Inawezekana wana point maana vyote hivyo vilizuiwa na aliyemtangulia.
Kama wana pointi basi hawajui namna ya kuielezea hiyo pointi yao au si ajabu hawajui hata wanachokiongelea!
Ikumbukwe pia kwamba hata huyu Rais wa sasa naye aliendeleza hiyo marufuku ya mikutano ya vyama vya siasa kwa kisingizio cha kutaka kwanza kuushughulikia uchumi.
Walimzushia na kumbambikia Freeman Mbowe kesi ya ugaidi. Tusilisahau na hilo.
Sasa yeye kaondoa zuio hilo.
Labda ni suala la semantics….hivi kaliondoaje hilo zuio wakati hakuwa hata na mamlaka ya kuliweka?
If anything, yeye na mtangulizi wake walivunja katiba lakini kwa vile tupo vile tulivyo, hakuna aliyethubutu kumgomea na kumweleza kuwa ame/walivunja katiba.
Katika hali ya kawaida ya jamii inayojielewa, vyombo vya dola vinapaswa kugoma kutekeleza amri zisizo halali.
Rais Biden au Waziri Mkuu Sunak hawawezi tu kuamka leo na kuagiza kwamba vyama vya upinzani kwenye nchi zao ni marufuku kufanya shughuli za kisiasa kisa tu eti chaguzi zimemalizika.
Kabla mashauri hayajafika hata mahakamani, si ajabu vyama vyao kwanza vikawawajibisha vyenyewe kabla ya kufika kwenye hatua zinginezo.
Wanapokosea ni kutaka tumshukuru na kumpogeza kwa kufanya hilo. Wanakosea kwa sababu zuio lilikiuka Katiba na alichofanya ni kuheshimu Katiba.
Amandla...
At the bare minimum, Rais anapaswa kuiheshimu katiba.
Hapaswi kupongezwa na kushukuriwa kwa kufanya the bare minimum.
Nadhani kwenye kiapo cha urais huwa wanaapa kwamba watailinda, wataitetea, na wataiheshimu katiba ya nchi.
Kutokuisigina katiba ya nchi ni takwa la msingi .
Machawa sidhani kama wanalijua hilo!
Rais Samia hajaruhusu maandamano ya vyama vya siasa.
Katiba ya nchi ndo inaruhusu hayo.
Machawa ni wajinga [igoramuses] tu.
Hivi siku Rais Samia akiamua kwamba kuanzia sasa ni marufuku watu kuamini dini/ imani wanazotaka wao, na kwamba ni marufuku kwa watu kwenda kwenye nyumba za ibada [haki ya kuamini imani yoyote ile ya kidini nayo ni haki ya kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 19], halafu baada ya miaka miwili akaliondoa zuio hilo, napo atapongezwa kwa kuwaruhusu watu kuamini imani zozote zile za kidini wazitakazo?