Yawezekana Zanzibar hawahitaji Katiba Mpya sasa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hii ni tafakuri ya wazi kufahamu tunasimama wapi.

Zanzibar kunazidi kunoga. Bila shaka uchumi wao ukiwamo wa mtu mmoja mmoja kwa sasa unazidi kupaa kwa kasi kuliko popote duniani.

Washukuriwe marais Mwinyi na Samia wana shupavu wa kitanzania.

Uvuvi wa majahazi unaondoshwa na wavuvi sasa kutumia maboti ya kisasa kama Ulaya.

Kwasemekana, Zanzibar kwaja jengo refu zaidi kuwahi kuonekana Afrika mashariki na kati.

Barabara, viwanja vya ndege, Bandari nk, vilinganishwe na vya wapi?

Bei za vitu, mfumuko wa bei nk, mwangwi wake hausikiki kutokea Zenji. Hivi huko hata tozo za Dk. Mwigulu nako zipo?

Wao wanapata ajira serikalini kwa quota isiyokuwapo kokote bara. Wanapata mgao wa mikopo na misaada kutoka nje kwa quota isiyokuwapo bara. Wanapata mgao wa mapato ya ndani kwa quota isiyokuwapo popote. Nk nk.

Kwa hakika kwa hali hii, kwa wazanzibari kipaumbele ni kukuza uchumi na maendeleo yao kwanza. Kukamata fursa zao au kuchukua chao mapema.

Kwa mtaji huu watake katiba mpya yenye kuyaweka rehani hayo ya nini?

Labda hiyo ije wakati rais JMT siyo Mama Samia.

Haina shaka kuwa utulivu tunaouona, ni matokeo ya maajabu ya hali ya uchumi unavyoendelea kushika nafasi yake huko.

--------
Nyuzi ambatanishwa:

Zanzibar Wavuvi wapewa Boti za Kisasa, Bara kulikoni?
 
Kisiwa kitazama..naona mmeanza kukiongezea unnecessary uzito.

#MaendeleoHayanaChama
 
Zanzibar wameichoka CCM, hawahadaiki na vitu vidogo.

Leo Zanzibar hawana issue na mfumuko wa bei, hawana tozo za mwigulu, uchumi wao unapaa katika kila sekta. Habari njema kabisa kwao.

Zanzibar walikuwa hapa:

Your browser is not able to display this video.


Leo kimyaaaa! Si Pemba, ACT, CUF, wala Jussa. Habari njema kabisa pia.

Nini kimebadilika?

Si kuwa ni uwepo wa rais JMT ambaye ni mzanzibari ndiyo iliyo tofauti kuu leo? Bila shaka wangependa ikiwezekana hali hii idumu milele?

Hali hii inaweza kudumu milele katika katiba ya sasa peke yake. Kwanini watake mpya?
 
Wazanzibari hasa wapemba kwasasa sijui msimamo wao uko wapi, ACT wamewavuruga wamejikuta wanaongozwa kupelekwa wasipopajua, mpaka watakaposhtuka usingizini ndio wajue wanataka kuelekea wapi na kiongozi wa safari yao awe nani.
 
Kisiwa kitazama..naona mmeanza kukiongezea unnecessary uzito.

#MaendeleoHayanaChama

Kazi ya ubongo ni kutafakari mkuu.

Kuwaza na kuwazua ni sehemu ya ubinadamu na hasa inapokuwa kwenye kuwamba ngoma, ngozi inapokuwa inakokotwa sana.

Ilikuwa Chatto leo Zanzibar. Utamaduni huu unaweza kuwa na madhara makubwa.

Kuzama si Zanzibar tu bali hata bara kunaweza kuzama. Si nasi twapakana na bahari na maziwa pia yakhe?
 
Wazanzibari hasa wapemba kwasasa sijui msimamo wao uko wapi, ACT wamewavuruga wamejikuta wanaongozwa kupelekwa wasipopajua, mpaka watakaposhtuka usingizini ndio wajue wanataka kuelekea wapi na kiongozi wa safari yao awe nani.

Hili si la ACT bali Zanzibar kumenoga mjomba. Yameangaziwa zaidi kwenye uzi huu:

Zanzibar Wavuvi wapewa Boti za Kisasa, Bara kulikoni?

Wazanzibari kwa umoja wao ni wa kupongezwa. Subira yao imewalipa. Huu ni muda wao sasa.

Kutaka katiba mpya ni kujaribu kuwatemesha minofu mdomoni.

Kwa kweli walivumilia mno.
 
Wazanzibar wana ushirikiano na muhali ( kulindana ) wa hali ya juu sana. KAMWE hawawezi kudai KATIBA MPYA kwa sasa kwa kuwa mwenzao ndio anatawala TANGANYIKA. Subirini mwaka 2030 huko mwenzao akiwa anamalizia muda wake.
 
Wazanzibar wana ushirikiano na muhali ( kulindana ) wa hali ya juu sana. KAMWE hawawezi kudai KATIBA MPYA kwa sasa kwa kuwa mwenzao ndio anatawala TANGANYIKA. Subirini mwaka 2030 huko mwenzao akiwa anamalizia muda wake.

Siyo 2030 mkuu. Kumbuka Mwinyi jnr ni rais JMT kazini 2030 - 2040.

Wangependa hata baada ya 2040 awe mzanzibari pia.

