Yanga yapigwa faini na CAF

Yanga yapigwa faini na CAF

H

Hata 2016 walipigwa faini kwa Mambo yao ya kipuuzi lakini wao wamekaa kuizushia Simba Mambo ya uongo
Labda kumbukumbu zako haziko sawa, Simba ndio timu iliyokua ikiongoza kwa kupigwa faini na Tff kwa kufanya vitendo vya kishirikina mechi ya Simba na Yanga kule Kigoma ili leta taharuki kwenye mageti , mechi ya Simba na Dodoma jiji mtaalamu wa mitishamba wa Simba alichimba kwenye kibendera Cha uwanja mchana kweupe apo atujazungumzia Mapaka ya uwanjani uvunjajji wa nazi kuzunguka uwanja wa taifa n.k
 
umemsahau mganga wenu siku ya mechi ya ngao ya jamii
 
Simba ndio timu iliyo Lengwa kwenye tuhuma za kupulizia madawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Ila kwakua uko nyuma CAF walishapokea malalamiko kutoka katika vilabu mbalimmbali.

CAF walicho fanya ni kuionya TFF juu ya malalamiko ambayo wamekua wakipata kutoka katika vilabu mbalimmbali vinavyo kuja nchini dhidi ya timu zetu.
Mbona simba hawajapewa adhabu kama ni walengwa ? Na kwa nini utopolo wapewe iyo fain na Wakati sio walengwa ? Au unajarb kuelekeza kitu usicho kijua ?
 
Tukisema hii timu ni kihuni inaendeshwa kama timu za ndondo wanakuja juu na kulalamika wanaonewa.

======

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeipiga faini ya Sh11 milioni klabu ya Yanga baada ya kushindwa kujibu madai ya kuwafanyia fujo baadhi ya watu waliokuwa kwenye msafara wa Rivers United ya Nigeria.

Malalamiko hayo yametokana na mechi ya hatua ya awali iliyochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Septemba 12 na Yanga kupoteza kwa bao 1-0, ambapo kupitia mitandao ya kijamii ya timu hiyo walilalamika kupigwa kwa watu mbalimbali akiwemo Ofisa habari wa timu hiyo, Charles Mayuku. Rivers United walipeleka malalamiko hayo CAF na kupitia mtandao wao wamethibitisha kupokea malalamiko hayo.

Pia CAF wamesema mechi hiyo haikutakiwa kuwepo mashabiki ila walibaini baadhi ya mashabiki uwanjani.CAF ilituma malalamiko hayo kwa Yanga kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), na wamesema hakukuwa na mrejesho wowote kutoka kwenye Shirikisho hilo. Kutokana na hilo bodi ya nidhamu imeipiga faini Yanga kiasi cha 5,000 USD sawa na Sh11 milioni za kitanzania
Mwaka 2016 timu hiyo ilipigwa faini kwa makosa mengine.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),limeipiga faini ya dola 5,000 Klabu ya Young African kwa kosa la kuchelewesha mchezo baada ya wachezaji wake.

Kumzonga mwamuzi wakati mchezo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya GD SagradaEsperanca uliofanyika Angola Mei 18, 2016.
Uongo uongo fc
 
Wanapitaje najua, wanashindaje najua, na nitatumia kujua kwangu kuwaonesha kwamba na mimi najua

Kabla ya mechi ya riverside tulipata kuona short clip ikionesha benchi la ufundi la yanga likika chini na manara kuzungumza namna ya kushinda mechi wanayo i-face kwakua manara alidai kujua mbinu zote walizokua wakitumiwa club bingwa kushinda mechi

Clip ilikua fupi hatukuelewa kilicho jadiliwa na kilikubalika vipi, na mbinu ipi ya manara aliyo propose, ila baada ya mechi tuliwaona wachezaji wa rivers wakiwa na majeraha ya kichwa ambayo yalikuwa mabichi kabisa

Unaweza ukaona ni mbinu gani ambayo ofsa manara aliwapa benchi la ufundi, na hii ndo outcome yake sasa
Kwa hiyo kwa makusudi mazima Haji Manara aliwaingiza Utopolo chaka ili waadhibiwe. Hata kwenye mchezo wa marudiano kule Port Harcourt Haji alishauri Utopolo wasiingize timu uwanjani akiwa na lengo la kuwakaanga Utopolo. Huu msukule utawagharimu sana Utopolo.
 
