Yanga yakubali kichapo cha kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara

Yanga yakubali kichapo cha kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara

mi nahisi yanga ndio haina hadhi ya kuwa na supoko

kwasababu ukianza kuangalia utaweza kujiuliza kipi kilichowafanya ken gold waombe mechi na yanga na sio simba?

ken gold waliona yanga ndio timu ambayo wana wiana uwezo na ni kweli na ndio maana hata gemu ken gold alicheza vizuri kumzidi yanga japo walibustiwa na kile ki penalty

Na ndio maana hata baada ya ushindi huo 99% mashabiki wa yanga hawakuufurahia huo ushindi
We mpumbavu ile mechi ilikuwa kombe la FA na mechi ilipangwa na TFF, nyau wewe
 
Jamani si tulikubaliana kwenye kikao kilichopita kuwa Yanga LAZIMA wapewe penati kwenye kila mchezo wao. Kwa nini refa hajawapa hiyo stahiki yao hadi leo wakafungwa?

Hivi mechi kamishina yuko wapi? Popote alipo mwambieni yeye na jopo lake waandike barua ya kujiuzulu haraka sana

By kilo 800...
 
Walikua wamepewaje??odds?
Achana na hii mambo, ila jamaa wamedhalauriwa sana. Yani yanga imapewa odd 150??
Screenshot_20210304-201939_WhatsApp.jpg
 
Baada ya mzunguko wa kwanza Yanga kuifunga Coastal union bao 3-0, leo Coastal Union wamesema wanachezea heshima kwa uwanja wake wa nyumbani na kocha Mgunda amejigamba atakuwa wa kwanza kuifunga Yanga msimu huu.

Yanga inahitaji matokeo kuendelea kujiweka vizuri kileleni lakini uwanja wa Mkwakwani umekuwa haumpi matokeo ya uhakika kwenye misimu ya karibuni.

Kuwa nami kukujuza yatakayojiri uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

=======

Mechi zilizochezwa mapema leo

FT' Polisi Tanzania 1-0 KMC | Sheikh Amri Abeid

FT' Mtibwa Sugar 0-0 Biashara UTD | Jamhuri

FT' Tanzania Prisons 1-1 Mbeya City FC

=======

00' Mwamuzi anapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa mcho na Coastal wanaanza kusukuma guzi

06' Yanga inapata penati baada ya Kipemba wa Coastal kumuweka chini mchezaji wa Yanga

08' Tuisila Kisinda anashindwa kufunga penati, mlinda mlango wa Coastal anasimama imara na kuidaka penalt.

10' Coastal wanaweka bao la kwanza baada ya Erick Msagati kupiga shuti mpira uliokuwa unaamba goli la Yanga ulioanzia mpira wa adhabu ndogo

19' Feisal Salum anajaribu shuti la kushtukiza lakini mlinda mlango wa Coastal alikuwa yuko makini na kuuondoa kwenye hatari

32' Yaqub anaingia kuchukua nafasi ya Sarpong kwa upande wa Yanga

37' Tuisila Kisinda anasawazisha, Coastal Union 1-1 Yanga

40' Farid Mussa anashindwa kuongeza bao la pili kwa Yanga baada ya kubaki na mlinda mlango

45' Mpira unaenda mapumziko

46' Mpira umesharejea kutoka mapumziko, Coastal 1-1 Yanga

53' Deus Kaseke anajaribu kupiga shuti lakini mpira unapaa juu ya lango la Coastal Union

64' Mfungaji wa Goli la Coastal, Erick Msagati anakwenda bench na nafasi yake kuchukuliwa na Issa Abusheikh

72' Omari Majimengi najaribu kuitanguliza Coastal kwa mkwaju mkali lakini mlinda mlango wa Yanga anasimama imara

83' Mudathir Abdallah anaweka goli la pili kwa shuti kali lililopita na wavu na kuipa uongozi Coastal Union

90' Dakika tano zinaongezwa kumaliza mtanange

90+5' Coastal Union inatamba uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Yanga magoli 2-1.

Yanga inashindwa kutamba uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal union kwa mwaka wa sita mfululizo na inapoteza mechi yake ya kwanza ligi kuu Bara, majaliwa ya Yanga kubaki kileleni ni kuchacha kwa viporo vya Simba
Yule aliyebebwa kwa machela kutoka airport hadi kidimbwini anaitwaje vile na ameshafunga goli ngapi
 
Back
Top Bottom