Yanga, yasema mchezo dhidi ya Simba upo palepale hakuna mabadiliko yoyote

Yanga, yasema mchezo dhidi ya Simba upo palepale hakuna mabadiliko yoyote

Uongozi wa Klabu ya Yanga SC umesema kuwa mchezo wa Derby ya Kariakoo uliopangwa kucheza leo Machi 8, 2025 dhidi ya Simba saa moja na robo usiku uko pale pale na hakuna mabadiliko yoyote

“Yanga SC kama wenyeji wa mchezo, tunaamini taratibu zote za mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni za Ligi Kuu ya NBC, ziko sawa na maandalizi yote yako tayari,” imeeleza taarifa ya Klabu ya Yanga

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa “Uongozi wa Young Africans SC utapeleka timu uwanja wa Benjamin Mkapa kama inavyoelekezwa kwenye kanuni, na hatutakuwa tayari kucheza mchezo huu siku nyingine tofauti na leo.

Tunawaalika uwanjani wanachama, mashabiki, wapenzi wa klabu yetu na wadau wengine waliosafiri kutoka mikoani, nchi za jirani na sehemu mbalimbali duniani kote kuja kushuhudia mchezo huu mkubwa Barani Afrika.View attachment 3263599

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Hii ni nini?
 

Attachments

  • IMG-20250308-WA0026.jpg
    IMG-20250308-WA0026.jpg
    91.2 KB · Views: 1
Tukafanye kazi sasa tuache tupoteza muda kwa maigizo,Trump ameshakata misaada tujitegemee
 
Sasa hapa yanga wanaleta nongwa za kika siku.
Ingekuwa bodi ya ligi haijasitisha mchezo na simba asingepeleka timu, ilipaswa simba aadhibiwe kama haki ingesimamiwa vema.

Sasa mandhari bodi imeghairisha mchezo, kisha watataja siku nyingine ya game, wao hawapaswi kugomea mchezo.
 
Waache ujinga waturusishie FEDHA zetu tulizokata ticket. Sasa ma bausa wao wawatume kwenda kuzuia haki ya msingi ya timu kufanya mazoezi halafu waseme hawatakubali? Wasubiri rungu na baadaye tutawaburuza mahakamani kwa breach of contract. Tumelipa FEDHA tukaone mechi ila mmetuma wajinga wajinga kwenda kuwafanyia Fujo wapinzanj wenu na kusababisha mechi kuhairishwa?Ninyi ndio chanzo. "SINE QUO NON"
 
Yani siku tukicheza na makolo tupige goli 7 kama adhabu ya kutuchelewesha kuwapa kipigo.
Unamkimbia Yanga wewe nani?

Hizi drama zinatukata sana Wananchi, tulishajiandaa kuchinja leo.

Huu mchezo niliupania sana ila nafsi iligoma kabisa kukata tiketi, Mungu aliniongoza.
 
Yani siku tukicheza na makolo tupige goli 7 kama adhabu ya kutuchelewesha kuwapa kipigo.
Unamkimbia Yanga wewe nani?

Hizi drama zinatukata sana Wananchi, tulishajiandaa kuchinja leo.

Huu mchezo niliupania sana ila nafsi iligoma kabisa kukata tiketi, Mungu aliniongoza.
Hata ikiahirishwa miaka 5 ....Simba Haina uwezo wa kuifunga yanga

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Hapana mkuu....Yanga ndo giant wa TZ .. kwenye Kila sector....... financially.... influence & connecteness..japo wew ni mwanafunzi huwezi elewa

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Bila kusahau sector ya ujinga.

Hiyo ndio mnafanya vizuri.

Hapo kwenye hilo hata ukiniambia mna balón Dor siwezi kupinga.

Haya msemaji wenu anawaambia nendeni uwanjani.

Na saizi kule mageti yashaanza kufungwa. Najua hii haiwezi kuwa big issue kwasababu kama tu wachezaji wanaruka ukuta inashindikanaje kwa mashabiki.

Screenshot_20250308-142852.png
 
Wananchi twendeni uwanjani mechi yetu ipo, ile ya ndunduka na tff ndiyo imeahirishwa
 
Back
Top Bottom