ndugu yangu kama hata mambo yaliyoanikwa wazi huoni? kweli wewe ubongo wako sijui toleo langapi?
mwenzako akitumbukia shimoni unajifunza na wewe unachukua tahadhari usije ukatumbukia shimoni!
lazima ujue shimo limetokana na nini na kwa nini hakuliona na wewe uangalie kwako kama kuna mashimo basi uyazibe na kama huwezi kuyaziba basi weka mabango kuwatahadharisha watumiaji wasije wakadumbukia.
tatizo la burundi linajumuisha mambo mengi ikiwemo jinsi gani katiba yao ilitengenezwa kwa kuweka checks and balansi katika mihimili.
yanayowakumba ndio kazi ya cheks and balansi kuvifanya vyombo vitumikie jamii na sio siku moja mtu mmoja au kikundi kinapora madaraka ya jamii kwa kutumia vyombo vya umma kwa maslahi binafsi.
kwetu sisi yawezekana hatujafika hatua ya mtu mmoja kutaka kubadili katiba ili aendelee kutawala au mambo mengine ambayo serikali inaweza kufanya kinyume na matakwa ya wananchi na wananchi kubaki hawana la kufanya zaidi ya kuingia kwenye vurugu au kufanywa wajinga na mtu mmoja au watu wachache.
je sisi tumehahakisha katika katiba yetu mashimo haya wanayotumbukia watu wa burundi tumeyaziba?
swala hili liko katika mihimili mitatu ya juu.
kwamba tumeunda mihimili hii kwa jinsi ambavyo mtu mmoja au kikundi cha watu kikitaka kufanya mabadiliko kama haya ya burundi kumuongezea mda raisi atakayekuwa madarakani wakati wowote au kufanya mabadiliko ya katiba kwa maslahi ya mtu au kikundi je bunge litabaki kuwatetea wananchi na kusema katiba haiwezi kubadilishwa kwa maslahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu?
je mahakama itatoa maamuzi ya haki kukemea yeyote anayetaka kujaribu kuchezea katiba ya wananchi?
tatizo kubwa ni kutengeneza mahakama ambayo inatokana na serikali na bunge ambalo linaingiliana na serikali.
katika hali kama hiyo unakuwepo uwezekano wa kikundi cha watu kushikilia vyombo vyote kwa maana wa nachukua serikali, katika kuunda mahakama wanawekana wao wenyewe na kama kuna muingiliano baina ya bunge na serikali basi wanaweza kutumia fursa za kuingiliana kuliteka bunge ili liwe upande wao.
hapo kikundi hiki kinaweza kufanya jambo lolote kwa maana kimeshikilia vyombo vyote vya kijamii.
hili ni jambo la msingi sana kwani kwa mfumo wa kipumbavu kama huu katika uandishi wa katiba unaweza kufanya nchi hata kutawaliwa na mashati yanayochaguliwa na wananchi lakini yakiwa yametumwa hata na watu kutoka nje ya nchi.
ni bora kama sauti za kutoka nje zina malengo ya kuingilia maamuzi tu ya nchi yenu au eneo lakini kama ni wezi wa rasilimali mtajuta.
tukiweka mifumo ambayo mfumo wa mahakama hautegemei mhimili mwingine ama kwa kupewa nafasi za kiutendaji au kupewa maslahi au maamuzi yoyote, hapo mahakama itakuwa huru kufanya maamuzi ya haki.
kama mbunge atajua anachaguliwa na wananchi na yeye hawezi kupata fursa yoyote kutoka katika mhimili mwingine bali ubunge wake umeshikiliwa na kura za wananchi atatumikia wananchi.
lakini tunatakiwa mambo haya kuyawekea mifumo ambayo walioko nje ya serikali hawawezi kutumia nguvu ya mhimili mmoja kubadili serikali lakini pia aliyeko serikali hawezi pia kutumia nguvu ya mihimili mingine kubakia ndani.
tutengeneze mifumo ambayo kila anayepata nafasi popote ajue kutumikia wananchi ndio njia pekee ya kujiimarisha.
​usilete ubabaishaji hapa unajifunzaje kwa walioshindwa???