrow down nikakutana na picha ya hao wachezaji ambao wote ni masela wangu tangu hapo nikajua kumbe kujiita wa KIMATAIFA hakufati itifaki
 
Kiukweli sisi mashabiki wa Yanga tunaishi kwa shida sanaaaa😁, mchawi n hela tu. Viongozi wawalipe wachezaji hela zao la sivyo tutashika hadi nafasi ya tatu🤔🤔
Yaani kwa yanga ile kama bado unaona tatizo lipo kwenye hela basi hilo ndio tatizo kubwa kuliko tatizo lenyewe
 
Ngoja tusubiri press conference ijayo tuone watatoa visingizio gani.
 
Kwani GSM hawawalipi wachezaji?
GSM inawalipa wachezaji kulingana na ubora wao

Timu ambayo inatafuta ushindi kwa tochi mpaka kwa tag ya penalty kwenye timu ya umiseta ken gold utegemee GSM awalipe shingapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…