Tetesi: Yawezekana hiki ndio kilichopelekea Kinana alalamikie Traffic

Tetesi: Yawezekana hiki ndio kilichopelekea Kinana alalamikie Traffic

Duh sisi waendesha pikipiki nikadhani ndiyo tunakiona cha moto kutoka kwa matrafic kumbe hata nyie wa magari,basi hawa jamaa WASHENZI sana
 
Marytina unajua tatizo liko wapi? Tatizo ni kuwa Kinana na wachangiaji karibu wote tuna-deal na ''dalili za ugonjwa'' badala ya ku-deal na ugonjwa wenyewe. Trust me. Trafiki polisi ni tatizo kubwa sana sikatai. Lakini hili ni tatizo linaloletwa na deep underlying problems za mfumo wetu mbovu wa uongozi na kutowajibika kwa viongozi wetu. Na siyo trafiki polisi tu, kila sekta na kila kona ya nchi yetu ina haya matatizo. Nilisikia jamaa mmoja anaelezea kisanga kilichotokea sehemu fulani ya Tanzani: Kijiji hakina maji, vijana wamejitolea kuchimba mtaro wa mabomba bure, wananchi wamechanga wakanunua mabomba, ikabakia kazi ya wahusika wa maji kwenda kuunganisha. Hawakwenda (bila sababu yoyote). Wananchi wakaenda kwa mkuu wa wilaya. Watu wa maji wakakasirika, wakawaambia wanakijiji ''si mnajifanya kushtaki, basi hatuwawekea huduma''. Mwaka umeisha na mpaka sasa wananchi hawana huduma. Na ukienda kila kona ya nchi kuna uozo mkubwa!
Ni kweli kabisa uozo uko kila kona ya Taifa hili, Hivi na TANESCO sijui tuwaweke upande gani maana kwa RUSHWA hawajambo kabisa japo askari polisi wameoza kabisa na hawana mpinzani kwa hili yaani hata Ufanyeje hakuna huduma utaipata polisi bila kutoa RUSHWA
 
Mh Kinana kakerwa na Trafiki huenda alipita hii njia kutokea Njiapanda hadi Arusha wanajipanga hivi.

Njiapanda - 4
Uchira - 4
Kawawa - 8
Mjohoroni - 2
Kiboriloni - 6
Changbay - 5
Kibosho - 4 na mmoja wakike mkalii
Mali Sita - 8
Machame - 4
Kwasadala - 11
Boma - 16
Kwa wasomali - 4
KIA - 4
King'ori - 2
Kikatiti - 6
Maji ya Chai - 12
USA - 16
Leganga - 4
Makumira - 4
Tengeru - 8
Kwa Mrefu - 8
Ngulelo - 4
Kimandolu - 4
Kwa Shabani - 6
Philips - 8
MountMeru - 2
Sanawari - 2
Mianzin - 6
Stand Kuu - 12

Ukichomoka wote hawa katambike.

😁😁😁😁😁😁
Barabara ya Njiro:
Impala Round about -4
Bia - 6
Relini - 4
Total - 4
ESAMI - 8
Round about Msola - 10

Kutoka Impala hadi Msola Round about ni 10km
 
Back
Top Bottom