the say
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,772
- 3,360
Mechi imeahirishwa unaletaje timu,, hivi mkinywaga Yale ma supu yenu huwa mnakosa akili eti..Sasa kama umekubali hujaleta timu huoni umejifunga wenyewe kwa kanuni mlizo refer wenyewe za TFF?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mechi imeahirishwa unaletaje timu,, hivi mkinywaga Yale ma supu yenu huwa mnakosa akili eti..Sasa kama umekubali hujaleta timu huoni umejifunga wenyewe kwa kanuni mlizo refer wenyewe za TFF?
Mambo mepesi unayaandika katika lugha husio ielewa hata wewe sasa mimi nitaelewa vipi? Nyie kususa mechi mmetumia kipengele gani au mliamua hukj mkitegemea hekima na busara.Sababu ipo kwenye barua yao, hujaisoma? Hiyo hapo mwisho nimekuwekea.
View attachment 3265169
Sio hoja, huwezi kuitumia kupewa point tatu maana haikidhi tafsiri ya kususa.
Mkuu, mambo mepesi haya. Mambo ya Ubaya Ubwela.
Kwani mechi ilihairishwa kabla ya nyie kususa au baada ya nyie kuleta drama zenu za kususa?Mechi imeahirishwa unaletaje timu,, hivi mkinywaga Yale ma supu yenu huwa mnakosa akili eti..
Safi sana.Kamati ya Utendaji ya Yanga, chini ya Rais Mhandisi Hersi Said, imefanya kikao cha dharura kujadili sintofahamu ya kuahirishwa kwa mechi yao dhidi ya Simba iliyopaswa kuchezwa tarehe 8 Machi 2025.
Katika taarifa yao, Yanga imetoa pole kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza kushuhudia mchezo huo na kueleza kuwa walifuata taratibu zote za maandalizi. Klabu hiyo imeeleza kuwa Simba ilishindwa kufuata utaratibu wa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa, jambo lililopelekea mgogoro uliosababisha wao kugomea mechi.
Kutokana na hali hiyo, Yanga imedai kupewa ushindi kwa mujibu wa kanuni, ikakataa kushiriki mechi hiyo kwa tarehe yoyote mpya itakayopangwa, na kutangaza kukosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu chini ya Steven Mnguto.
Klabu hiyo imeiomba TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wapya.
Soma: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
==
TAARIFA KWA UMMA
MACHI 09, 2025
Kamati ya Utendaji ya YANGA, chini ya Rais Mhandisi Hersi Said imefanya Kikao cha dharura leo tarehe 9 Machi 2025 kwa njia ya mtandao kujadiliana na kukubaliana mambo yafuatayo;
Kwanza, Uongozi wa YANGA unatoa pole kwa Wanachama, Mashabiki, Wapenzi na wadau wamchezo wa mpira wa miguu waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na kushindwa kushuhudia mechi yetu dhidi ya Klabu ya Simba iliyokuwa ifanyike jana tarehe 8 Machi 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Klabu ya YANGA ilifanya maandalizi yote ya mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni ikiwemo kushiriki kwenye kikao cha maandalizi ya mechi [MCM] kilichofanyika tarehe 7 Machi 2025, saa 8 mchana kwenye Hoteli ya Spice, Jijini Dar es Salaam.
Kwenye kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Klabu ya YANGA na Simba, wasimamizi wa mchezo ikiwemo Mratibu wa mchezo, Afisa Usalama wa mchezo, Mtathimini Waamuzi, Kamishna wa mchezo na watendaji wa Bodi ya Ligi, Klabu ya Simba haikutoa taarifa ya kutaka kuutumia uwanja wa Mkapa siku moja kabla ya mchezo husika kwa ajili ya kufanya mazoezi kama kanuni inavyoruhusu.
Katika hali ya kushangaza, Usiku wa tarehe 7 Machi, 2025, Klabu ya Simba iliwasili katika uwanja wa Mkapa ikiwa na magari kadhaa, kwa ajili ya kufanya mazoezi huku wakifahamu hawakuwa wamefuata taratibu za kupata haki yao ya kikanuni kama ilivyoainishwa kwenye taarifa ya Bodi ya Ligi, ikiwemo kuleta ombi hilo kwenye MCM, kuwasiliana na Msimamizi wa mchezo, Meneja wa Uwanja wala timu mwenyeji ambayo ni YANGA.
