Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 2,369
- 1,775
Lita ya petroli kwa sasa ni zaidi ya shilingi 2640.Tofautisha wabara na CCM pamoja na walio madarakani ambao hawatataka katiba mpya lije jua au ije mvua. Hao ndiyo walio walamba asali.
Tutambuane, nani ni nani katika kudai Katiba mpya
Si kweli kuwa wabara tumekuwa tunashangaa madai ya katiba mpya bali tumekuwa bega bega na tunaendelea kuidai kwa kasi ile ile.
Swali la msingi:
"Kwa kauli yako hiyo ina maana harakati za madai ya katiba mpya sasa ndiyo basi tena?"
Hata hivyo nikushukuru kwa kutambua kuwa hata sisi hatuna tatizo na mafanikio yenu au ya awaye yote. Pamoja nayo ingependeza zaidi tukajua japo kwa namba. Vipi huko kwenu:
1. Lita moja ya petrol ni shs ngapi?
2. Lita moja ya diesel ni shs ngapi?
Kwamba:
(a) Majahazi kwenu yaenda kuwa historia huo ni ukweli na utekelezaji wake ushaanza. Jambo la kupigiwa mfano kabisa kote Afrika, Asia, South na Central America.
(b) Kwamba wazee wote kwenu wanalipwa mishahara hili nalo la kupigiwa mfano duniani kote.
Kwa hakika mko kwenye right track. Huku si ndiko kulamba asali?
Kwenye haya mengine kwanini tusiungane sote kuona kuna usawa wa migao ya fursa zote (mikopo, misaada, mapato, ajira nk)? Yaani ikawa per capita, ukiwamo ulipaji wa madeni?
Suala la jahazi kuondoka sijalisikia ila, kama nilivyosema, ningependa kuona hilo likitendeka.
Wazee hawalipwi mshahara ila wanapewa fursa za ustawi wa jamii kama shiligi 20,000.
Ama kuhusu hayo mengine sidhani kwamba kutakuwa na usawa ila kinachotakiwa ni kila mtu kupata haki anayostahiki kulingana na sheria na taratibu tulizojiwekea wenyewe, jambo ambalo sasa halifanyiki.