Kwa mujibu wa kitabu cha Biblia, mtu mwanamume na mtu mwanamume waliumbwa kwa wakati mmoja tena waliumbwa ili kufanana na huyo aliyewaumba, hii ipo mlango wa kwanza kitabu cha Mwanzo.
Nukuu...
Mwanzo 1
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.