Mamlaka ya Uwanja ilikataa kuwaruhusu kuingia ndani ya Uwanja kwa sababu hakuku- wa na taarifa wala maandalizi yoyote yaliyofanywa kwa ajili yao, na baada ya kuwepo kwa sintofahamu hiyo, Klabu ya Simba iliamua kuondoka uwanjani hapo.
Usiku wa kuamkia siku ya mchezo, tarehe 8, Machi 2025, Klabu ya Simba ilitoa tamko rasmi la kugomea mchezo huo kwa kigezo cha kutopata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi, huku wakielewa dhahiri kwamba hawakuwa wamefata taratibu.
Huku kukiwa na taharuki kwa wapenzi wengi wa soka kuhusu uwepo wa mchezo huo baada ya tamko hilo la Klabu ya Simba, asubuhi ya tarehe 8 Machi 2025 Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Steven Mnguto alinukuliwa na vyombo vya habari akiwatoa wasiwasi na kuwahakikisha mashabiki waende uwanjani kwa sababu ratiba ya mchezo huu namba 184, iko palepale hakuna kilichobadilika.
Lakini licha ya tamko hilo la Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, mchana wa siku hiyo hiyo, tarehe 8 Machi 2025, Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu ambayo Mwenyekiti wake ni Steven Mnguto ilitoa taarifa ya kuahirisha mechi namba 184, kinyume na taratibu na Kanuni zinazoendesha Ligi Kuu.
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, ufuatao ndio msimamo wa Kamati ya Utendaji wa YANGA;
1: Klabu ya YANGA kupewa haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi.
2: Kamati ya Utendaji ya YANGA imekubaliana kutoshiriki mchezo namba 184 kwa tarehe yoyote itakayopangwa.
3. Kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, Klabu ya YANGA imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo, hivyo tunaliomba Shirikisho la Mpira wa miguu - TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wengine waadilifu na wenye nia njema kwa maslahi mapana ya mpira wetu.
Mwisho, lakini siyo kwa umuhimu, tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga kote duniani kuendelea kuwa watulivu wakati Uongozi ukiendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa sheria na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu, na harakati za kudai haki yetu zikiendelea.
Imetolewa na Kamati Ya Utendaji
Young Africans Sports Club
09.03.2025
Nimeshagundua shida ilipoNi kitu kile kile sema kimekuwe represented into variable kwa kutumia Algebra. Hamna sehemu nilipo changanya mafaili labda kama ulikimbia hesabu.
Hujanijibu umedakia kwa mtu mwimgineNikuelewe vip wakati hata unacho kiandika ww mwenyewe hukielewi.Kwa hiyo TFF wamefuta mechi bila sababu ? Kwa hiyo kile mlicho fanya juzi cha kususa sio hoja kabisa? Sasa kama sio hoja ile barua mliiandika ya nini?
Kukujibu nini?Umekiri hujaa uwanjani sasa kama umesusa huoni tayari umekosea tena umesema huji na kanuni zipo wazi asiye kuja hastahili point tatu.Hujanijibu umedakia kwa mtu mwimgine
Hahahaha, we jamaa bana. Haya Twende taratibu.Mambo mepesi unayaandika katika lugha husio ielewa hata wewe sasa mimi nitaelewa vipi? Nyie kususa mechi mmetumia kipengele gani au mliamua hukj mkitegemea hekima na busara.
Simba wajanja sana! Uto mganga wao aliwaambia kuroga ni kipindi cha jua (mchana)na hakuna mtu kugusa pitch mpk siku ya mchezo (mechi). Uto wakajipanga kwa kulipia gharama kwa kuwazuia Simba wasiingie (kwakuwa watavunja masharti).Simba wakapenyezewa hii. Wakapiga simu tutachelewa kuja,wakijua sharti la mganga wa Uto.Sasa mchezo utapangiwa tarehe nyingine ole wenu msipeleke timu uwanjani mtakatwa point 3 goli 3 pamoja na kushushwa daraja utopolo wakubwa nyie mmezoea kubembelezwa?
