Yanga yamkataa mwamuzi Ahmed Arajiga kuchezesha fainali Kombe la Shirikisho Julai 25, 2021

Yanga yamkataa mwamuzi Ahmed Arajiga kuchezesha fainali Kombe la Shirikisho Julai 25, 2021

Ila wametoa hoja fikirishi sana. Tanzania ina wamuzi wangapi? Je ni kwanini huyu pekee ahusike kwenye mechi zote za Simba tena kwa hatua zinazofuatana ( robo, nusu na fainali) je ni huyu pekee ndio mtenda haki kwa Simba na wengine hawawezi? Au ni kipi hasa?

Upande wa uongozi wa Yanga nao wasingeishia hapo bali wangewinisha madhaifu ya huyo maamuzi ni yapi mpaka kufikia kutokuamini. Kama mechi zote alichezesha kwa kufuata sheria na kanuni za FIFA, sioni tatizo hata akipangwa tena kuchezesha na ngao ya hisani.
 
Yaani utopolo wapo kienyeji mnoo,yaani wanawapangia hadi tff refa wa kuchezesha mechi yao,kwa hiyo asipobadilishwa hawataingiza timu uwanjani?

Hii mijamaa inatia aibu kweli soka letu,yaani kika siku ni mijitu ya hila na malalamiko tu
 
Si shabiki wa mipira yenu ya kitanzania lakini kimantiki inatia shaka mwamuzi mmoja kuchezesha mechi 4 consecutively. Hata wewe liangalie hilo halafu njoo na uchambuzi usioegemea upande wowote tuone. Hata mahakamani hili haliwezi kutokea kesi NNE zinazomhusu mshtakiwa mmoja kupewa hakimu mmoja.
 
Yaani utopolo wapo kienyeji mnoo,yaani wanawapangia hadi tff refa wa kuchezesha mechi yao,kwa hiyo asipobadilishwa hawataingiza timu uwanjani?

Hii mijamaa inatia aibu kweli soka letu,yaani kika siku ni mijitu ya hila na malalamiko tu
Balimi zikiisha kichwani hebu kaa kwa kutulia halafu ujaribu kudiscuss hili la refa mmoja kuchezesha timu moja toka robo fainal hadi fainal,tumia akili za kawaida tu ulizoumbiwa nazo kama zipo lakini
 
Achana na masuala ya Yanga wakati wewe ni Simba na Chadema Damu. Hivi una habari kuwa Mbowe yupo lupango, muulize Erythrocyte maana yupo anapika kumpelekea uji. Ila mkumbuke mtu akihudhuria msiba wa aliyekufa kwa COVID-19 lazima aji lockdow. Je Mbowe wenu anaisambaza mwanza baada ya kuhudhuria maziko ya kaka yake aliyekufa kwa Corona kutokana na makijidai yake? Jibu analo brazaj
Ya Mbowe hapa yanahisu nn?

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Balimi zikiisha kichwani hebu kaa kwa kutulia halafu ujaribu kudiscuss hili la refa mmoja kuchezesha timu moja toka robo fainal hadi fainal,tumia akili za kawaida tu ulizoumbiwa nazo kama zipo lakini
Shida ni nini kwani kama yupo vizuri zaidi ya wengine?

Hoja yenu ni nn,hana uwezo au ana mapungufu gani?
 
Wampe Manara achezeshe mechi maana nasikia kibarua cha usemaji kimeanza kuota nyasi kwa kasi kubwa sana🤣
 
Mbona barua yenyewe wameandika kiuoga hivyo! Hawajamkataa, wametilia shaka tu.

Kisaikolojia kwa kumuogopa Refa tu ni wazi Yanga ishafungwa goli nje ya uwanja.
 
Back
Top Bottom