Yawezekana kabisa Mungu hakukusudia kumuumba mwanamke.

Yawezekana kabisa Mungu hakukusudia kumuumba mwanamke.

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Tunaosoma maandiko wenyewe bila kusomewa na wachungaji ni wazi kuwa halikuwa kusudi la Mungu kumuumba mwanamke(Eva)

Huenda Mungu angelitupatia njia nyingine ya kuzaliana nje na kumtumia mwanamke.

Ndio maana hata baada ya Adam kushawishiwa kula tunda lile na kujificha mwenyezi Mungu alipo mtafuta (muita) na kumuuliza kwanini amekula tunda/ amejificha

Adam alijibu bila woga akimlaumu Mungu Kwa kusema "Si huyu mwanamke uliyenipa!"

Hili ni jibu la wazi Kwa Adam kuwa hakumuhitaji mwanamke kabisa kabisa ila Mungu mwenyewe ndiye alitaka hapo badae baada kuona Adam yu peke yake pengine adamu angeliulizwa kama anahitaji msaidizi sidhani kama angekubali.

Maandiko yanasema Mungu ilimpasa Adam ampe usingizi mzito sana Kisha akatoa ubavu wake na kumuumba mwanamke!

Kwanini Mungu amlaze kiumbe wake aliyemuumba yeye Kwa matakwa yake yeye mwenyewe na kwamba alikuwa na uwezo wa kumuondoa Kisha akaumba mwingine amtakae?
Hili ni swali nyeti twapaswa kujiuliza huenda isingekuwa rahisi Kwa Adam kukubali Kwa ridhaa yake atolewe ubavu Kisha aumbiwe mwenzie.

Baada ya Mungu kulaumiwa na Adamu(si huyu mwanamke uliyeniletea) Mungu hakuendelea na Adam akamgeukia mwanamke Kisha kutoa laana kama zote Kisha akarudi Kwa Adam badae sana😁😁

Na Mimi Niko hapa kukiri kwamba kama kungelikuwa na namna nyingine ya kuzaliana pasina kumtegemea mwanamke Sina uhakika kama wanaume tungekuwa tunaoa uhakika huo Sina Sina Sina kabisa.

Sipingi kuwa ndoa hazitakiwi la Bali hii ni tafakuri yangu kuhusu uumbaji huo ......Kwa maana dhma ya mwanaume kuoa ni kutaka kuwa na watoto na sio tendo pekee na Kwa ushahidi ndoa nyingi mno huvunjika Kwa sababu TU mwanamke hazai au mwanaume kuzaa nje ya ndoa ama kuongeza mke ili TU apate watoto!

Hata ndoa ya Ibrahim na sarai mke wake iliingia mchanga Hadi akazaa na beki tatu. Hii inamaanisha kuwa dhumuni kubwa la mwanaume kuoa ni kupata watoto!

Jambo la kushangaza watakuja watu kwenye Uzi huu kutukana sana pasina sababu Wala hoja ya kupinga 😹
 
Nitarudi kukuonesha kuwa mwanaume na mwanamke waliumbwa pamoja isipokuwa walidhihishwa wakati tofauti...
 
Kwa mujibu wa kitabu cha Biblia, mtu mwanamume na mtu mwanamume waliumbwa kwa wakati mmoja tena waliumbwa ili kufanana na huyo aliyewaumba, hii ipo mlango wa kwanza kitabu cha Mwanzo.

Nukuu...

Mwanzo 1
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
 
Sasa ukienda mbele kwenye sura ya pili ya Mwanzo, unakutana na vitu viwili

1. Huyo mtu aliyeumbwa ndio anadhihirishwa katika mwili...

2. Mtu maana yake ni Adam (muunganiko wa mwanamume na mwanamume), ukisoma mbele zaidi utaona hili...

Mwanzo 2
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
 
Huu mstari unaonesha namna ambavyo mwanamke anadhihirishwa katika mwili...

Mwanzo 2
21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
 
Back
Top Bottom