Yanga walileta team uwanjani?Kukujibu nini?Umekiri hujaa uwanjani sasa kama umesusa huoni tayari umekosea tena umesema huji na kanuni zipo wazi asiye kuja hastahili point tatu.
Halafu hiyo comment sijareply kwako kama vip msaidie kujibu?Huo nimeanza kumjibu mda mrefu au ulitaka ni mwache.....?
Timu isiyokuja uwanja inatakiwa ifanywe nini?Yanga walileta team uwanjani?
Timu isiyokuja uwanja inatakiwa ifanywe nini?
Kaka unakichwa kigumu sana kuelewa, yaan ni hivi wenye mpira wao waliahirisha mechi baada ya timu ya Simba kulalamika kwao kuwa hawakupewa haki Yao ya kikanuni kafanya zoezi kwenye uwanja ambao mchezo utafanyika na muda ule ule wa mchezo wakalalamika kwa barua kwenda bodi ya ligi na kisha kwa press na wakatishia kutoshiriki mchezo huo namba 148Kwani mechi ilihairishwa kabla ya nyie kususa au baada ya nyie kuleta drama zenu za kususa?
Kwani source mpaka ya kufika hapa pameanzia wapi kama sio nyie kususa?au ndionkama ulivyosema kususa sio hoja, ila baadae mkaandika barua.Hahahaha, we jamaa bana. Haya Twende taratibu.
Tafsiri ya kususa ni nini kikanuni? Ili useme, Timu A imesusa hivyo point zake watapewa timu B ambayo ni timu pinzani, ni mambo gani yanatakiwa yawe yametokea?
Tuanzie hapa kwanza.
Jibu hilo swali then nitakujibu na mimi? Au kuna ubaya wewe ukianza kujibu?Mimi nimekuuliza kwanza Nijibu Kisha nitakijibu swali lako,
Je Yanga walileta team uwanjani?
Haya uliza?Jibu hilo swali then nitakujibu na mimi? Au kuna ubaya wewe ukianza kujibu?
Twende taratibu.Kwani source mpaka ya kufika hapa pameanzia wapi kama sio nyie kususa?au ndionkama ulivyosema kususa sio hoja, ila baadae mkaandika barua.
Sisi tumeenda uwanjani, hatupata taarifa OFFICIALLY? Tunahaki ya kudai points zetu tatu hata kama kamisaa hakuja, sasa hapo TFF watupe sababu ya kikanuni kwa nini mechi ilifutwa na kwa nini wao hawakuleta hao Makamisaa, sisi kwa upande wetu tumetimiza wajibu wetu,kama tunavyofanya kwenye mechi nyingine. Ndio maana kwenye hiyo barua tumetoa tunacho kitaka.
Kanuni gani kwenye inayosema ukizuiwa kufanya mazoezi susia mechi? Mbona simple.Kaka unakichwa kigumu sana kuelewa, yaan ni hivi wenye mpira wao waliahirisha mechi baada ya timu ya Simba kulalamika kwao kuwa hawakupewa haki Yao ya kikanuni kafanya zoezi kwenye uwanja ambao mchezo utafanyika na muda ule ule wa mchezo wakalalamika kwa barua kwenda bodi ya ligi na kisha kwa press na wakatishia kutoshiriki mchezo huo namba 148
Bodi wakapitia malalamiko hayo wakaona Yana mashiko waka ahirisha mchezo, Sasa kama wangekuta hakuna mashiko wangewaambia Simba mechi iko pale pale na hapo ndio Simba wasingetokea basi point tatu zingeenda yanga...
Mchezo uliahirishwa ndio maana yanga hawakukuta waamuzi, match com etc etc
Usipoelewa na hapa basi tena
Sasa hapa ulikuwa unamuuliza nani akujibu kwanza? Unataka nirudie mara ya pili?Haya uliza?
Mimi nimekuuliza kwanza Nijibu Kisha nitakijibu swali lako,
Je Yanga walileta team uwanjani?