Yawezekana watanzania wanapenda zaidi kandanda kuliko Siasa, siyo kwa nyomi hii ya Yanga hapa Mkapa

Basi vyama vianze kuanda vipindi vya youtube wasihangaike kwenda mikoani, wawe wanawambia wananchi waingie youtube
 
Lissu awe karibu na Wananchi mara ngapi? Unayajua aliyoyafanya Lissu Nchi kuwasaidia Watanzania wanyonge mbali mbali bila kudai hata senti moja?
Perspective is bias.

Unadhani Mo na Lissu nani muhimu kwa Wanasimba?
 
Yaani na kwenye Mpira ingekuwa timu moja ndo inachagua mkereketwa wake awe refa halafu Huyo refa kabla mechi haijaanza anawapiga kadi nyekundu wachezaji 7 wa timu shindani usingeona shabiki hata mmoja uwanjani bwasheee!

Kula tano mwanangu, watu wanaoshabikia mpira kwani ndio sehemu ambayo kuna haki. Huko kwenye mpira tuombe tu Magufuli asiwe na timu. Itakuwa sio ajabu timu anayoishabikia ikachukua kombe bila hata kuingia uwanjani.
 
Hio ni sababu nojawapo, ila yaliyofanyika miaka hii mitano(siasa za kuunga mkono juhudi na haya ya leo ya kuengua wapinzani na mengineyo ya siku za nyuma),yamechangia sana kuwakatisha wananchi tamaa kufuatilia mambo ya siasa.
Poleni
 
Kula tano mwanangu, watu wanaoshabikia mpira kwani ndio sehemu ambayo kuna haki. Huko kwenye mpira tuombe tu Magufuli asiwe na timu. Itakuwa sio ajabu timu anayoishabikia ikachukua kombe bila hata kuingia uwanjani.
Anayo sana ndiyo kipindi chake ubunifu wa vilabu umeongezeka hadi tukafika AFCON chuki yenu kwa Magufuli mtaugua vichomi yule ni mtendaji ni sawa na kumkaba Messi atakuacha tu.T2020JPM
 
Basi vyama vianze kuanda vipindi vya youtube wasihangaike kwenda mikoani, wawe wanawambia wananchi waingie youtube
Teh teh teh. Una point kubwa hapa. Nawapa ari hawa wanasiasa na wafuasi wao walio mstari wa mbele wawe na plans A, B, C n.k. Mfano mzuri hakuna siasa kwenye radios, magazeti na Tvs kwa takribani miaka mitano iliyopita. Lakini bado wameweza kuwafikia wananchi kwa kiwango kizuri kupitia mitandao niliyoianisha hapo juu.... Bila plan B na C wangeshatoweka kwenye ulingo wa siasa. Ni mtazamo tu.......
 
Ila siku ya kupiga kura watajitokeza na kukipa kura chama cha rangi za jezi zao.
P

Kwa taarifa yako uchaguzi huu utakuwa na wapiga kura wachache sana. Fuatilia vizuri, hamasa ya kisiasa imeshuka sana ndani ya hii miaka mitano ya Magufuli. Tulizoea vipindi moto moto vya kampeni kwenye TV, tulikuwa tunaona mijadala moto moto inayoonyesha mafanikio na mapungufu ya miaka mitano iliyoisha, na matarajio ya miaka mitano inayofuata. Midahalo kadhaa iliyopandisha hamasa. Ila sasa hivi muandishi kama ww Paskali na ww upo kwenye mijadala ya nyomi kwenye kampeni, badala ya mijadala mizito kwenye luninga ya uchaguzi!

Yaani kama taifa tumegeuzwa tunajadili burudani zaidi, kuliko kipindi kizito cha mustakabali wa maisha yetu. Cha ajabu kuanzia wasomi mpaka wasiojua kusoma tunajadili matukio badala ya issues. Nilitarajia muandishi nguli kama ww saa hii ungekuwa hata umeaandaa vipindi maalum vya uchaguzi, hasa midahalo ya wagombea kadhaa wa uchaguzi. Waandishi nguli wa nchi nyingine, wangekuwa wanajua nini wawape wananchi wao kwa wakati nyeti wa taifa kama huu. Hali hii inasikitisha na kuumiza, lakini hapo ndio Magufuli katufukisha.
 
Hio ni sababu nojawapo, ila yaliyofanyika miaka hii mitano(siasa za kuunga mkono juhudi na haya ya leo ya kuengua wapinzani na mengineyo ya siku za nyuma),yamechangia sana kuwakatisha wananchi tamaa kufuatilia mambo ya siasa.
Acha umbea loh!
 