Haitakuwa ajabu kama wanakolenga kuanzia sasa ni wao vinginevyo kila mtu achukue njia yake.

Hii ndiyo imetoka hivyo.

Ninakazia: Karume Snr, Samia na Billal waliona mbali sana. Wakasubiri.

Kwa hakika wanastahili pongezi.
 
napita tu

Katika watu wakieleweka kwenye kudai katiba mpya, walikuwa wapemba (Jussa ndani). Sina hakika clip hii ni ya lini.

Hata hivyo na rais JMT mzanzibari? Damu ni nzito kuliko maji.

Kwani Zanzibar kuna tozo za Mwigulu? Bei za mafuta Zanzibar huko ziko je? Na mengi ya wazi.

Si kuwa Zanzibar ina vyote vya kupata kwa hali iliyopo? Tuliyoyaona Chatto si tunayaona leo Zanzibar?

Mzungu baada ya kaburu kuachia nchi kwa weusi SA, kwani atakuja ipewa lini tena?

Wazanzibari kwa umoja wao, wanaweza hata kutuhadaa sote. Wenyewe wakiita kula na vipofu yakhe. Wanajua wanachotaka na namna ya kukipata.

Mbona nafasi ya kugeuka Ulaya au Dubaii ni hii.

Ukweli mchungu!
 
O
Hua wanajifanyiaga mambo yao...

Zamu yao hii mkuu. Tokea 1964 hadi leo wao wamekalia kiti kwa miaka kumi tu, tena wakati huo kiongozi Zanzibar hakuwa na madaraka kama leo.

Leo wameshika kote baada ya subira kuu ya kupigiwa mfano.

Kwanini tusiisome namba? Kwa hakika wakiipoteza nafasi hii wajilaumu wenyewe.

Tutachezana shere hapa ikiwezekana hadi 2050. Ya kaburu na mtu mweusi SA, mbona yametukuta sisi Ya Rabi?

Habari ndiyo hiyo.

Cc: Jumbe Brown
 
Unayakuza mambo kihisia......
 
Unayakuza mambo kihisia......

Jambo gani nilikuze mkuu? Kwani wasikia mwangwi gani toka kwa wenzetu? Yako vipi haya:

1. Mfumuko wa bei?
2. Kupanda kwa bei ya mafuta?
3. Tozo za hovyo hovyo kama za Mwigulu?
4. Makali ya UVIKO 19?
5. Nk.

Zanzibar kuna mahoteli yaliungua moto. Nje ya utaratibu wa bima wenyewe walilipwa.

Kwetu kadhia za matetemeko si wakumbuka?

Maboti ya kisiasa ya uvuvi kutoka kwenye majahazi tumeyasikia.

Majengo marefu na rekodi zake tumesikia nk nk.

Hatupaswi kutambua kuwa sasa hivi Zanzibar kama Chatto wameshika hatamu? Waziachie vipi hatamu hizo kirahisi?

Haya si mambo ya kuyaelewa tu mkuu?
 
Kwani kampuni ya AICL na XCasia zilizotengewa DOLA BILIONI 1.3 kujenga ghorofa 72 huko Zanzibar zimetengwa na kupitishwa na bunge la JMT?!!!
 
Kwani kampuni ya AICL na XCasia zilizotengewa DOLA BILIONI 1.3 kujenga ghorofa 72 huko Zanzibar zimetengwa na kupitishwa na bunge la JMT?!!!

Wewe hujui misaada na Mikopo nchi iliyopokea kutoka nje kuna quota imeenda Zanzibar katika proportions ambazo sisi hatukushirikishwa? Hii pia ni hivyo kwa mapato yetu ya ndani.

Pamoja na mapato yetu yaliyochukuliwa juu kwa juu, nani asiyejua kuwa kwenye kulipa mikopo hiyo hata quota ya Zenji na sisi inatuhusu?

Hata kwa kuangalia quotas hizo per capita. Si kuwa sisi tumebebeshwa zigo la miba kweli kweli?
 
Hizi quotas zimeanza awamu hii ya 6 ?!!!!😳😳

Vipi kuhusu 4% ya mgawanyo wao?!!!

Wamekuwa wakiupata kila mwaka ?!!!
 
Hizi quotas zimeanza awamu hii ya 6 ?!!!!😳😳

Vipi kuhusu 4% ya mgawanyo wao?!!!

Wamekuwa wakiupata kila mwaka ?!!!

Yote hayo ni mgogoro mkuu.

Kwa nini kwa mkopo uliochukuliwa na nchi per capita wazanzibari wachukue zaidi. Kwenye kulipa wao walipe kidogo zaidi.

Kwanini mapato ya ndani yatoke bara kwenda Zanzibar lakini si Zanzibar kuja bara?

Wewe unaona kupo fair hapo?

Kwanini kuuweka rehani utaratibu lucrative Zenji kama huo? Huo ndiyo msingi wa hoja.
 
Hukumuelewa alichozungumza alisema Zanzibar inaelemewa na uzito hasa litakapojengwa hilo jengo refu Afrika mashariki. Niliwahi kusoma ripoti moja ya mabadiliko ya tabia nchi ileleza kwamba kisiwa cha Zanzibar sio Pemba kinaweza kutoweka ndani ya miaka mia ijayo usiseme ni mimi ninayetabiri tafuta kwenye majarida ya tabia nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…