Yawezekana Zanzibar hawahitaji Katiba Mpya sasa

Yawezekana Zanzibar hawahitaji Katiba Mpya sasa

Hukumuelewa alichozungumza alisema Zanzibar inaelemewa na uzito hasa litakapojengwa hilo jengo refu Afrika mashariki. Niliwahi kusoma ripoti moja ya mabadiliko ya tabia nchi ileleza kwamba kisiwa cha Zanzibar sio Pemba kinaweza kutoweka ndani ya miaka mia ijayo usiseme ni mimi ninayetabiri tafuta kwenye majarida ya tabia nchi

Kama vinaweza kuzama, kumbe vyaelea hivyo vyaweza pia kuhama vilipo.

Kwa mukthadha wa hoja haikuwa rahisi kumwelewa ndugu mjumbe.

Cc: jiwe angavu
 
Katiba mpya ya kuendelea kuburuza na kukandamiza Wazanzibari? Ondoeni kwanza jeshi la uvamizi, Zanzibar inataka mamlaka kamili.

Asante kwa jibu lako. Kwamba wazanzibari hamuoni tena umuhimu wa katiba mpya tuliyokuwa tukiidai sote wala si zamani.

Hivi ndugu Bepari2020:

1. Kwani mkuu Muungano una faida gani kwa mtu yeyote wa bara?

2. Kwa hali ilivyo sasa, Zanzibar si ni mnufaika mkubwa wa Muungano huu kwa kila hali?

3. Tangia Samia aingie madarakani kwani zingalipo chokochoko zozote tena zenye viashiria vya kutoridhika na Muungano huu kutokea Zanzibar?

4. Si kuwa Muungano kwa wazanzibari ni muhimu tu, kama rais JMT ni mzanzibari?

Mwongozo wako tafadhali.
 
Kazi ya ubongo ni kutafakari mkuu.

Kuwaza na kuwazua ni sehemu ya ubinadamu na hasa inapokuwa kwenye kuwamba ngoma, ngozi inapokuwa inakokotwa sana.

Ilikuwa Chatto leo Zanzibar. Utamaduni huu unaweza kuwa na madhara makubwa.

Kuzama si Zanzibar tu bali hata bara kunaweza kuzama. Si nasi twapakana na bahari na maziwa pia yakhe?
Wakati mwingine choyo na roho mbaya inaweza kukuua. Ni kipi hasa kikubwa ilichopata Zanzibar kiasi cha kushughulisha watu wakawa hawalali? Hii nchi ambayo ina ardhi chini ya 1/1000 ya Bara, na rasilmali nyengine kedekede leo boti za uvuvi Zanzibar zinaumiza watu roho. Watu hawa ndo wenye mawazo ya kwamba Zanzibar ni nchi ya kutawaliwa tu.

Wanadhani udogo wa ardhi ndio kigezo cha kuitawala nchi. Ni hawahawa waliosema Rwanda na Burundi zichukuliwe na Tanzania ili kuzidhobiti; leo zimejiunga tu EAC zinawendesha.

Zanzibar na maendeleo yake ilikuwepo na itaendelea kuwepo iwe kwenye huu muungano au nje ya Muungano. Kwa kawaida zumari ikipigwa Zanzibar hudemka walioko maziwa makuu. Waliosema haya hawakukosea.
 
Ndugu Zawadini ni kweli kuwa Zenji labda ni 1/1000 kwa ukubwa bila kusahau ulinganifu wa idadi ya watu. Ila kwa haya, labda utusaidie wewe:

1. Tozo za Mwigulu ziko huko kwenu pia?
2. Bei ya mafuta ya kula, magari na m
fumuko wa bei vikoje huko kwenu?

Haya tunayajua:

1. Wazee wote kwenu wanalipwa mishahara.
2. Wenzetu mu mbioni kuachana na majahazi.
3. Wenzetu mnapata mgawo spesheli wa mapato yakiwamo ya ndani (hata kutokea Mbeya), mikopo na misaada toka nje kwa quota ambazo kwingine hamna.

4. Kuna majengo marefu kabisa yaja kwenu na uchumi wa buluu umeshika kweli kweli..
5. Mna fursa za ajira kwa quota JMT.
6. Nk nk.

Mambo ya kheri kabisa. Bila shaka kama yaliyowahi kujiri Chatto.

Hayupo anayesema kuwa haya ni mabaya au hata kulalamika. Haieleweki ni kwa vipi wewe uone tuna choyo au hata roho mbaya.

Hoja ya msingi ni:

"Je, wazanzibari mngali mnataka katiba mpya au kipaumbele kimebadilika?"

Ni hilo tu ndugu mjumbe.
 
Ndugu Zawadini ni kweli kuwa Zenji labda ni 1/1000 kwa ukubwa bila kusahau ulinganifu wa idadi ya watu. Ila kwa haya, labda utusaidie wewe:

1. Tozo za Mwigulu ziko huko kwenu pia?
2. Bei ya mafuta ya kula, magari na m
fumuko wa bei vikoje huko kwenu?

Haya tunayajua:

1. Wazee wote kwenu wanalipwa mishahara.
2. Wenzetu mu mbioni kuachana na majahazi.
3. Wenzetu mnapata mgawo spesheli wa mapato yakiwamo ya ndani (hata kutokea Mbeya), mikopo na misaada toka nje kwa quota ambazo kwingine hamna.

4. Kuna majengo marefu kabisa yaja kwenu na uchumi wa buluu umeshika kweli kweli..
5. Mna fursa za ajira kwa quota JMT.
6. Nk nk.

Mambo ya kheri kabisa. Bila shaka kama yaliyowahi kujiri Chatto.

Hayupo anayesema kuwa haya ni mabaya au hata kulalamika. Haieleweki ni kwa vipi
wewe uone tuna choyo au hata roho mbaya.

Hoja ya msingi ni:

"Je, wazanzibari mngali mnataka katiba mpya au kipaumbele kimebadilika?"

Ni hilo tu ndugu mjumbe.
Nianze na hii katiba. Wazanzibari wamekuwa wakililia katiba mpya wakati Wabara wakiwashangaa wakati huo wakifaidi keki ya taifa.

1. Kuhusu tozo na mafuta ya kula hili ni swala la kodi ambalo ni la muungano hivyo ni sawa na Tanganyika. Ni hivyohivyo kwa mafuta ya kula ambayo yanahusu pia kodi ya mapato

2. Wazee wetu wanalipwa kweli fursa za ustawi wa jamii tokea mapinduzi 1964 kabla ya muungano. Hii ilikuwa sera ya ASP
.
3. MAJAHAZI yapo ila nitafurahi siku moja tukiachana nayo kwa uvuvi.

4. Mgao tunastahiki kupata. Huu unatokana na kodi ya mapato ya muungano. Hata hivyo ndo inatakiwa. Ingekuwa vema kama ningekusikia huko nyuma ukikumbusha tawala zilizopita juu ya Zanzibar kukoseshwa.

5. Majengo marefu ni uwekezaji kutoka nje. Hauna uhusiano na kodi. Hailingani na Bara kujenga bandari Bagamoyo?

6. Quota ya ajira ipo kwenye makaratasi. Haijawahi kutekelezwa na haitotekelezwa kwasababu ya choyo.

Nimeona niseme hayo machache,huenda yako mengi.

Zawadini.
 
Hii ni tafakuri ya wazi kufahamu tunasimama wapi.

Zanzibar kunazidi kunoga. Bila shaka uchumi wao ukiwamo wa mtu mmoja mmoja kwa sasa unazidi kupaa kwa kasi kuliko popote duniani.

Washukuriwe marais Mwinyi na Samia wana shupavu wa kitanzania.

Uvuvi wa majahazi unaondoshwa na wavuvi sasa kutumia maboti ya kisasa kama Ulaya.

Kwasemekana, Zanzibar kwaja jengo refu zaidi kuwahi kuonekana Afrika mashariki na kati.

Barabara, viwanja vya ndege, Bandari nk, vilinganishwe na vya wapi?

Bei za vitu, mfumuko wa bei nk, mwangwi wake hausikiki kutokea Zenji. Hivi huko hata tozo za Dk. Mwigulu nako zipo?

Wao wanapata ajira serikalini kwa quota isiyokuwapo kokote bara. Wanapata mgao wa mikopo na misaada kutoka nje kwa quota isiyokuwapo bara. Wanapata mgao wa mapato ya ndani kwa quota isiyokuwapo popote. Nk nk.

Kwa hakika kwa hali hii, kwa wazanzibari kipaumbele ni kukuza uchumi na maendeleo yao kwanza. Kukamata fursa zao au kuchukua chao mapema.

Kwa mtaji huu watake katiba mpya yenye kuyaweka rehani hayo ya nini?

Labda hiyo ije wakati rais JMT siyo Mama Samia.

Haina shaka kuwa utulivu tunaouona, ni matokeo ya maajabu ya hali ya uchumi unavyoendelea kushika nafasi yake huko.

--------
Nyuzi ambatanishwa:

Zanzibar Wavuvi wapewa Boti za Kisasa, Bara kulikoni?
Katiba ya nini tena wakati Hangaya anawalambisha asali
 
Asante kwa jibu lako. Kwamba wazanzibari hamuoni tena umuhimu wa katiba mpya tuliyokuwa tukiidai sote wala si zamani.

Hivi ndugu Bepari2020:

1. Kwani mkuu Muungano una faida gani kwa mtu yeyote wa bara?

2. Kwa hali ilivyo sasa, Zanzibar si ni mnufaika mkubwa wa Muungano huu kwa kila hali?

3. Tangia Samia aingie madarakani kwani zingalipo chokochoko zozote tena zenye viashiria vya kutoridhika na Muungano huu kutokea Zanzibar?

