Yanga yakubali kichapo cha kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara

Yanga yakubali kichapo cha kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara

Hawa Coastal Union Wangekuwa Wanakamia hivi kila mechi si wangekuwa mbali, af mechi ijayo utaskia kapigwa nne na KMC [emoji23][emoji23][emoji23]
Waliyecheza nae leo ndiyo kiwango chake
 
MVUA IMENYESHA SASA NI MUDA WA KUTAFUTA MATOBO YANAYOVUJA

Anaandika @exaud_msaka_hqbari

Kufungwa Yanga ilikuwa ni swala la kusubiri, yani ni kama kumuona Tembo juu ya mti ni kusubiri maana ataanguka tu

Ilikuwa inashangaza mpira wanaocheza Yanga kwa mechi za karibuni alafu unaambiwa hawajapoteza mchezo.

Mechi Tano za nyuma zilikuwa zinaonesha kabisa kuwa Yanga anafungwa Siku yoyote na wao walikuwa wanajua hilo

Yanga shukuruni Mungu mmefungwa sasa ili mjue shida iko wapi, maana ushindi na sare vilikuwa vinawafanya mdhani kikosi chenu hakina mapungufu

Yanga haina shida ya kocha ina shida ya wachezaji, wachezaji wao ndio wale ile ndio kiwango chao kabisa wala wasilaumiwe

Kama watamtimua Kaze watakuwa wanamuonea tu ila hana uwezo wa kubadilisha aina ile ya wachezaji, hana uwezo wa kumfanya Farid akapata goli kama lile alilokosa pale

Ubingwa wa Tanzania ni Mchakato sana na unahitaji kusubiri na kujipanga, sio kuamka na kuahidi tusipochukua mtuulize

Sasa Yanga wakae chini kistarabu waulizane tuna shida gani na tunaifanyaje, maana sasa Marefa na TFF hawahusiki
images.jpg
 
Mkuu ni ni ujinga mtupu hakuna timu humu kabisaa, yaani hapa naomba sana Mungu biashara na Azam wafanye vizuri ili washike nafasi ya pili na ya tatu au namungo Kama Mungu akiwajalia sababu bado wana match Kama Kama 7 hivi za vipo ili hawa utopolo wwsipate nafasi ya kuenda kimataifa meimu ujao sababu tayari tuna nafasi 4, wakienda hawa itakuwa ni aibu tu kwa kweli.

We haiwezekani kila msimu timu inatema wachezaji karibu wote na kusajili wapya halafu unategemea ushinde huu si ujinga huu.

Unamuacha molinga unasajili Sarpong, unamuacha Sibomana eti kisa una kaseke, unamuacha Beki Kama Yondani kisa una Makapu, unamuacha Juma Abdul unasajili Kibwana Shomari.

Na usishangae mwisho wa msimu watatema Tena kikosi kizima hawa.
Ni kweli, viongozi weupe pale.
 
Fiston kapiga mtu ngumi mbele ya refa, hata kadi ya njano haijatolewa

Huyu refa
Huyo sio mchezaji huyo ni boxer

Huoni jina lenyewe tu Fiston

Fuatulia movie zote zenye ngumi kali utagundua neno fist halikosekani...fist of legend, fist of fury, fist fighting, fist of the north of star, fist within four walls

Na ligi yetu ya bongo haijawa mbali imepata bahati ya kuwa na fist on
 
Huu ndo ubaya wa kuwa unbeaten, yani kila timu inasaka nafasi ya kubunja hiyo rekodi, ndiyo maana tunakutana na ugumu mwingi sanaaa, nadhani wachezaj hawajapewa hii elimu ya ugumu tunaoupata😆
Tatizo unbeaten yenu ni ya droo na penalty nyingi za kubustiwa

Unbeaten mpira unapigwa mwingi kila mechi inashinda na hata ikitoea sare ni ya 1-1 au 0-0 na zote mikoani. Unajiita unbeaten unatoa sare ya 3-3 kwa Mkapa halafu wewe ndio msawazishaji?
 
Refa anawabeba Sana utopolo
Refa alikuwa anaangalia hali ya usalama wake baada ya mechi

Kama wachezaji tu ndani ya mechi wanarusha ngumi vipi kuhusu mashabiki ambao walitoa vitisho kuwa watakuja kumnyonga refa siku moja?

Refa alifika angle ya mbali na hivi pamoja ya kuwapa promo lakini wamefungwa itabidi marefa wataochezesha mrchi ya yanga waingie na ma bodyguard uwanjani
 
Back
Top Bottom