Yawezekana kabisa Tanzania inaongozwa na watu ambao hawajawahi kabisa hata kuisoma kabisa!

Bashit sidhani Kama hata katiba ya chama chake ameisoma na kuielewa na kuiheshimu.
 
mtu akikushauri kitu cha kipuuzi akiwa anajua,na ukakifata,anakudharau-bynyerere.

mtu akikupamba ujinga(kukutia bichwa)akiwa anajua na ukafurahia tu unacheka cheka maana yake anakujua vyema kitambo kwamba wewe ni tutusa- by mimi.

huyu mana wanaofanya hayo wanamjua vyema kwamba kwamba hapindui,
mwenzake alimkazia kangi akamwambia hapana usinisifu huku unafanya ujinga.
 
Kwa taarifa yako Kasella-Bantu alibatizwa kwa jina la Joseph. Udini uliomfanya Mwalimu amtie kizuizini na amsikilize Rashidi Mfaume ni upi?

Amandla...
 
Kwa taarifa yako Kasella-Bantu alibatizwa kwa jina la Joseph. Udini uliomfanya Mwalimu amtie kizuizini na amsikilize Rashidi Mfaume ni upi?

Amandla...
Hilo suala wapaswa kujibu mwenyewe kwa faida ya wengine nimesite kisa cha kasella bantu juu ya suala la ukiukwaji wa utawala wa kisheria, hilo la udini ambalo limeamsha hisia zako sikuweka mfano wake unaweza rejea makablasha upitie namna tulivyofikishwa hapa na mwalimu kupitia udini aliouasisi pasina kutazama mbali
 
Kuisoma wanaweza kuwa wameisoma, tatizo kubwa sana na la msingi ni je wameielewa!!??

Kuna watu huwa wanasoma kila kitu kama wanasoma gazeti la KIU!!
 
Hiyo ndio bongolala,
Unaweza kuta mtu ana phd lakini hajui Hata alichosomea.
Mwambie sasa tuingie kwenye thesis tuone uko lever ipi.
Atakwambia bwamdogo twende tukanywe bia we una kiu na njaa.
Dah unaenda kunywa bia tu hamna jinsi.
 
ok tusubiri
 
Umeingiza udini mahali ambapo sipo. Haukuweka mfano kwa sababu unasema tuu kama kasuku bila kuelewa ulisemalo. Watu kama wewe ndio mnataka kutupeleka kusipo.

Amandla...
 
Hata Kiongozi au mgombea uongozi akisema, ".....nitawaletea maendeleo."; huyo ni tapeli tu, maana hakuna sehemu anapoenda kuyachukua hayo 'maendeleo' na kuwaletea wananchi.!
 
Ni kujitoa ufahamu tu. Watu wanakwambia Kila linalofanyika nchini linafanywa na Samia? Ni juzi tu wameshituka wakakubaliana hela za kujenga vyoo wasimtaje Samia maana ni aibu.
 
Wewe ulieisoma Kwa nini huiongozi kutwa kucha kulalamika kama simbilisi 🤣🤣
 
Huenda hatuongozwi, bali tunatawaliwa.

Huenda wanaotutawala na watu wajinga, wasiojua Katiba ni nini.

Huenda kwa ujinga wao, basi wanaamini kuwa uongozi ni kufuata Utashi wao na siyo kuzingatia Matakwa ya Katiba.

Na huenda kwa ujinga wao, wamewakumbatia wale wanaowasujudia na kuwalamba viatu. Na wanawachukia wale wote wanaotumia uhuru wao kuwakosoa kwa mustakabali mwema wa Nchi.
 
Umeingiza udini mahali ambapo sipo. Haukuweka mfano kwa sababu unasema tuu kama kasuku bila kuelewa ulisemalo. Watu kama wewe ndio mnataka kutupeleka kusipo.

Amandla...
Hiyo Stockholm syndrome uliyonayo sina msaada labda umtafute mwana psychology, nenda katazame kwenye files vyuo, jumuia na teuzi zilizokwaa kisiki wakati wa Mwalimu kwasababu ya udini, halafu nikushauri pia ni vyema kuwa na ustahimilivu kusikiliza usiyoyapenda kadhalika Taifa hili tiba yake ni kuambizana ukweli si kwa ulongo na mbwembwe za mtindo wa nzi kelele nyingi kufakamia mzoga wenye funza.

Chukua na hii ➡️ mwalimu alishindwa nini kurejesha mali za chama(ambazo si za chama in such kwasababu waTanganyika waliporwa kwa ulaghai) wakati ameshika uenyekiti kamuachia mzee mwinyi Ukulu, kwa dhana yake ya "Tujisahihishe"
 
Maneno mengi. Weka data hapa. Usipende kutafuniwe kila kitu. Ukweli sio kwa sababu unasema. Ukweli ni kwa sababu umeujengea hoja. Umesema Mwalimu alikuwa mbaguzi wa kidini halafu unamtolea mfano mtu aliyebaguliwa kwa sababu ya dini kumbe nae ni mmisheni kama Mwalimu.
Kwa nini umlaumu Mwalimu kwa kushindwa kurudisha mali zilizoporwa na chama chake wakati wenyeviti wote waliomfuata ( wakristu na waislamu) hawajafanya hivyo! Kama unaumie sana mwambie Mwenyekiti wa sasa afanye hivyo ili apate thawabu kwa Mwenyezi Mungu. Oh, kumbe ni Muislamu!
Btw, msomi fake, ni " as such" sio "in such".
Unataka niwe mstahimilivu? Bahati mbaya sina ustahimilivu when it comes to fools na idiots. Mpaka sasa nimekuvumilia sana. Naona niishie hapa kabla uvumilivu haujaniishia. Sita kujibu tena.

Amandla...
 
We punguani kama hukuweza kuelewa kwanini nimemuweka Bantu na T Georges kwenye mifano ya utawala bora sina lakukusaidia kwa uvivu wako wakujisomea, baki na ujinga wako na hiyo syndrome iliyokuviza
 
Hata Kiongozi au mgombea uongozi akisema, ".....nitawaletea maendeleo."; huyo ni tapeli tu, maana hakuna sehemu anapoenda kuyachukua hayo 'maendeleo' na kuwaletea wananchi.!
Hizo ni kauli za kitapeli,eti nitawaletea maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…