Yanga, yasema mchezo dhidi ya Simba upo palepale hakuna mabadiliko yoyote

Watacheza na "SIMBA WA BAHARI" ya Counsellor Salaah wa Silent Ocean inayoshiriki Ramadhan Cup!
 
CCM Ndio inapenda vijana Wa Tanganyika waweke nguvu zao huko kwenye simba Na YANGA".

Great Thinker
.

Leo Tutaona Nyuzi za Simba na Yanga zaidi ya elfu 60 humu jukwaani.

TUKIWAAMBIA KUSHABIKIA SIMBA NA YANGA NI UPUMBAVU HAMUELEWI
Na wewe umekuja ku comment humuhumu ku support upumbavu wao hivyo wewe ni .....
 
Wakisusa wao siye twala. Simba wanajua nini kitawapata, wameona bora nusu shari, kuliko shari kamili. Leteni timu, mmeshajua mtagongwa hakuna namna. Kufanya mazoezi ni meamua kuitumia tu. Sisi tutaenda Uwanjani.
Kwa nini mmezuia wasifanye mazoezi?
 
Yanga inatakiwa wasafishe hali ya hewa kwanza. Sababu ya kuwazuia Simba kufanya mazoezi ni ipi?
Kwani huo uwanja ni mali ya Yanga mpaka wazuie timu nyingine kufanya mazoezi? Na unaweza kumtaja kiongozi yeypte yule wa Yanga aliyewazuia hao simba kufanya mazoezi?
 
Kwani huo uwanja ni mali ya Yanga mpaka wazuie timu nyingine kufanya mazoezi? Na unaweza kumtaja kiongozi yeypte yule wa Yanga aliyewazuia hao simba kufanya mazoezi?
Tunapenda sana kujadili hisia.
 
Tunapenda sana kujadili hisia.
Binafsi natamani sana kujikita kwenye uhalisia. Na hakuna hisia yoopte ile. Je, sababu ya simba kususia mechi ina mashiko? Kwa kisingizio cha meneja wa uwanja kuwazuia kuingia kufanya mazoezi siku ya mwisho?

Ni kwa nini wasijikite kwenye kumshtaki huyo meneja kwa kwa wakubwa wake ili kuchukuliwa hatua kama itabainika ana makosa?
 
Uaneni 😁😁
 
Uongozi wa Klabu ya Yanga SC umesema kuwa mchezo wa Derby ya Kariakoo uliopangwa kucheza leo Machi 8, 2025 dhidi ya Simba saa moja na robo usiku uko pale pale na hakuna mabadiliko yoyote

“Yanga SC kama wenyeji wa mchezo, tunaamini taratibu zote za mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni za Ligi Kuu ya NBC, ziko sawa na maandalizi yote yako tayari,” imeeleza taarifa ya Klabu ya Yanga

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa “Uongozi wa Young Africans SC utapeleka timu uwanja wa Benjamin Mkapa kama inavyoelekezwa kwenye kanuni, na hatutakuwa tayari kucheza mchezo huu siku nyingine tofauti na leo.

Tunawaalika uwanjani wanachama, mashabiki, wapenzi wa klabu yetu na wadau wengine waliosafiri kutoka mikoani, nchi za jirani na sehemu mbalimbali duniani kote kuja kushuhudia mchezo huu mkubwa Barani Afrika.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…