Mbona hata Azam waligoma kupita geti la kawaida kwenye mechi yao na Coastal Union kule Tanga! Simba kwenye mechi na FC Platinum, shabiki wao aliingia na paka uwanjani!

Bado timu ya As Vita ililalamikia faulo mbalimbali walizo fanyiwa na simba! Una lipi la kusema?
Hizo record unazo wewe tu CAF hawana ndiyo maana Simba hawakuadhibiwa. Nyie endeleeni tu kumsikiliza Haji mnafungwa na kupigwa faini ndefu yeye mshahara wake anapata.
 
Tukisema hii timu ni kihuni inaendeshwa kama timu za ndondo wanakuja juu na kulalamika wanaonewa.

======

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeipiga faini ya Sh11 milioni klabu ya Yanga baada ya kushindwa kujibu madai ya kuwafanyia fujo baadhi ya watu waliokuwa kwenye msafara wa Rivers United ya Nigeria.

Malalamiko hayo yametokana na mechi ya hatua ya awali iliyochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Septemba 12 na Yanga kupoteza kwa bao 1-0, ambapo kupitia mitandao ya kijamii ya timu hiyo walilalamika kupigwa kwa watu mbalimbali akiwemo Ofisa habari wa timu hiyo, Charles Mayuku. Rivers United walipeleka malalamiko hayo CAF na kupitia mtandao wao wamethibitisha kupokea malalamiko hayo.

Pia CAF wamesema mechi hiyo haikutakiwa kuwepo mashabiki ila walibaini baadhi ya mashabiki uwanjani.CAF ilituma malalamiko hayo kwa Yanga kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), na wamesema hakukuwa na mrejesho wowote kutoka kwenye Shirikisho hilo. Kutokana na hilo bodi ya nidhamu imeipiga faini Yanga kiasi cha 5,000 USD sawa na Sh11 milioni za kitanzania
Mwaka 2016 timu hiyo ilipigwa faini kwa makosa mengine.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),limeipiga faini ya dola 5,000 Klabu ya Young African kwa kosa la kuchelewesha mchezo baada ya wachezaji wake.

Kumzonga mwamuzi wakati mchezo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya GD SagradaEsperanca uliofanyika Angola Mei 18, 2016.
Simba ndiyo wa kulaumiwa wasingewatupia mbeleko hawa Utopolo yasingewakuta haya,nyie Simba punguzeni kiherehere wenzenu Uto hawapendi mjue.
 
Inawezekana tff walijua hyo ishu.ila sababu ni wajeuri wakapiga kimyaa
 
Tatizo utopolo jeuri. Kuna siku mtangazaji wa startv alimuuliza bumbuli je, wao kama club watamuadhibu mchezaji wao aliyeonesha alama ya tusi kwa mashabiki?

Bumbuli akasema hatumuuadhibu na hatuna mpango wa kumuadhibu kwa sababu mchezaji wetu alikanyagwa kabla ya kuonesha hilo tusi, kwa hiyo alikuwa analipiza.
Nikajisemea kweli pale uto mwenye akili ni kikwete tu.
 
Simba ndio timu iliyo Lengwa kwenye tuhuma za kupulizia madawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Ila kwakua uko nyuma CAF walishapokea malalamiko kutoka katika vilabu mbalimmbali.

CAF walicho fanya ni kuionya TFF juu ya malalamiko ambayo wamekua wakipata kutoka katika vilabu mbalimmbali vinavyo kuja nchini dhidi ya timu zetu.

Yah! Simba ndiyo mlengwa lakini Faini kapigwa Yanga! Hii ina maana CAF wanaihujumu Yanga au CAF wamelikosea Jina la Simba kwa kuandika Yanga.
 
Hili liwazindue TFF kwani wao ndio wanalea hizi tabia mbovu mbovu kwenye mpira wa Tanzania. Kwenye ligi kila siku timu zinavunja sheria na hasa tabia ya kuruka ukuta badala ya kupitia mageti sahihi ya kuingilia lakini utasikia faini TZS 500,000. Laiti kama faini ingekuwa millioni 50 au kukatwa pointi naamini vilabu vyetu vingekuwa vinafuata sheria na hata hiyo adhabu ya CAF isingekuwepo kwa Yanga. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo TFF imezilea vibaya timu zetu hasa hizi kubwa sasa tunaanza kuvuna matunda yake na isipochukua hatua stahiki haraka basi tutegemee adhabu kubwa huko mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom