- Thread starter
- #61
Mkuu nazungumzia taasisi ya urais ambayo hushikiliwa na mtu/watu. Unataka kunambia Nyerere alimwambia aachane na Zanzibar? Ikitokea kuwa hivyo maneno yangu ya kwamba mama atakuwa anafanya mambo yaliyowashinda wengine itakuwa na mashiko. Siamini hoja hiyo.
Hili la kujenga kwao awamu hii sijaliona, huenda nahitaji ushahidi.
Hili nalo linataka ushahidi. Hivi ninaweza kupata Umakonda na Usabaya kwenye awamu hii?
Huku kwetu mvua zinanyesha napaswa kukimbilia jahazini kutoa maji. Nina ndoto siku jahazi zikihama niweke moja makumbusho kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Mkuu rais ni mtu wala siyo taasisi. Lugha ya kudai hiyo ni taasisi ni yenye nia ovu iliyoanza kushika kasi kutokea awamu ya tano:
Kama CCM siyo adui, mchawi wetu ni nani?
Tofauti ya awamu ya 6 na ya 5 bila tume ya ukweli na maridhiano inakuwa haipo.
Watu walewale waliofanya maovu, wangalipo, huru maofisini mwao biashara kama kawaida.
Maovu yale yale yangalipo.
Kuna wafungwa wa kisiasa magerezani, kuna kesi za kubambikiziana mahakamani, haki nyingi za watu ikiwamo za kisiasa zingali ni haramu, nk.
Business as usual.
Utake ushahidi gani zaidi ya huo?