4. Si kuwa Muungano kwa wazanzibari ni muhimu tu, kama rais JMT ni mzanzibari?

Mwongozo wako tafadhali.

Unakosea unapoongelea muungano. Hakuna muungano, kuna vamizi. Ukishaelewa uvamizi uliotokea, utaona Zanzibar kamwe haiwezi kufaidika kama nchi iliyovamiwa. Ndiyo maana umaskini umeongezeka na majeshi yenu yanamwaga damu za Wazanzibari tangu mwaka 1964.
 
Tuko pamoja mkuu.

Kama kuna uvamizi unaonaje umuhimu wa katiba mpya itakayoondoa uvamizi?

Kulikoni wenzetu hamna haja tena na katiba mpya?
 
Tuko pamoja mkuu.

Kama kuna uvamizi unaonaje umuhimu wa katiba mpya itakayoondoa uvamizi?

Kulikoni wenzetu hamna haja tena na katiba mpya?
Hiyo katiba mpya ndiyo inasema hivyo? Kila siku tunasikia katiba mpya inaleta serikali 3 siyo Zanzibar kupata mamlaka kamili.
 
Hiyo katiba mpya ndiyo inasema hivyo? Kila siku tunasikia katiba mpya inaleta serikali 3 siyo Zanzibar kupata mamlaka kamili.

Kwa hiyo katiba ndiyo mmeachana nayo kwa sababu haitoi mamlaka kamili japo mapema mkiidai?

Kwani nini kimebadilika basi?
 
Nianze na hii katiba. Wazanzibari wamekuwa wakililia katiba mpya wakati Wabara wakiwashangaa wakati huo wakifaidi keki ya taifa.

1. Kuhusu tozo na mafuta ya kula hili ni swala la kodi ambalo ni la muungano hivyo ni sawa na Tanganyika. Ni hivyohivyo kwa mafuta ya kula ambayo yanahusu pia kodi ya mapato

2. Wazee wetu wanalipwa kweli fursa za ustawi wa jamii tokea mapinduzi 1964 kabla ya muungano. Hii ilikuwa sera ya ASP
.
3. MAJAHAZI yapo ila nitafurahi siku moja tukiachana nayo kwa uvuvi.

4. Mgao tunastahiki kupata. Huu unatokana na kodi ya mapato ya muungano. Hata hivyo ndo inatakiwa. Ingekuwa vema kama ningekusikia huko nyuma ukikumbusha tawala zilizopita juu ya Zanzibar kukoseshwa.

5. Majengo marefu ni uwekezaji kutoka nje. Hauna uhusiano na kodi. Hailingani na Bara kujenga bandari Bagamoyo?

6. Quota ya ajira ipo kwenye makaratasi. Haijawahi kutekelezwa na haitotekelezwa kwasababu ya choyo.

Nimeona niseme hayo machache,huenda yako mengi.

Zawadini.

Tofautisha wabara na CCM pamoja na walio madarakani ambao hawatataka katiba mpya lije jua au ije mvua. Hao ndiyo walio walamba asali.

Tutambuane, nani ni nani katika kudai Katiba mpya

Si kweli kuwa wabara tumekuwa tunashangaa madai ya katiba mpya bali tumekuwa bega bega na tunaendelea kuidai kwa kasi ile ile.

Swali la msingi:

"Kwa kauli yako hiyo ina maana harakati za madai ya katiba mpya sasa ndiyo basi tena?"

Hata hivyo nikushukuru kwa kutambua kuwa hata sisi hatuna tatizo na mafanikio yenu au ya awaye yote. Pamoja nayo ingependeza zaidi tukajua japo kwa namba. Vipi huko kwenu:

1. Lita moja ya petrol ni shs ngapi?
2. Lita moja ya diesel ni shs ngapi?

Kwamba:

(a) Majahazi kwenu yaenda kuwa historia huo ni ukweli na utekelezaji wake ushaanza. Jambo la kupigiwa mfano kabisa kote Afrika, Asia, South na Central America.

(b) Kwamba wazee wote kwenu wanalipwa mishahara hili nalo la kupigiwa mfano duniani kote.

Kwa hakika mko kwenye right track. Huku si ndiko kulamba asali?

Kwenye haya mengine kwanini tusiungane sote kuona kuna usawa wa migao ya fursa zote (mikopo, misaada, mapato, ajira nk)? Yaani ikawa per capita, ukiwamo ulipaji wa madeni?
 
Zanzibar kuna katiba nzuri

Kwa sasa Zanzibar wanawajibika kwa katiba 2. Ya Zanzibar na ya JMT.

Hakuna shaka kuwa ya kwao ni nzuri. Ila hili koti la Muungano.

Ila kama koti la Muungano nalo ghafla liko vizuri, ndipo msingi wa hoja ulipo.

Anayelamba asali ni nadra kuwa mwenzako.
 
Back
Top Bottom