kusema haupo upande wowote haihalishi kuwa kweli haupo upande wowote bali unachokisema kinaegemea wapi au kipo katikati ndio jambo la kuangalia.
hapa hakuna mwenye historia iliyo huru ya burundi ambayo imekubalika kwani kila mmoja akitaka kutoa historia anaangalia yale yanayoegemea upande anaousapoti ambayo ni mabaya hayasemi bali lakini mtiririko ni ule ule. hivyo historia haifai.
jambo la msingi hapa ni warundi wamechoka na vita, watanzania wamechoka na wakimbizi, jumuiya ya afrika mashariki inaathiriwa na migogoro ya burundi, afrika mpaka umoja wa mataifa hakuna anayenufaika na migogoro ya burundi labda wauza silaha.
ni jambo gani linaweza kuepusha vita burundi ndio suluhisho.
haijalishi nkulunzinza ana haki ya kuendelea na muhula wa tatu lakini kama kuendelea kwake kunaweza kuleta vurugu kwa burundi basi akae pembeni maana haki isiyotimiza wajibu haipo.
hapa tunajadili swala la burundi kwa mustakabali wa tanzania.
tunatakiwa kujua kuwa kinachozidi kuivuruga burundi ni madaraka ya raisi ya kuteua viongozi mbalimbali.
madaraka haya yanamfanya raisi kuwa na washirika wa kumuunga mkono na wakiwa tayari kuingia kwenye mapambano kwa maana wanajua kuondoka kwa nkurunziza ndio mwisho wa utumishi wao.
lakini kwa upande wa hatua iliyochukuliwa na jeshi ya kutangaza nkurunzinza asirudi ilikuwa ni hatua ya kupongeza kama hatua hiyo ingekomesha machafuko na katika mda mfupi kurudisha utawala wa kidekrasia kwa kuitisha uchaguzi.
na hivyo ndivyo vyombo vya wananchi vinatakiwa kufanya kazi kwa kuwatumikia wananchi na pale viongozi wanapotaka kuipeleka jamii kubaya kunatokea chombo chenye uwezo kuirudisha jamii katika mstari.
lakini jukumu hili la vyombo vya wananchi kutumikia wananchi linakwazwa na madaraka ya raisi kuteua kwani nani ashikilie madaraka kama hayo ya kufanya mfumo mzima uwe wake akaiacha?
lakini ukisha muondoa aliyekiuka na kurudisha kwa wananchi nani ataingia na kukuamini wewe uliyemtimua mtangulizi na kukuacha kwenye madaraka?
nani anaweza kucheza upatu kama "waziri mkuu msaidizi pekee tanzania" kukamata mpaka wakubwa lakini malipo yake tunayaona leo?
hapo ndipo mimi binafsi naamini tukitengeneza katiba ikawa nzuri kwa kuondoa mianya ya watu kujiimarisha kwa kutengeneza mitandao ya kuwasapoti bila kujali wanachokifanya kila mtu anaweza kuitumikia jamii yetu kwa uaminifu naweledi mkubwa.
Naona humu wengi tu ni kama mimi.
(Nakiri sipo vizuri kwenye masuala ya kisiasa)
Wengi hawajui nini hasa wanajadili kuhusu Burundi,
Hawajui muda wake wa urais unaisha lini, au kama uliisha ni tangu lini kwa mujibu wa kalenda yao ya uchaguzi.
Hawaelewi kuhusu katiba na madai ya PN kuhusu kugombea kwa kipindi kingine.
Yani naona ni ushabiki tuuuuuu!
Sipo upande wowote, ila kiukweli humu kuna watu wanapotosha sana kuhusu yanayoendelea.