Yanga yatoa msimamo mkali: Yadai pointi 3 kwa Simba, yakataa mechi ya marudio na kutaka Kamati ya Ligi Kuvunjwa!

Sababu ipo kwenye barua yao, hujaisoma? Hiyo hapo mwisho nimekuwekea.
View attachment 3265169

Sio hoja, huwezi kuitumia kupewa point tatu maana haikidhi tafsiri ya kususa.

Mkuu, mambo mepesi haya. Mambo ya Ubaya Ubwela.
Mambo mepesi unayaandika katika lugha husio ielewa hata wewe sasa mimi nitaelewa vipi? Nyie kususa mechi mmetumia kipengele gani au mliamua hukj mkitegemea hekima na busara.
 
Safi sana.
 
Nikuelewe vip wakati hata unacho kiandika ww mwenyewe hukielewi.Kwa hiyo TFF wamefuta mechi bila sababu ? Kwa hiyo kile mlicho fanya juzi cha kususa sio hoja kabisa? Sasa kama sio hoja ile barua mliiandika ya nini?
Hujanijibu umedakia kwa mtu mwimgine
 
Hujanijibu umedakia kwa mtu mwimgine
Kukujibu nini?Umekiri hujaa uwanjani sasa kama umesusa huoni tayari umekosea tena umesema huji na kanuni zipo wazi asiye kuja hastahili point tatu.

Halafu hiyo comment sijareply kwako kama vip msaidie kujibu?Huo nimeanza kumjibu mda mrefu au ulitaka ni mwache.....?
 
Mambo mepesi unayaandika katika lugha husio ielewa hata wewe sasa mimi nitaelewa vipi? Nyie kususa mechi mmetumia kipengele gani au mliamua hukj mkitegemea hekima na busara.
Hahahaha, we jamaa bana. Haya Twende taratibu.

Tafsiri ya kususa ni nini kikanuni? Ili useme, Timu A imesusa hivyo point zake watapewa timu B ambayo ni timu pinzani, ni mambo gani yanatakiwa yawe yametokea?

Tuanzie hapa kwanza.
 
Sasa mchezo utapangiwa tarehe nyingine ole wenu msipeleke timu uwanjani mtakatwa point 3 goli 3 pamoja na kushushwa daraja utopolo wakubwa nyie mmezoea kubembelezwa?
Simba wajanja sana! Uto mganga wao aliwaambia kuroga ni kipindi cha jua (mchana)na hakuna mtu kugusa pitch mpk siku ya mchezo (mechi). Uto wakajipanga kwa kulipia gharama kwa kuwazuia Simba wasiingie (kwakuwa watavunja masharti).Simba wakapenyezewa hii. Wakapiga simu tutachelewa kuja,wakijua sharti la mganga wa Uto.
NB:UTO WALIJICHANGANYA KUAMINI SIMBA WATAKUBALI KUTOFANYA MAZOEZI KWA KISA YA FUJO ZAO,NA WALIJIPNGA KULIPIA GHARAMA TFF. KUMBE SIMBA WALISHAELEWA MPANGO MZIMA. UTOPO HAWAAMINI KM WAMEZIDIWA MAARIFA ZAID YA KELELE ZA VYURA TU.
 
Yanga walileta team uwanjani?
 
Kwani mechi ilihairishwa kabla ya nyie kususa au baada ya nyie kuleta drama zenu za kususa?
Kaka unakichwa kigumu sana kuelewa, yaan ni hivi wenye mpira wao waliahirisha mechi baada ya timu ya Simba kulalamika kwao kuwa hawakupewa haki Yao ya kikanuni kafanya zoezi kwenye uwanja ambao mchezo utafanyika na muda ule ule wa mchezo wakalalamika kwa barua kwenda bodi ya ligi na kisha kwa press na wakatishia kutoshiriki mchezo huo namba 148
Bodi wakapitia malalamiko hayo wakaona Yana mashiko waka ahirisha mchezo, Sasa kama wangekuta hakuna mashiko wangewaambia Simba mechi iko pale pale na hapo ndio Simba wasingetokea basi point tatu zingeenda yanga...
Mchezo uliahirishwa ndio maana yanga hawakukuta waamuzi, match com etc etc

Usipoelewa na hapa basi tena
 
Hahahaha, we jamaa bana. Haya Twende taratibu.

Tafsiri ya kususa ni nini kikanuni? Ili useme, Timu A imesusa hivyo point zake watapewa timu B ambayo ni timu pinzani, ni mambo gani yanatakiwa yawe yametokea?

Tuanzie hapa kwanza.
Kwani source mpaka ya kufika hapa pameanzia wapi kama sio nyie kususa?au ndionkama ulivyosema kususa sio hoja, ila baadae mkaandika barua.

Sisi tumeenda uwanjani, hatupata taarifa OFFICIALLY? Tunahaki ya kudai points zetu tatu hata kama kamisaa hakuja, sasa hapo TFF watupe sababu ya kikanuni kwa nini mechi ilifutwa na kwa nini wao hawakuleta hao Makamisaa, sisi kwa upande wetu tumetimiza wajibu wetu,kama tunavyofanya kwenye mechi nyingine. Ndio maana kwenye hiyo barua tumetoa tunacho kitaka.
 
Walikuja Mzee, tena walikuwa peke Yao bado wakapitia mlango pori, na Leo wameenda bunju eti kucheza na Simba wanafikiri ligi kuu ni ndondo
 
Twende taratibu.

Anza na tafsiri ya kususa inayotajwa kwenye kanuni boss. Yaani unaposema, timu imesusia mechi, kikanuni maana yake hiyo timu imefanya vitendo gani?

Tukimaliza hapa tutakuja suala la nyinyi kwenda uwanjani.

Mdogo mdogo mpaka mwisho..
 
Kanuni gani kwenye inayosema ukizuiwa kufanya mazoezi susia mechi? Mbona simple.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…