Anayo sana ndiyo kipindi chake ubunifu wa vilabu umeongezeka hadi tukafika AFCON chuki yenu kwa Magufuli mtaugua vichomi yule ni mtendaji ni sawa na kumkaba Messi atakuacha tu.T2020JPM

Tumefika AFCON sio kwa sababu ya uwepo wa Magufuli madarakani, bali ni kwakuwa nchi za kushiriki fainali zimeongezwa. Kwa sasa nchi ni 24, toka 16 za awali. Afrika ina nchi chini ya 60, hivyo nchi 24 ni nusu kabisa ya nchi hizo. Ukiona timu inashindwa kufuzu kwenye hilo kombe ujue ni dhaifu ajabu. Tungebeba hilo kombe wangalau utetezi wako ungekuwa na maana, sio hiyo kushiriki bila kushinda hata mechi moja.
 
Kuna mambo mengine katika maisha yana umuhimu mkubwa sana kuliko kwenda kuangalia mpira.

Uko sahihi kabisa, na kila jambo linategemea muhusika linafaida au anapa hasara gani, hata siasa si lazima wote wapende CCM kama ambavyo sio lazima wote wapende Chadema.

Na hakuna mpumbavu kwa kuwa amependa chama ambacho wewe hukipendi. Na hiyo ndio Demokrasia ya maisha.

KUCHAGUZI KITU AU JAMBO LENYE MANUFAA KWAKO.
 
Siasa haina mvuto kutokana na kukosa fair ground. Watu wanaona bora wakaangalie mpira tuu. Huko kwenye siasa CCM inataka kila siku yenyewe ishinde tuu hata kwa kutumia nguvu sasa kuna siasa tena hapo.
 
Reactions: BAK
Siasa haina mvuto kutokana na kukosa fair ground. Watu wanaona bora wakaangalie mpira tuu. Huko kwenye siasa CCM inataka kila siku yenyewe ishinde tuu hata kwa kutumia nguvu sasa kuna siasa tena hapo.
Hiyo 'fair ground' inapiganiwa... Hauletewi kwenye kisahani. Yaani upinzani ukianza kukata tamaa sababu ya vitu ambavyo si muhimu sana ( kama Segerea hakukuwa na nyomi na kadhalika) badala ya kunadi sera za maendeleo na kuzisambaza kwa njia mbalimbali. Mtashindwa uchaguzi asubuhi hii wakati bado mna miezi miwili ya kampeni......
 
WANAMCHI WAMERIDHIKA NA KAZI YA JPM SASA WAHANGAIKIE NINI TENA?
TUKUTANE OCTOBER 28
 
Sipati picha nyomi kama hii ikisheheni kwenye mkutano wa chama cha siasa hali itakuwaje huko mitandaoni.

Je, mapenzi ya vilabu vya mpira hasa Simba na Yanga yanazidi yale ya vyama vya siasa?

Maendeleo hayana vyama!

Ni Mbwiga ( Mshamba ) tu pekee na Mtu asiyejua Masuala ya Mpira na pia siyo Mfuatiliaji angeshangaa 'Nyomi' la leo la wana Yanga SC pale Benjamin Mkapa Stadiium. Wana Yanga SC leo wamejitokeza kwa wingi ule kwa sababu Kuu zifuatazo...

1. Hasira za Michambo ya Msemaji wa Simba SC Haji Manara kuwa hawana Ubavu wa Kujaza Uwanja.
2. Kuaminishwa Kwao na Uongozi wao lakini hasa hasa Wadhamini GSM kuwa sasa nao Wamesajili Majembe na wana Jeuri ya Pesa.
3. Wana Yanga SC wamejitokeza kwa wingi vile ili Kuwaangalia na Kuwathibitisha Wachezaji Wao wapya waliosajiliwa na kupokelewa kwa Nyodo
4. Hamasa Kubwa kutoka katika Vyombo mbalimbali vya Habari nayo imechangia Kuujaza Uwanja
5. Mafanikio ya Simba SC ambayo Kwao Yanga SC imekuwa ni Kero na Karaha hivyo nao wametaka Kujitutumua Kujazana ili Kuwajibu Simba SC
6. Uwepo wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ( ambaye ni mwana Yanga SC ) Mwenzao umechochea Mashabiki wengi Kujitokeza kwa Umati
7. Ujio wa Msanii Harmonize ( Konde Boy ) ambaye ni Mshindani mkubwa wa Diamond ( mwana Simba SC ) nao ni Kichocheo cha Kujazana

Yangu ni haya tu!
 
Tuache kwenda Kwenye Yanga tukasikilize siasa za Bongo [emoji2]
Tunasubiri hio siku mtu ashinde aingie ikulu basi.Mambo mengine watajijua wenyewe
 
Nimekuelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…