Yanga yamtaka Fei Toto arudi klabuni haraka na pia klabu ipo tayari kumuuza

Yanga yamtaka Fei Toto arudi klabuni haraka na pia klabu ipo tayari kumuuza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Klabu ya Yanga inapenda kuutaarifu umma kuwa imepokea maamuzi ya marejeo ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kuhusu suala la mchezaji wetu Feisal Salum Abdallah.

Baada ya kupokea maamuzi hayo, Klabu ya Yang imemwandikia barua Feisal Salum kumtaka aripoti kambini haraka iwezekanavvo na kuendelea kuutumikia mkataba wake kama mchezaii halali wa Yanga mpaka tarehe 30, Mei 2024, kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.

Aidha, Klabu ya Yanga iko tayari kumpokea Feisal Salum na kumjumuisha kwenye kikosi, na kwa kuzingatia sera na utaratibu wa Klabu ya Yanga katika kuwaongezea mikataba wachezai wake wanaofanya vizuri, Uongozi wa Yanga uko tayari kuendelea na mazungumzo na Feisal Salum Abdallah na wawakilishi wake juu ya kuboresha mkataba wake, kama wataridhia.

Mwisho, Klabu ya Yanga inapenda kuutaarifu umma kwamba iko tavari kumruhusu Feisal Salum Abdallah kuondoka klabuni kwa kuzingatia matakwa ya mkataba na utaratibu wa sheria za uhamisho wa wachezait zinazotambulika na TFF pamoja na FIFA. Ikiwa pia kuna klabu yoyote inahitaji huduma ya mchezaji huyu, klabu ya Yanga iko tayari kufanya mazungumzo wakati wowote.

IMG_20230306_190642_367.jpg
 
Wapo tayari kuboresha maslahi yake. Mpira umerudi kwa Fei, kama ishu ni maslahi anaboreshewa pamoja na yote yaliyotokea.

Fei anachotaka mpaka sasa ni mkataba uvunjike na hakuna timu iliyosema inamtaka.
 
Na kama alikua sawa mbona anaomba tena kuvunja mkataba kwanini asimame na aliloanza nalo mwanzo?
Alikuwa sawa lakini anachokifanya saizi kimeegemea kwenye maamuzi ya TFF kwenye review iliyofanyika last Friday

Kwa maana ya kwamba yeye yupo kwenye msimamo wake ule ule wa kwamba hataki kuichezea Yanga, ila TFF kwasababu imemtambua kuwa ni mchezaji halali wa Yanga

Basi ameona aifate hiyo hiyo TFF kuachana na Yanga
 
Back
Top Bottom